Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Mbele ya mwili wa Jenista Mhagama na kabla hajazikwa kiongozi mkubwa katika moja ya mihimili alinukuliwa akisema Victor Mhagama, mtoto wa Jenista arithi Ubunge wa Jimbo la Peramiho. Hii ilikuwa kampeni tosha na hivyo Victor hakuhitaji kupiga kampeni yeyote achilia mbali kutoa takrima.
Mara baada ya Victor 'kushinda' katika kura za maoni ndani ya CCM, TAKUKURU wameibuka na tuhuma za rushwa! Hii inaleta tafsiri gani?
1. Tafsiri ya kwanza ni kuwa, wakubwa walitaka kuwaonyesha Wangoni wa Peramiho kuwa wao wanawajali sana. Hivyo walifanya hivyo kama kiini macho tu lakini walijua watafanya njia ya 'kumnyofoa'! Kwa hiyo, hii ndio njia ya kumtosa ili wasiwe na lawama.
2. Tafsiri ya pili ni kuwa kuna makundi ndani ya CCM katika ngazi za juu: moja linamtaka Victor na lingine halimtaki. Hilo ambalo halimtaki ndio linaloitumia TAKUKURU.
3. Tafsiri ya tatu ni kuwa huko huko Peramiho kuna watu ambao wamekasirishwa na kitendo cha wakubwa 'kuwachagulia' mrithi. Kwa hiyo watu hao wameshirikiana na wakubwa ambao pia hawataki Victor awe mrithi wa Jenista hivyo wameamua kuitumia TAKUKURU!
Je, uliona tangu lini TAKUKURU ikajihangaisha na milungula ya makada wa CCM? TAKUKURU ni kama mbwa mlinzi ambaye hawezi kung'ata bila ya kutumwa na mwenye mbwa!
Pengine, atajiuliza? Askofu anahangaika nini na kura za maoni ndani ya CCM ambao hata hilo Bunge lao ni haramu? Jibu ni jepesi! Hata katika tenga la malankona (samaki) waliochina, unaweza kupata wazima. Kwa hiyo hao samaki au malankona wazima ndani ya tenga ni vizuri wakatunzwa vizuri wasije wakachina na wao!
Ninawaza kama Jenista akiwatazama CCM kutoka huko aliko atajisikiaje? Inawezekana akakumbuka 'ushauri' wa Askofu mwembamba aliwaowahi kumpatia kabla hajaenda katika ile ziara ya maafa ya mafuriko kule Kusini! Zikomo
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 22 Januari 2026; Saa 1:10 jioni