Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Mhe. Stephen Wasira anaanza kuiongoza CCM kama Makamu Mwenyekiti akiwa na umri wa miaka 80. Pengine, huu ni umri mkubwa sana kwa mtu yeyote kupewa uongozi wa juu katika chama cha siasa. Inawezekana kabisa kuwa Wasira atakuwa kiongozi wa kwanza mwenye umri mkubwa zaidi kushika nafasi ya juu ndani ya CCM baada ya Rashid Mfaume Kawawa.
Pengine watu wengi watauliza, inakuwaje CCM wameamua kumteua mtu wa umri wa miaka 80 kuwa Makamu Mwenyekiti? Kwa kawaida huo ndio utamaduni wa vyama dola vyote duniani ambavyo havitegemei kushinda chaguzi zao kwa njia za kidemokrasia. Vyama dola ni vile ambavyo majeshi yote huwa sehemu ya chama ya chama ama kwa kificho ama cha wazi.
Siasa za vyama dola huendeshwa na nguvu za majeshi (Jeshi, Polisi, Usalama wa Taifa, nk). Dola au majeshi hufanya kila kitu lakini wao huhitaji taswira (figure) ya kisiasa kwa ajili ya kugonga muhuri maamuzi yaliyofanywa kijeshi au kiimla. Kwa kawaid, mikakati katika vyama dola hufanywa katika matawi ya majeshi. Hata viongozi wa vyama dola hupata mafunzo yote ya kijeshi, usalama au ujasusi. Lakini mafunzo hayo hayalengi katika kujenga uwezo wa vijana kujenga hoja zenye nguvu, bali katika kujenga nguvu zenye hoja.
Viongozi wa kisiasa katika vyama dola huanza kuandaliwa katika matawi maalum ya usalama na kisha kupelekwa kufanya mazoezi katika nafasi za umma: Katibu Tawala wa Wilaya DAS; Mkurugenzi wa Halmashauri, DED; Mkuu wa Wilaya, DC; Mkuu wa Mkoa, RC; nk.
Lakini pia, minyukano ndani ya CCM inaweza kuwa imepelekea wachague mtu mwenye umri mkubwa sana ili awapitishe katika kipindi cha mpito kuelekea Uchaguzi Mkuu. Mtu huyo pia atawavusha katika kipindi pasipo kugawanyika. Lakini baada ya Uchaguzi Mkuu kumalizika, hapo ndipo ataletwa katika nafasi hiyo mtu ambaye ameandaliwa au anaandaliwa. Lakini kwa hali ilivyo sasa, huyo aliyeandaliwa au pia anayeandaliwa kama jina lake lingeletwa mbele ya wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na baadaye Mkutano Mkuu, angechafua kabisa hali ya hewa ndani ya CCM.
Kama uchambuzi huu wa Askofu Mwamakula kwako hauna mashiko, achana nao badala yake ungana naye kumpongeza Stephen Wasira kwa kuteuliwa hatimaye kupigiwa kura na Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM kushika wadhifa wa Makamu Mwenyekiti Bara. Moja ya sifa kuu ambayo naweza kumpa Wasira ni unyenyekevu wake. Katika vikao vya kidemokrasia ambavyo tumewahi kushiriki pamoja, hakuwahi hata siku moja kuninyanyapaa kwa sababu ya umbile hili.
Askofu Mwamakula anatoa pongezi kwa Mhe. Wasira kwa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara. Je, wewe una neno lo lote kwa Mhe. Stephen Wasira?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 18 Januari 2025; saa 1:20 usiku