Askofu Mwamakula: Sikutarajia yaliyoandikwa na Kabendera yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu

Askofu Mwamakula: Sikutarajia yaliyoandikwa na Kabendera yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu

KABENDERA ANADAI BEN SANANE ALIUAWA NA 'BWANA MKUBWA'!

Mwishoni mwa mwaka 2020, nilipata ujumbe mzito kutoka kwa Rais Magufuli kupitia kwa mtu wake mmoja ambaye jina lake linatunzwa. Rais alimtuma kwangu akiniomba nishawishi Mhe. Freeman Mbowe na Mhe. Tundu Lissu waridhie wabunge wanawake 19 waapishwe kuwa Wabunge wa Viti Maalum.

Nilijitahidi kufurukuta kueleza Rais ajue kuwa sikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA wala mimi sikuwa na ushawishi wowote katika jambo lile. Lakini Rais aliamini kuwa Lissu na Mbowe watanisikiliza mimi. Lilikuwa jambo gumu sana kwangu kumshawishi mtu yule aniamini mimi. Ahadi niliyoahidiwa na ambayo pia CHADEMA wangepewa kama 'dili' lile lingefanyika ingali katika kilindi cha moyo.

Nakiri kuwa baada ya ombi la Rais la kunitaka niwashawishi Lissu na Mbowe kushindikana, zoezi la uapishwaji liliendelea na mimi nikajua kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari. Lakini hoja la andiko hili sio jambo hili.

Mwezi Januari 2021, alitumwa tena kwangu mtu yule yule. Safari hii haikuwa kunishawishi ili niwashawishi Mbowe na Lissu, bali ilikuwa ni kunitisha niachane na harakati, la sivyo basi nilikuwa nachungulia mauti. Nilikuwa nimetoka kuitangazia dunia kuwa maisha ya Mhe. Lissu yalikuwa hatarini na ndipo Ubalozi mmojawapo ukamchukua na kumpeleka nje ya nchi.

Kwa hiyo jibu langu kwake lilikuwa moja tu: "Mwambie Mheshimiwa kuwa akitaka aniue, lakini Askofu hatarudi nyuma"! Vitisho vya aina hiyo niliwahi kupewa na Polisi mmoja nikiwa Central Polisi, Dar es Salaam mwezi mmoja kabla Rais Magufuli hajafariki dunia.

Baada ya majibu yale, yule mtu alitetemeka na ikabidi aropoke mambo mengi sana ambayo sio sehemu ya andiko hili kwani kwa sasa Bado mambo yale ni 'classified information'! Baada ya hapo nikaanza kupata taarifa nyingi ambazo zilinitisha na kunipatia matumaini.

Siku moja nilitafutwa na mtu mmoja ambaye ni mzima na kada wa CCM. Kwa kuwa mtu huyo tunaheshimiana na kwa kuwa aliaminishwa ya kuwa mimi nilikuwa natumiwa na 'mabeberu'; ilibidi nimueleze pia baadhi ya mambo ambayo yalikuwa yanamzunguka Rais. Nilifanya hivyo ikiwa kinga yangu kwani nilijua kuwa ataelewa mazingira yangu na hivyo ataweza kupangua hoja dhaifu dhidi yangu akiwa katika 'Pango la Wakilindi'. Aliishia kunikodolea macho na ndipo tukaagana akiwa kama mtu asiyeamini.

Lakini kabla mtu huyo hajaondoka, aliniuliza: "Wewe umejuaje habari hizi'? Nikamjibu kuwa: "Mimi ni mskofu wa mnyororo na pia mimi ni askofu wa kiapo"! Mambo haya yaliaminiwa pia kwangu chini ya kiapo kwa hiyo nisingeyasema hadharani wakati ule na hata sasa. Hapa sio mahali pake kuelezea kisa cha askari aliyeacha kufanya ibada baada ya kushiriki kuwaua watu na baadaye kumbukumbu za watu wale zikawa zinamjia na kuharibu akili yake.

Mambo haya ni ya kitubio na kwa hiyo mtu ye yote atakayemuendea Mchungaji (Padri) au Askofu kwa kitubio, jambo lile linabakia katika kifua cha mtubishaji, anayetubu na Mungu.

Taarifa za kuchapishwa kwa kitabu cha Erick Kabendera zimeanza kusambaa kwa kasi sana mitandaoni siku ya leo tarehe 3 Januari 2025. Kitabu kinaitwa: 'In the Name of the President: Memoirs of a Jailed Journalist'. Nimesikiliza mahojiano ya Erick Kabendera kuhusu kitabu hicho. Nimeanza kufuatilia maudhui ya kitabu. Mengi ya mambo anayojadili ni sehemu ya yale niliyojulishwa kama 'sisi Askofu'! Ila sikutarajia mambo yale yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu. Ujasiri wa Kabendera unaivuka mipaka ya Nshamba na Kamachumu.

Ninaamini watu ambao walinishangaa kwa nini mimi nilijitoa muhanga kwa ajili ya kutetea haki nchini sasa wataanza kuelewa baada ya kuona na kusoma kitabu cha Erick Kabendera. Taarifa nyingi zilizofikishwa katika kilindi cha moyo wangu ziliishurutisha nafasi yangu kuchukua ili kupaza sauti na kutetea pale nilipoweza. Lakini pamoja na uropokaji wangu, mambo ambayo yalitiwa muhuri (sealed) katika moyo wangu yameamriwa na dhamiri iliyo kuu ili yasiyoke.

Kitabu cha Kabendera kitasaidia katika mambo muhimu. Kwamba tukisome na kumjua Rais Magufuli nje ya uelewa uliojulikana. Baada ya hapo, tuone kuwa alikuwa binadamu kama sisi na mwenye mapungufu na kisha tumsamehe. Kikubwa, kama jamii tutafute njia ya kuponya ikiwemo kuondoa vimelea au masalia ya yale aliyoayaasisi ambayo hayakuwa mazuri na hili itawezekana kama tutasoma na kuielewa sura ya mwisho ya Kitabu cha Kabendera.

Kitabu hiki kinaposambazwa na kusomwa ni vizuri tujue kuwa kinayahusu maisha fichika ya Rais Magufuli na sio maisha ya familia na ukoo wake. Hatuhitaji kwa namna yeyote kuwaona ndugu hata familia kama sehemu ya mambo aliyoyafanya kama Rais kwani nao walikuwa ni washangaaji kama sisi.

Mwisho, natoa wito kwa viongozi wa dini walio karibu na familia ya Ben Sanane na familia ya Azorly Gwanda kuzifikia kwa ajili ya huduma ya kiroho. Kupitia kitabu cha Erick Kabendera na mahojiano yake ni rasmi sasa ya kuwa umma umejulishwa kuwa watu hao hawapo pamoja nasi katika maisha haya.

Hekima iliyo ndani ya kilindi cha moyo wa Rais Samia inaweza kumsaidia afanye nini kwa ajili ya familia hizo. Bila shaka, CHADEMA itatafuta namna njema ya kuhitimisha kwa heshima kwa kumkumbuka Ben, mwanachama na Msaidizi maalum wa Mhe. Mbowe. Kadhalika, Gazeti la Mwananchi litaona pia namna ya kulihitimisha l kwa heshima ya Azorly, aliyekuwa mtumishi.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 3 Januari 2025; saa 2:00 usiku
Hapo ndio ajue Samia ni mtu sio kama kibaraka Mkuu anaemtetea anavyoropoka huko.
 
Tatizo lao hawasemi hata mazuri yaliyofanywa, wanapiga kampeni kuhusu upande mmoja tu kwa ajili ya 2025.

Hawaoni elimu bure, maji, umeme, usiokatika wa being nafuu. Vituo vya afya, hospitali, barabara, masoko mapya, SGR, bwana ya umeme, uwajibikaji, wote kupata huduma kwa wakati bila rushwa, kuthibiti inflation, ufisadi, wizi wa maliasili.

Hawaoni mikakati iliyowekwa kulikomboa hili taifa. Lazima uwe ba tatizo la afya ya akili usipoyaona haya na kujomalia issue moja tu.
Hayo mazuri ulikuwa ni wajibu wake kuyatekeleza maana alikuwa analipwa kwa kodi zetu na wala hakuwa akitoa hela yake mfukoni kuyatekeleza zilikuwa ni kodi zetu pia.
Halafu wema huwa hauvumi sana kama ubaya.
Na kabendara si wa kwanza kuandika ubaya wa kiongozi ndo maana biblia imeandika wazi kuwa mfalme daudi alimchukua mke wa mwanajeshi wake na akamzalisha na akatengeneza mazingira ya mume wa mwanamke huyo kuuwawa
Hivyo hamna cha ajabu alichofanya kabendera
 
Jifunzeni kuthamini kazi za watu nyie wamatumbi. Mtu kachukua muda wake kuandika wewe unataka bure na kusambaza bure, ingekua ni kazi yako ungejisikiaja? Aendeshe vp familia yake?
Ndio maisha yetu sisi wamatumbi kwani vipi?
Kutumia muda wangu Kusoma hicho Kitabu ni heshima kubwa nitakuwa nimempa.
Alikwambia amekichapisha ili aendeshe familia au we ndio mkewe?
 
Nasikia kuna hadi video clips.Ni maombi yangu kwamba hizo clips zisiletwe humu.wala tusiendelee na ubishi utakaosababisha hizo clips ziletwe humu.Wacha jambo hili liishie haoa tuangalie yajayo.hata kama ni kweli au ai kweli jambo jema ni kulimaliza hili jambo ambalo ni gunu kwa kweli.

Unajua mtu hawezi kuleta tuhuma zenye ukakasi mkubwa namna hii bila kuwa na hard back up.

Nafahamu,Kabendera ni kati ya well trained Investigative Journalist hapa nchini,by the way ni wachache wandishi wenye kaliba yake.Pia tusishau kwenye network yake wapo pia watu wa mifumo ambao pengine hawakupenda uonevu.

Nilimlifuatilia kwa karibu wakati akiwa na ile kesi ya kuhujumu uchumi nikagundua ni mtu jasiri ambaye pia ni consistent.

Jamaa hawexi kutunga story kama hizo.

Tatizo la Watanzania ni wabishi bila sababu. Hangover ya Ujamaa inawasumbua. Wamezoea kuishi kwa propaganda. Kuna watu hata hawaamini kuwa Lissu alikuwa auwawe kwa maelekezo toka juu. Makonda roho inamruka huko aliko. Soon kila kitu kitakuwa wazi. Nasubiri kesi ya Lissu ipande mahakani huko UK.
 
Jamaa hawexi kutunga story kama hizo.

Tatizo la Watanzania ni wabishi bila sababu. Hangover ya Ujamaa inawasumbua. Wamezoea kuishi kwa propaganda. Kuna watu hata hawaamini kuwa Lissu alikuwa auwawe kwa maelekezo toka juu. Makonda roho inamruka huko aliko. Soon kila kitu kitakuwa wazi. Nasubiri kesi ya Lissu ipande mahakani huko UK.
Sijui anajiskiaje akisikia hizi habari za bosi wake zinalipuka hivi wazi wazi.
 
Hayo mazuri ulikuwa ni wajibu wake kuyatekeleza maana alikuwa analipwa kwa kodi zetu na wala hakuwa akitoa hela yake mfukoni kuyatekeleza zilikuwa ni kodi zetu pia.
Halafu wema huwa hauvumi sana kama ubaya.
Na kabendara si wa kwanza kuandika ubaya wa kiongozi ndo maana biblia imeandika wazi kuwa mfalme daudi alimchukua mke wa mwanajeshi wake na akamzalisha na akatengeneza mazingira ya mume wa mwanamke huyo kuuwawa
Hivyo hamna cha ajabu alichofanya kabendera
Hakika
 
Hayo mazuri ulikuwa ni wajibu wake kuyatekeleza maana alikuwa analipwa kwa kodi zetu na wala hakuwa akitoa hela yake mfukoni kuyatekeleza zilikuwa ni kodi zetu pia.
Halafu wema huwa hauvumi sana kama ubaya.
Na kabendara si wa kwanza kuandika ubaya wa kiongozi ndo maana biblia imeandika wazi kuwa mfalme daudi alimchukua mke wa mwanajeshi wake na akamzalisha na akatengeneza mazingira ya mume wa mwanamke huyo kuuwawa
Hivyo hamna cha ajabu alichofanya kabendera
Kwahiyo kila mtu anaweza kuita mwingine mbakaji, mlawiti, muuaji akaandika kitabu bila ushahidi wowote mtu huyo akiwa kafariki.

Tuhuma nzito kama hizo inabidi ziwe na ushahidi usio na shaka, sio nimeambiwa hivi, vile, hearsay, huwasemi hata walikuambia.

Vipi wewe ukipewa hizo tuhuma bila ushahidi wowote unaona ni sawa?
 
Nafahamu,Kabendera ni kati ya well trained Investigative Journalist hapa nchini,by the way ni wachache wandishi wenye kaliba yake.Pia tusishau kwenye network yake wapo pia watu wa mifumo ambao pengine hawakupenda uonevu.
Bila shaka
 
N
Mtanikumbuka kama alivosema... Kabendera na Mwamakula wameshaeleza naamin hao ndo wamwisho lakin kama kunamwingine atakujakutoa shuhuda yake ajetumsikilize..ilamuacheni mzee wa watu apumzike mlimsema akiwahai mpaka marehemu !! kwahyo mnatujengea taswila gani sisi wananchi tulikuwa wanyonge lakini pia kwa nchi yetu na viongozi wetu tunaowaamini na kuwachagua? mnapaswa kuziheshimu na kuzitii mamlaka zinazowaangoza kamamlikengeuka kwanini siziwaadhibu? nawashauri tu mnapoandika mavitabu yenu uchwara niombe nanyi maovu yenu myaweke wazi sio kuzungumzia mabaya ya mwenzenu kwani mimi huwa naamini hakuna binadamu mkamilifu...lakini pia mavitabu yenu uchwara yaweyaeleza na mazuri aliotuachia katika nchi yetu pendwa..kwawale niliokwaza mnisamehe.
Ndiyo, watu wanakengeuka nchini then wanataka huruma kwa wananchi. Pumbavu kabisa hao mbwa. Kuna watu ukikutana nao mtaani unaweza kusema Ni watu lkn anga zao Ni hatari kuliko simba. Sasa Kama Ni kiongozi kwa Nini wasipunguzwe nchi ipumue?
 
hakuna kuisha bila haki kutendeka
Hayaishi bila mwafaka....huko.ndani wataendelea kuwindana kama paka na panya. Nchi zote duniani yalitulia baada ya kuchapana na baadae wakwekeana mwafaka kupitia mifumo yao ya utawala. Hapo ndio wakaanza kupata maendeleo ya kiuchumi, utawala bora na demokrasia ya kueleweka hata kama sio 100%
 
Una ushahidi JPM alimpiga risasi Saanane, Lissu au alimtesa Kabendera?
Yes, kadendera asingelithubutu kuyaandika kwenye kitabu chake....wanasheria wa dunia wali Ok akichapishe maana walihakikisha kuna ushahidi usio na mashaka
 
JPM alitufunulia na kutuonyesha namna mambo mengi mazuri yanaweza kufanyika katika nchi hii na nchi ikaenda mbele kwa haraka.

Taifa hili hela nyingi inapotea mikononi mwa watu wasiowaaminifu kuanzia watumishi, wafanyabiashara na makampuni ya nje yaliyojikita kwenye fraud kwa kushirikiana na watumishi na viongozi.

Kupitia JPM watu wengi walijua shida ya nchi hii ni ombwe la uongozi na kukiwa na kiongozi shupavu basi mambo yanaweza kwenda kwa kasi.

Mapenzi ya wananchi mitaani dhidi ya JPM ni makubwa sana na ukweli uliowazi, WANANCHI WANAHITAJI JPM mwingine.

Binafsi kwangu JPM alikuwa na huruma sana, alipaswa kuua wapumbavu na wajinga weeengi sana katika nchi hii ambao wanaua watu kila siku kupitia upumbavu wao.
100 % Truth !
Ndio maana HACHAFUKI na HACHAFUKIKI !
Acha waendelee kubwabwaja !
 
Back
Top Bottom