Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,016
- 6,759
"Kati ya mahabusu wa kiume 48 waliokuwepo katika Kituo cha Kirumba, kuna mtoto mwenye umri wa miaka 13. Mtoto huyu, alimsogelea Askofu na kumueleza kwa masikitiko kisa chake. Kwamba siku moja aliamua kuchuma limao moja katika mlimao wa jirani yake ili aweke kwenye dagaa ili ale. Jirani yake ambaye ni mwanamke pamoja na watoto wake walimshukia kwa kipigo kizito mtoto yule wakimshambulia kuwa ni mwizi.
Mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Johnson Frank, anasoma Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari ya Ibungilo iliyoko Ilemela. Askofu anakumbuka kuwa mtoto yule alisema kuwa shuleni anajulikana kwa jina la Ibrahim Frank na kwamba anakaa na bibi yake kwani mama yake yupo Dar es Salaam. Bibi yake, Mama yake na hata Uongozi wa Shule yake hawajui kama yupo mahabusu. Lakini kwa umri kama ule mtoto kuchanganywa mahabusu na watu wazima ni jambo lililomuumiza sana Askofu.
Askofu anajiuliza kama Mwanza hakuna Mahabusu ya Watoto? Askofu anatoa wito kwa makundi ya kutetea haki za watoto kufika haraka sana katika Kituo cha Polisi Kirumba, Mwanza ili kuangalia namna ya kumsaida mtoto yule. Lakini pia mtoto yule anatakiwa kufanyiwa vipimo kwani alikuwa analalamika maumivu katika mkono wake wa kulia kutokana na kipigo alichokuwa ameshushiwa na mwenye mti wa mlimao. Mazingira hayakuruhusu kwa Askofu kupata picha ya mtoto yule." - Askofu Emmaus Mwamakula