BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
ASKOFU MWAMAKULA KUFANYA MIKUTANO JIJINI DAR ES SALAAM KABLA YA KWENDA MIKOANI!
Ndugu Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa!
Ninapenda kuchukua nafasi hii kuwajulisha kuwa adhma yangu ya kuongoza "Matembezi ya Hiyari" kwa nchi nzima kwa lengo kuhamasisha umma kuhusu umuhimu na uhitaji wa Katiba Mpya iko palepale. Katika Mkoa wa Dar es Salaam ambao ndio tulipanga kuzindua Matembezi tarehe 16 Februari 2021, hatukufanya kwa kuwa mimi nilikamatwa na Jeshi la Polisi ambalo lilikuwa limejipanga kuvuruga Mpango wetu.
Kwa kuwa Jeshi la Polisi limenituhumu kuwa nilitaka kuchochea vurugu katika Mkoa wa Dar Es Salaam na kwa kuwa bado linaendelea na uchunguzi wake, kwa sababu hiyo, na ili kupisha uchunguzi wao, kutakuwa na mabadiliko kidogo katika ratiba na mpango wetu katika Mkoa wa Dar es Salaam kuhusu namna ya kufanya Matembezi hayo. Hivyo, badala ya kufanya "Matembezi ya Hiyari" katika Mkoa wa Dar es Salaam tutakuwa tukifanya Mikutano ya Hadhara ya Hiyari" na "Mikutano ya Ndani ya Kumbi ya Hiyari". Mabadiliko hayo yanahusu mkoa wa Dar es Salaam tu.
Utaratibu huo unatarajia kuanza wakati wowote. Kabla ya kuanza kufanya, Wanasheria wangu watawasiliana na mamlaka husika na kuwapa taarifa kwa njia ya maandishi. Ratiba ya kufanya mikutano ya Hadhara na mikutano ya ndani katika Jiji la Dar es Salaam itatolewa wakati wo wote baadaye.
Hata hivyo, Mpango wa kufanya Matembezi katika Jiji la Dar es Salaam bado upo palepale. Nitashauriana na Wanasheria wangu kuhusu namna ya kufanya Matembezi hayo katika mazingira ambayo yatauhakikishia umma na dunia kwa ujumla kuwa yatakuwa ni "Matembezi ya Amani".
Tukimaliza hatua ya mikutano katika Jiji la Dar es Salaam tutaelekea mikoani ambako tutafanya "Matembezi ya Hiyari" au tutafanya Mikutano ya Hadhara au Mikutano ya Ndani au tutafanya vyote kulingana na mazingira ya kila Mkoa au Wilaya!
Washindi siku zote hawakati tamaa na wanaokata tamaa hawawezi kushinda (Quiters never win and winners never quit)! Hatuwezi sote kukaa chini na kuendelea kunung'unika chini kwa chini kama wanafiki badala ya kuchukua hatua! Dunia haijawahi kubadirishwa na kuboreshwa na waoga, wenye hofu na wavivu! Jiandae kuniunga mkono katika kampeni nzito za kiutu na kimaadili kuwahi kutokea katika nchi yetu.
Tamanio langu ni kuona Tanzania inaingia katika Uchaguzi Mkuu wa 2025 ikiwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya! Tukiunganisha nguvu na tukiweka nia njema tutafanikiwa!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfutate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula