BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,767
- 288,340
Mheshimiwa Jaffo, wakati ule Halmashauri nyingi zikiwemo zile zenye nguvu ya kiuchumi zilipokuwa zikishikiliwa na kuongozwa na UPINZANI, Serikali yenu iliamua kuzinyang'anya ukusanyaji wa mapato. Kwa sababu hali ile haikuwa ya kawaida, wengi tulijua kuwa mlifanya vile ili kuwakomoa viongozi wa upinzani na kuwachonganisha na wananchi ili waonekane wameshindwa kuratibu na kusimamia maendeleo kwa kuwa wasingeweza kufanya bila kuwa na udhibiti wa mapato.
Sasa CCM kimeshikilia Halmashauri zote mmeamua kurudisha ukusanyaji wa mapato kwa Halmashauri kwa kuwa mmeona mkiendelea kufanya hizo mtakuwa mnajichongea wenyewe kwa wananchi.
Utaratibu huu wa Serikali ya CCM kuendesha nchi kwa misingi ya ubaguzi ndio tunaoupinga. Kwa kuwa Bunge zima ni la CCM haliwezi kuwaonya na kuwakemea kwa ubaguzi huo mnaoufanya ninyi mnaoendesha Serikali. Sisi tuliobeba wajibu usio na mipaka kwa jamii ni wajibu wetu pia kuwaonya na kuwakemea hasa katika zamani hizi za utawala wenu ambapo mmejenga mazingira ya kuwafanya wengine na taasisi nyingine wasiweze kufanya hivyo.
Wazaramo wana msemo usemao: "Sema wewe kiazi, nikisema mie muhogo nina mzizi"! Kwa kuwa wewe unafahamu vizuri lugha na misemo ya Kizaramo, waambie na wafafanulie wenzako Serikalini kuwa Askofu Mwamakula hafurahishwi na ubaguzi huo unaofanywa na ninyi mnaoendesha nchi. Watu wengi sana katika nchi wanachukizwa na hayo mnayoyafanya lakini wanaotakiwa kusema hawawezi kwa sababu mbalimbali ambapo sababu mojawapo imefafanuliwa na msemo huo wa Kizaramo! Sasa, miye siyo 'muhogo' na wala sina 'mzizi', bali miye ni 'kiazi' na ndiyo maana nimesema na 'nimelonga'!
Kwa sababu hiyo, kama nilivyotangaza, nitaongoza "Matembezi ya Hiyari" katika nchi nzima ili kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na kuandika Katiba Mpya. Tunataka kwa pamoja tutengeneze mfumo utakaoondoa ubaguzi katika kuendesha nchi na kuweka mfumo wa haki wa kuwapata viongozi kuliko huu wa sasa ambao haufai na unaacha maumivu na manung'uniko mengi kwa watu.
Tunatoa wito kwa Watanzania wote katika Halmashauri zote wajitokeze kwa wingi na kuyaunga mkono "Matembezi ya Hiyari" ili kuonyesha hisia zao kuonyesha kuwa wanataka kuwa na mifumo ya haki ya namna ya kuongoza nchi. Hatuwezi kuendelea kuwa na mfumo unaoruhusu na kutoa mianya ya viongozi kuingia kwa hila na kuongoza au kutawala kwa hila na kuruhusu ubaguzi wa kificho!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula