Hata Mimi nimemuelewa hivyoKwa maneno mengine, Askofu anatuthibitishia kwamba yaliyoandikwa katika kitabu cha Kabendera ni kweli kwani naye alipewa taarifa hizohizo ila hakuwahi kuzisema kokote.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata Mimi nimemuelewa hivyoKwa maneno mengine, Askofu anatuthibitishia kwamba yaliyoandikwa katika kitabu cha Kabendera ni kweli kwani naye alipewa taarifa hizohizo ila hakuwahi kuzisema kokote.
Mtu aue watu alafu watu wakae kimya viongozi wa dini kazi yake ni kukemea maovu na sio kuyakalia kimyaUkitoka maoni dhidi ya nchi badala ya kutoa maoni ya kujenga nchi Tena ukiwa kiongozi wa dini...lazima tujiulize maswali.
Uthibitisho ni nini? Ushahidi usio na shaka.Kwa maneno mengine, Askofu anatuthibitishia kwamba yaliyoandikwa katika kitabu cha Kabendera ni kweli kwani naye alipewa taarifa hizohizo ila hakuwahi kuzisema kokote.
Wewe ungeweza?Ukitaka kujua mtu muongo aliyekubuhu wana sifa moja za kufanana wawe maaskofu au yeyote utasikia marehemu aliniambia wakijua marehemu hawezi fufuka kujitetea au kusema muongo huyu Askofu
Askofu Mwamakula anaangukia kwenye hilo kundi la waongo wabobezi kwa nini hakusema hayo Magufuli akiwa hai?
Daah aisee kumbe ni kweliKABENDERA ANADAI BEN SANANE ALIUAWA NA 'BWANA MKUBWA'!
Mwishoni mwa mwaka 2020, nilipata ujumbe mzito kutoka kwa Rais Magufuli kupitia kwa mtu wake mmoja ambaye jina lake linatunzwa. Rais alimtuma kwangu akiniomba nishawishi Mhe. Freeman Mbowe na Mhe. Tundu Lissu waridhie wabunge wanawake 19 waapishwe kuwa Wabunge wa Viti Maalum.
Nilijitahidi kufurukuta kueleza Rais ajue kuwa sikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA wala mimi sikuwa na ushawishi wowote katika jambo lile. Lakini Rais aliamini kuwa Lissu na Mbowe watanisikiliza mimi. Lilikuwa jambo gumu sana kwangu kumshawishi mtu yule aniamini mimi. Ahadi niliyoahidiwa na ambayo pia CHADEMA wangepewa kama 'dili' lile lingefanyika ingali katika kilindi cha moyo.
Nakiri kuwa baada ya ombi la Rais la kunitaka niwashawishi Lissu na Mbowe kushindikana, zoezi la uapishwaji liliendelea na mimi nikajua kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari. Lakini hoja la andiko hili sio jambo hili.
Mwezi Januari 2021, alitumwa tena kwangu mtu yule yule. Safari hii haikuwa kunishawishi ili niwashawishi Mbowe na Lissu, bali ilikuwa ni kunitisha niachane na harakati, la sivyo basi nilikuwa nachungulia mauti. Nilikuwa nimetoka kuitangazia dunia kuwa maisha ya Mhe. Lissu yalikuwa hatarini na ndipo Ubalozi mmojawapo ukamchukua na kumpeleka nje ya nchi.
Kwa hiyo jibu langu kwake lilikuwa moja tu: "Mwambie Mheshimiwa kuwa akitaka aniue, lakini Askofu hatarudi nyuma"! Vitisho vya aina hiyo niliwahi kupewa na Polisi mmoja nikiwa Central Polisi, Dar es Salaam mwezi mmoja kabla Rais Magufuli hajafariki dunia.
Baada ya majibu yale, yule mtu alitetemeka na ikabidi aropoke mambo mengi sana ambayo sio sehemu ya andiko hili kwani kwa sasa Bado mambo yale ni 'classified information'! Baada ya hapo nikaanza kupata taarifa nyingi ambazo zilinitisha na kunipatia matumaini.
Siku moja nilitafutwa na mtu mmoja ambaye ni mzima na kada wa CCM. Kwa kuwa mtu huyo tunaheshimiana na kwa kuwa aliaminishwa ya kuwa mimi nilikuwa natumiwa na 'mabeberu'; ilibidi nimueleze pia baadhi ya mambo ambayo yalikuwa yanamzunguka Rais. Nilifanya hivyo ikiwa kinga yangu kwani nilijua kuwa ataelewa mazingira yangu na hivyo ataweza kupangua hoja dhaifu dhidi yangu akiwa katika 'Pango la Wakilindi'. Aliishia kunikodolea macho na ndipo tukaagana akiwa kama mtu asiyeamini.
Lakini kabla mtu huyo hajaondoka, aliniuliza: "Wewe umejuaje habari hizi'? Nikamjibu kuwa: "Mimi ni mskofu wa mnyororo na pia mimi ni askofu wa kiapo"! Mambo haya yaliaminiwa pia kwangu chini ya kiapo kwa hiyo nisingeyasema hadharani wakati ule na hata sasa. Hapa sio mahali pake kuelezea kisa cha askari aliyeacha kufanya ibada baada ya kushiriki kuwaua watu na baadaye kumbukumbu za watu wale zikawa zinamjia na kuharibu akili yake.
Mambo haya ni ya kitubio na kwa hiyo mtu ye yote atakayemuendea Mchungaji (Padri) au Askofu kwa kitubio, jambo lile linabakia katika kifua cha mtubishaji, anayetubu na Mungu.
Taarifa za kuchapishwa kwa kitabu cha Erick Kabendera zimeanza kusambaa kwa kasi sana mitandaoni siku ya leo tarehe 3 Januari 2025. Kitabu kinaitwa: 'In the Name of the President: Memoirs of a Jailed Journalist'. Nimesikiliza mahojiano ya Erick Kabendera kuhusu kitabu hicho. Nimeanza kufuatilia maudhui ya kitabu. Mengi ya mambo anayojadili ni sehemu ya yale niliyojulishwa kama 'sisi Askofu'! Ila sikutarajia mambo yale yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu. Ujasiri wa Kabendera unaivuka mipaka ya Nshamba na Kamachumu.
Ninaamini watu ambao walinishangaa kwa nini mimi nilijitoa muhanga kwa ajili ya kutetea haki nchini sasa wataanza kuelewa baada ya kuona na kusoma kitabu cha Erick Kabendera. Taarifa nyingi zilizofikishwa katika kilindi cha moyo wangu ziliishurutisha nafasi yangu kuchukua ili kupaza sauti na kutetea pale nilipoweza. Lakini pamoja na uropokaji wangu, mambo ambayo yalitiwa muhuri (sealed) katika moyo wangu yameamriwa na dhamiri iliyo kuu ili yasiyoke.
Kitabu cha Kabendera kitasaidia katika mambo muhimu. Kwamba tukisome na kumjua Rais Magufuli nje ya uelewa uliojulikana. Baada ya hapo, tuone kuwa alikuwa binadamu kama sisi na mwenye mapungufu na kisha tumsamehe. Kikubwa, kama jamii tutafute njia ya kuponya ikiwemo kuondoa vimelea au masalia ya yale aliyoayaasisi ambayo hayakuwa mazuri na hili itawezekana kama tutasoma na kuielewa sura ya mwisho ya Kitabu cha Kabendera.
Kitabu hiki kinaposambazwa na kusomwa ni vizuri tujue kuwa kinayahusu maisha fichika ya Rais Magufuli na sio maisha ya familia na ukoo wake. Hatuhitaji kwa namna yeyote kuwaona ndugu hata familia kama sehemu ya mambo aliyoyafanya kama Rais kwani nao walikuwa ni washangaaji kama sisi.
Mwisho, natoa wito kwa viongozi wa dini walio karibu na familia ya Ben Sanane na familia ya Azorly Gwanda kuzifikia kwa ajili ya huduma ya kiroho. Kupitia kitabu cha Erick Kabendera na mahojiano yake ni rasmi sasa ya kuwa umma umejulishwa kuwa watu hao hawapo pamoja nasi katika maisha haya.
Hekima iliyo ndani ya kilindi cha moyo wa Rais Samia inaweza kumsaidia afanye nini kwa ajili ya familia hizo. Bila shaka, CHADEMA itatafuta namna njema ya kuhitimisha kwa heshima kwa kumkumbuka Ben, mwanachama na Msaidizi maalum wa Mhe. Mbowe. Kadhalika, Gazeti la Mwananchi litaona pia namna ya kulihitimisha l kwa heshima ya Azorly, aliyekuwa mtumishi.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 3 Januari 2025; saa 2:00 usiku
Kweli ww ni mfoasi wa jiwe.Kwo kufukuzwa kazi mwenzako ww ndo furaha yako!!Vp kama huyo mtu ameonewa? Mara ngapi watu wanaonewa kwa makosa ya wengine?Enzi za jiwe sukuma gang ilikuwa inachukia sana watumishiTunaona matokeo ya approach nyingine sasa hivi awamu ya sita. Approach ya kumbebelezana badala ya kuwawajibisha watu.
Achafuke mara ngapi!Hivi unajuaje kama mtu katumwa na Rais kuja kwako? Yaani ni kigezo kipi kinakuonesha ni kweli huyu mtu kaagizwa na Rais au wanakujaga na barua?. Maana nijuavyo mimi afisa yeyote kwa utashi wake anaweza akawa hapendi wewe unachokifanya cha kuchafua image ya serikali au ya nchi hivyo ili akunyamazishe itabidi aje akutishe kidogo. All in all JPM hawezi chafuka kwa hadithi za kutunga sababu kazi zake na wema wake kwa taifa bado vinaishi na kila unaposafiri nchii hii kazi zake nzuri zinaonekana na zinamtetea.
Kwako,bt kwangu raisi wangu wa muda wote ni JK wa piliMimi sio sisiemu, sio cdm lkn katika marais waliowahi kuiongoza nchi yangu ya Tanzania wakwanza Ni nyerere wa pili Ni jpm.
Wapo marais wamepita lkn bado hawajawakaribia hata robo kwa uongozi na ushawishi, angalia hata misiba yao ilivyo na mguso kwa raia.
Najua pamoja na Mambo yote yanayoongelewa lkn hatujafahamu Nini walifanya wahanga kiasi Cha kupelekea kifo Chao. Tunachojua zaidi Ni tukio lakupotea. Na hata Kama wasingepotea sidhani Kama wangeweza fikia hata robo la aliyoyafanya rais. Kuna maumivu kwa familia na raia lkn haitoweza kubadilika. Kingine hayo Ni maneno watu waweke ushahidi hapa itakuwa rahisi kuamini.
Ukishindwa majukumu yako wapishe wengine wenye uwezo kutimiza majukumu yao.Kweli ww ni mfoasi wa jiwe.Kwo kufukuzwa kazi mwenzako ww ndo furaha yako!!Vp kama huyo mtu ameonewa? Mara ngapi watu wanaonewa kwa makosa ya wengine?Enzi za jiwe sukuma gang ilikuwa inachukia sana watumishi
Asante mkuu sasa nakuamini kwamba kuwa halitasalia Jiwe juu ya Jiwe na sasa yanaanza kuja taratibu! Nani angejua kwamba Afande Mafwele angetajwa hadharani na serikali kuchukua nguvu kubwa kuzuia damage kuhusu yeye! Watajulikana hata tukio Zima la abduction and subsequently murder ya Kibao Ali Mchana kweupe! Asante Mwalimu Kwa Karma na Voice from Withinkaribu Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana
hili la mimi kumchomea EK ni kweli nilihisiwa,alipofiwa na mama, kwanza nilimuombea kwa JPM Personal Plea Kwa Rais Magufuli: Kama ameweza kuwasamehe wabakaji, wauaji, mafisadi, wahujumu, anaweza pia kumsamehe Eric Kabendera, amzike mama yake
Mimi ni miongoni mwa waandishi tuliomzika mama yake EK, kisha nikajibu tuhuma Pascal Mayalla ndiye aliyemchongea Erick Kabendera kwa dola
Nikiwa UK, nikamtafuta,akanijulisha jinsi alivyokuwa akipelekewa print out za jf jinsi ninavyomchomea!。 Thanks God he is an intelligent man,angekuwa mjinga mjinga angeamini huo ujinga!
P
ongea kiswahili unadhani wote humu ni waingereza?Wao wameyaweka humu kwaajili ya nini?of what use here?
Anza kubadili Jina au ID iwe ya kiswahili na uanze kumuonesha njia huyo mchangiajiongea kiswahili unadhani wote humu ni waingereza?Wao wameyaweka humu kwaajili ya nini?
Kwani alichoandika ni ushahidi alikua anafanya submission mahakamani Ili wewe uliyejipa mamlaka ya kijaji useme huo sio ushahidi ni maoni? Kwako Nini kinayapima ni maoni meanwhile akisema aliwekwa jail wote tuliona Kabendera akiwa behind the bars na hakuna Kesi dhidi yake Hadi mama yake anapatwa na umauti! Kwamba Kuna sababu ya kusema Kifo Cha mama yake ni maoni au yeye kuwa jail ni maoni au Lisu kubutuliwa ni maoni?Uthibitisho ni nini? Ushahidi usio na shaka.
Uthibitisho upo wapi hapo? Ushahidi wa kujitosheleza aliouweka upo wapi?
Kuunga mkono kauli, taarifa ya Kabendera sio uthibitisho, bila ushahidi ni maoni yake binafsi. Kwa watu makini hajatoa uthibitisho wowote wa kutosha kuhukumu.
ID isimpeshida afatilie maoni yangu kama natumia Kiswanglish kama chake.Anza kubadili Jina au ID iwe ya kiswahili na uanze kumuonesha njia huyo mchangiaji
Kila siku Lisu alikuwa anamtaja Magufuli kuwa ndio aliyeagiza yeye ashambuliwe kwa risasi, na alikuwa anayatamka haya akiwa hai tena hadharani. Uliwahi kukiri kuwa ni ukweli maana alisema Magufuli akiwa hai?Ukitaka kujua mtu muongo aliyekubuhu wana sifa moja za kufanana wawe maaskofu au yeyote utasikia marehemu aliniambia wakijua marehemu hawezi fufuka kujitetea au kusema muongo huyu Askofu
Askofu Mwamakula anaangukia kwenye hilo kundi la waongo wabobezi kwa nini hakusema hayo Magufuli akiwa hai?