Askofu Mwamakula, Kila siku yumo kwenye siasa!
Kuna mahali una shida kabisa kichwani na hiyo shida itakutesa sana.
Ina maana mtu hawezi kufanya shughuli zake akajihusiha pia na siasa? Kwani nchi hii mtu kijihusisha na siasa ni dhambi?
Maneno haya ungemwabia basi Mchungaji Msigwa na Bwana Josephati Gwajima! Au wakati ule ungemuuliza Padre Augustin Ramadhani!
Ukiwa mpumbavu hakuna namna unaweza kuficha upumbavu wako ni aibu sana. Nilitegemea swali hili ungemuuliza Mchungaji Mtikila na Mama Lwakarare. Ila kwakua unajua kwamba ni mpumbavu huwezi kuhusianisha watu hao na mjadala wako. Mwamakula amekua sauti ya watu wengi kiasi hata hao unaojaribu kwalamba matako wanamtambua na wanamtambua mchango wake.
Mohammed alikua sio halifa au Mtume wa dini Bali hata kiongozi wa kisiasa aliyetawala.
Yesu Kristo alishtakiwa katika mahakama zote, za kidini na za kiraia Kwa sababu mahubiri yake yaligusa siasa (maisha) ya watu pamoja na dini! Ndio mana alipalekwa Kwa Gavana Pontius Pilate!
Mitume na manabii wote walitangulia walichukua wajibu wa Kimungu sio kuhubiri dini tu! Bali kukemea Wana siasa ambao walikua kinyume na mpango wa Mungu. Waliwakemea wanasiasa waliojitazama wao na kujiona Bora zaidi kuliko waliowaongoza. Yohanne Mbatizaji alikatwa kichwa kwa kumkemea Herodi (Mfalme) kwa kumuua ndugu yake na kumtwaa mke wake!
Serikali Yako imeanzisha kamati za amani zikiongozwa na hao viongozi wa dini. Sasa hawakujua kwamba Wana wajibu wa kuwajua waamini wao kuliko kuhusika na siasa?
Viongozi wa dini wanahubiri watu wao kuwa na amani upendo na mshikamano Kila siku! Mbweha kama wewe unaandika kushusu watu kuchukiana. Ni wajibu wa kiongozi wa dini kwenda Moja kwa Moja kwenye shina linalotaka waamini wachukiane sababu ya tofauti zao za kisiasa..
Hii ni kutokana na ukweli kwamba chuki hizo zinawwza kusababisha mauji ambayo ni dhambi Kwa mujibu wa amri za Mungu. Kanisa litafanyaje kazi wakati wote watu wanauana na kuwa wakimbizi?
Kanisa ni watu, na watu Hawa Ndio wanaotenda haya matendo ya wizi wa kura, ufisadi na Mauaji, watu wanaopora Haki za watu. Sasa Askofu au mchungaji ana wajibu wa kunakumbusha hawa watu kuwa matendo Yao ni kinyume na maelekezo ya mwenyezi Mungu!
Askari ni watu wanaolinda usalama wa watu na Mali zao! Wanapogeuka kuwa majambazi. Askofu ana wajibu wa kiroho wa kuwakemea mana imeandikwa kuiba ni dhambi na kudhulumu Haki ni dhambi! Hakuna namna unaweza kuchora mstari wankimajukumu linapokuja swala la siasa na Imani. Soma hapa
“Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msipokele rushwa kwa mtu awaye yote, wala msisingizie mtu bure; mkatosheka na mishahara yenu.”
(Luka 3:14).
Na mwisho Mshauri Mwenyekiti asiwaalike ikulu Wala juwapigia simu kuwapa michango ya makanisa Yao katikati ya ibada, lakini wakati wa uapisho wasiwaalike, na Wala wasiwatake kukuombea Taifa na wasivunje wanazoita kamati za amani za Mkoa na taifa!
Wewe ni Mjinga Ashakum sio matusi