Askofu Mwamakula: Sikutarajia yaliyoandikwa na Kabendera yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu

Nimechagua kusimama na the late. Dr. John Pombe Joseph Magufuli.



Kuongoza nchi, ni kazi kubwa sana, sijawahi kuongoza nchi wala kuwa kiongozi mawandamizi, lakini nafahamu kuongoza over 50+ cloud ni kazi inayohitaji, DAMU, JASHO NA MACHOZI.



Serikali kuu (hasa ofisi kuu ya taifa, ofisi namba moja ya taifa) ni taasisi, siyo mtu mmoja. Urais siyo mtu mmoja ni taasisi kubwa ambayo ina kila kitu.



Serikali ya nchi yoyote inaweza kuuwa, kushikilia watu kwa siri, hakuna sehemu katika katiba hivi vitu vimeandikwa. Niamini mimi kuwa hivi vitu vipo na vinafanyika kila nchi, hata ile nchi inayotumia mtawala wa kidini (pope) hivi vitu hufanyika.



Angalieni series ya Tylor inaitwa THE OVAL (Ameongelea white house ya Marekani), baadhi ya matukio ya mauaji yamefanyika in the name of the oval (white hoise ya marekani), wakati ambao hata mkuu wa oval(Rais) hafahamu.



Nenda ukaangalie series ya kikorea inafundisha kuhusu uongozi na namna ya kudeal watu wanaoweza kuangusha serikali inaitwa SHINE OR GO CRAZY.



Machepele, kwa sasa nipo

Nzela, Geita Tanzania.
 
Magufuli kwa vitendo vyake alikuwa anatekeleza kwa vitendo maagizo ya Mungu. Mwamakula kama ni mcha mungu wa kweli ingebidi azitambue kazi na sera za JPM kwa maskini wengi wa Tanzania kupigania haki zao za msingi.

Hapa chini Mungu anasema watu gani wanafanya kazi yake kwenye Mathayo 25.34-46. Linganisha kazi, sera za Magufuli, Kabendera na Mwamakula zipi zipo karibu na kuwapigia wanyonge wengi wa Tanzania?

Kisha Mfalme atawaambia wale walio upande wake wa kulia, ‘Njoni enyi mliobarikiwa na Baba yangu; pokeeni ufalme mliotayarishiwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu. 35Maana nilikuwa na njaa nanyi mkanipa chakula; nilikuwa na kiu nanyi mkanipa maji; nilikuwa mgeni nanyi mkanikaribisha;

36nilikuwa uchi, mkanivika; nilikuwa mgonjwa nanyi mkaja kunitazama; nilikuwa gerezani nanyi mkaja kunitembelea.’ 37Hapo, hao watu wema watamjibu mfalme ‘Bwana, ni lini tulikuona mwenye njaa nasi tukakupa chakula, au ukiwa na kiu nasi tukakunywesha maji? 38Ni lini tulikuona ukiwa mgeni nasi tukakukaribisha, au bila nguo nasi tukakuvika? 39Ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa au mfungwa nasi tukaja kukutazama?’

40Mfalme atawajibu, ‘Kweli nawaambieni, kila kitu mlichomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.’
41“Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokeni mbele yangu enyi mliolaaniwa! Nendeni katika moto wa milele aliotayarishiwa Ibilisi na malaika wake. 42Maana nilikuwa na njaa nanyi hamkunipa chakula; nilikuwa na kiu nanyi hamkunipa maji. 43Nilikuwa mgeni nanyi hamkunikaribisha; nilikuwa mgonjwa na mfungwa nanyi hamkuja kunitazama.’
44“Hapo nao watajibu, ‘Bwana, ni lini tulikuona ukiwa na njaa au kiu, ukiwa mgeni au bila nguo, ukiwa mgonjwa au mfungwa, nasi hatukukuhudumia?’

45Naye atawajibu, ‘Nawaambieni kweli, kila mlipokataa kumtendea mambo haya mmojawapo wa hawa wadogo, mlikataa kunitendea mimi.’ 46Basi, hawa watakwenda kwenye adhabu ya milele, lakini wale waadilifu watakwenda kwenye uhai wa milele.”
 
Hitler asamehewe maana hayupo nasi tena
Lakini msisahau sisiem ni genge kama magenge mengine.
 
Kwa maneno mengine, Askofu anatuthibitishia kwamba yaliyoandikwa katika kitabu cha Kabendera ni kweli kwani naye alipewa taarifa hizohizo ila hakuwahi kuzisema kokote.
Uthibitisho ni nini? Ushahidi usio na shaka.
Uthibitisho upo wapi hapo? Ushahidi wa kujitosheleza aliouweka upo wapi?

Kuunga mkono kauli, taarifa ya Kabendera sio uthibitisho, bila ushahidi ni maoni yake binafsi. Kwa watu makini hajatoa uthibitisho wowote wa kutosha kuhukumu.
 
Wewe ungeweza?
 
Daah aisee kumbe ni kweli
 
Tunaona matokeo ya approach nyingine sasa hivi awamu ya sita. Approach ya kumbebelezana badala ya kuwawajibisha watu.
Kweli ww ni mfoasi wa jiwe.Kwo kufukuzwa kazi mwenzako ww ndo furaha yako!!Vp kama huyo mtu ameonewa? Mara ngapi watu wanaonewa kwa makosa ya wengine?Enzi za jiwe sukuma gang ilikuwa inachukia sana watumishi
 
Achafuke mara ngapi!
 
Kwako,bt kwangu raisi wangu wa muda wote ni JK wa pili
 
Kweli ww ni mfoasi wa jiwe.Kwo kufukuzwa kazi mwenzako ww ndo furaha yako!!Vp kama huyo mtu ameonewa? Mara ngapi watu wanaonewa kwa makosa ya wengine?Enzi za jiwe sukuma gang ilikuwa inachukia sana watumishi
Ukishindwa majukumu yako wapishe wengine wenye uwezo kutimiza majukumu yao.

Enzi za Jiwe watumishi walikuwa kweli wanatumikia umma na kulikuwa na kesi chache za kuonewa makazini, au kufukuzwa kwa kuonewa, kuombwa rushwa.

Watu walipata huduma ambayo ni haki yako. Duniani kote, nchi zinazojitambua ndio utaratibu fanya kazi, uliyoiomba na kuapa kuifanya kwa nguvu, akili, uadilifu na uaminifu na weledi.
 
Asante mkuu sasa nakuamini kwamba kuwa halitasalia Jiwe juu ya Jiwe na sasa yanaanza kuja taratibu! Nani angejua kwamba Afande Mafwele angetajwa hadharani na serikali kuchukua nguvu kubwa kuzuia damage kuhusu yeye! Watajulikana hata tukio Zima la abduction and subsequently murder ya Kibao Ali Mchana kweupe! Asante Mwalimu Kwa Karma na Voice from Within
 
Kwani alichoandika ni ushahidi alikua anafanya submission mahakamani Ili wewe uliyejipa mamlaka ya kijaji useme huo sio ushahidi ni maoni? Kwako Nini kinayapima ni maoni meanwhile akisema aliwekwa jail wote tuliona Kabendera akiwa behind the bars na hakuna Kesi dhidi yake Hadi mama yake anapatwa na umauti! Kwamba Kuna sababu ya kusema Kifo Cha mama yake ni maoni au yeye kuwa jail ni maoni au Lisu kubutuliwa ni maoni?
 
Hakunaga Siri ya watu wawili na kuendelea Duniani.
Kila ubaya utawekwa wazi, ni swala la muda tu.
Damu ya binadamu ina Siri kubwa sana na aijuaye ni Muumbaji Mungu mwenyewe .

Imeandikwa; kila liliositirika kwa hila, dhuruma na ouvu litawekwa wazi na Muumbaji Yaani Mungu kwa njia azijuazo yeye.
Muda ni Mwamuzi mzuri sana.
 
Kila siku Lisu alikuwa anamtaja Magufuli kuwa ndio aliyeagiza yeye ashambuliwe kwa risasi, na alikuwa anayatamka haya akiwa hai tena hadharani. Uliwahi kukiri kuwa ni ukweli maana alisema Magufuli akiwa hai?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…