Askofu Mwamakula: Sikutarajia yaliyoandikwa na Kabendera yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu

Askofu Mwamakula: Sikutarajia yaliyoandikwa na Kabendera yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu

Hakika !
Mtanikumbuka kama alivosema... Kabendera na Mwamakula wameshaeleza naamin hao ndo wamwisho lakin kama kunamwingine atakujakutoa shuhuda yake ajetumsikilize..ilamuacheni mzee wa watu apumzike mlimsema akiwahai mpaka marehemu !! kwahyo mnatujengea taswila gani sisi wananchi tulikuwa wanyonge lakini pia kwa nchi yetu na viongozi wetu tunaowaamini na kuwachagua? mnapaswa kuziheshimu na kuzitii mamlaka zinazowaangoza kamamlikengeuka kwanini siziwaadhibu? nawashauri tu mnapoandika mavitabu yenu uchwara niombe nanyi maovu yenu myaweke wazi sio kuzungumzia mabaya ya mwenzenu kwani mimi huwa naamini hakuna binadamu mkamilifu...lakini pia mavitabu yenu uchwara yaweyaeleza na mazuri aliotuachia katika nchi yetu pendwa..kwawale niliokwaza mnisamehe.
 
Haha mkuu mbona unauliza kitu ambacho unajua kabisa abadan kisingewezekana? It was still a classified information ndiomana hata yeye anashangaa imekuwaje mambo haya yamewekwa wazi akiwa bado hai meaning hata yeye alitegemea kubakia kuwa "CONFIDENTIAL"
Waongo na wanafiki wana sifa za kufanana jinsi wao walivyokuwa lopolopo mbona ingekuwa wazi mapema?
 
Hata huo ubunge alioshinda mara ya kwanza ni baada ya kufanya fouls kibao
Kimaadili jamaa alikuwa mchafu haiwezekani kusema alikuwa na angalau kijiusafi fulani
Yule alikuwa na kaushetani yule.
 
Ukitoka maoni dhidi ya nchi badala ya kutoa maoni ya kujenga nchi Tena ukiwa kiongozi wa dini...lazima tujiulize maswali.
Huwezi kumsikia huyo Mwamakula akijaribu kuunganisha wananchi majukwaani.

Akipongeza kujengwa kwa hospitali hivyo kuokoa maisha. Umeme, maji, kudhibiti mfumuko wa bei, kupunguza rushwa, ufisadi, haki ya wazee, yatima, wajane kutodhulumiwa ardhi yao, nyumba, mashamba yao.

Haoni kwamba haki ilitendeka kwa sera hizi. Kwamba mikakati hii iliwasaidia watoto wengi maskini, watoto wa Mungu.

Asijiche kwamba aliambiwa na watu wa ndani. Anatoa tuhuma zisizo na ushahidi. Biblia imeandika usimsingizie jirani yako uongo. Mwambieni awe jasiri aweke ushahidi wazi. Mungu atamlinda.
 
Ukitaka kujua mtu muongo aliyekubuhu wana sifa moja za kufanana wawe maaskofu au yeyote utasikia marehemu aliniambia wakijua marehemu hawezi fufuka kujitetea au kusema muongo huyu Askofu

Askofu Mwamakula anaangukia kwenye hilo kundi la waongo wabobezi kwa nini hakusema hayo Magufuli akiwa hai?
Ungekua wewe ungefunua nyumba Yako ya meno uzungumze hayo ilinushindane na nani?
Na hapo wapi amesema Magufuli alimwambia au alisema!
Kuna mambo ni Magumu kutetea, huyu Mtu alikua ni binadamu!
 
KABENDERA ANADAI BEN SANANE ALIUAWA NA 'BWANA MKUBWA'!

Mwishoni mwa mwaka 2020, nilipata ujumbe mzito kutoka kwa Rais Magufuli kupitia kwa mtu wake mmoja ambaye jina lake linatunzwa. Rais alimtuma kwangu akiniomba nishawishi Mhe. Freeman Mbowe na Mhe. Tundu Lissu waridhie wabunge wanawake 19 waapishwe kuwa Wabunge wa Viti Maalum.

Nilijitahidi kufurukuta kueleza Rais ajue kuwa sikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA wala mimi sikuwa na ushawishi wowote katika jambo lile. Lakini Rais aliamini kuwa Lissu na Mbowe watanisikiliza mimi. Lilikuwa jambo gumu sana kwangu kumshawishi mtu yule aniamini mimi. Ahadi niliyoahidiwa na ambayo pia CHADEMA wangepewa kama 'dili' lile lingefanyika ingali katika kilindi cha moyo.

Nakiri kuwa baada ya ombi la Rais la kunitaka niwashawishi Lissu na Mbowe kushindikana, zoezi la uapishwaji liliendelea na mimi nikajua kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari. Lakini hoja la andiko hili sio jambo hili.

Mwezi Januari 2021, alitumwa tena kwangu mtu yule yule. Safari hii haikuwa kunishawishi ili niwashawishi Mbowe na Lissu, bali ilikuwa ni kunitisha niachane na harakati, la sivyo basi nilikuwa nachungulia mauti. Nilikuwa nimetoka kuitangazia dunia kuwa maisha ya Mhe. Lissu yalikuwa hatarini na ndipo Ubalozi mmojawapo ukamchukua na kumpeleka nje ya nchi.

Kwa hiyo jibu langu kwake lilikuwa moja tu: "Mwambie Mheshimiwa kuwa akitaka aniue, lakini Askofu hatarudi nyuma"! Vitisho vya aina hiyo niliwahi kupewa na Polisi mmoja nikiwa Central Polisi, Dar es Salaam mwezi mmoja kabla Rais Magufuli hajafariki dunia.

Baada ya majibu yale, yule mtu alitetemeka na ikabidi aropoke mambo mengi sana ambayo sio sehemu ya andiko hili kwani kwa sasa Bado mambo yale ni 'classified information'! Baada ya hapo nikaanza kupata taarifa nyingi ambazo zilinitisha na kunipatia matumaini.

Siku moja nilitafutwa na mtu mmoja ambaye ni mzima na kada wa CCM. Kwa kuwa mtu huyo tunaheshimiana na kwa kuwa aliaminishwa ya kuwa mimi nilikuwa natumiwa na 'mabeberu'; ilibidi nimueleze pia baadhi ya mambo ambayo yalikuwa yanamzunguka Rais. Nilifanya hivyo ikiwa kinga yangu kwani nilijua kuwa ataelewa mazingira yangu na hivyo ataweza kupangua hoja dhaifu dhidi yangu akiwa katika 'Pango la Wakilindi'. Aliishia kunikodolea macho na ndipo tukaagana akiwa kama mtu asiyeamini.

Lakini kabla mtu huyo hajaondoka, aliniuliza: "Wewe umejuaje habari hizi'? Nikamjibu kuwa: "Mimi ni mskofu wa mnyororo na pia mimi ni askofu wa kiapo"! Mambo haya yaliaminiwa pia kwangu chini ya kiapo kwa hiyo nisingeyasema hadharani wakati ule na hata sasa. Hapa sio mahali pake kuelezea kisa cha askari aliyeacha kufanya ibada baada ya kushiriki kuwaua watu na baadaye kumbukumbu za watu wale zikawa zinamjia na kuharibu akili yake.

Mambo haya ni ya kitubio na kwa hiyo mtu ye yote atakayemuendea Mchungaji (Padri) au Askofu kwa kitubio, jambo lile linabakia katika kifua cha mtubishaji, anayetubu na Mungu.

Taarifa za kuchapishwa kwa kitabu cha Erick Kabendera zimeanza kusambaa kwa kasi sana mitandaoni siku ya leo tarehe 3 Januari 2025. Kitabu kinaitwa: 'In the Name of the President: Memoirs of a Jailed Journalist'. Nimesikiliza mahojiano ya Erick Kabendera kuhusu kitabu hicho. Nimeanza kufuatilia maudhui ya kitabu. Mengi ya mambo anayojadili ni sehemu ya yale niliyojulishwa kama 'sisi Askofu'! Ila sikutarajia mambo yale yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu. Ujasiri wa Kabendera unaivuka mipaka ya Nshamba na Kamachumu.

Ninaamini watu ambao walinishangaa kwa nini mimi nilijitoa muhanga kwa ajili ya kutetea haki nchini sasa wataanza kuelewa baada ya kuona na kusoma kitabu cha Erick Kabendera. Taarifa nyingi zilizofikishwa katika kilindi cha moyo wangu ziliishurutisha nafasi yangu kuchukua ili kupaza sauti na kutetea pale nilipoweza. Lakini pamoja na uropokaji wangu, mambo ambayo yalitiwa muhuri (sealed) katika moyo wangu yameamriwa na dhamiri iliyo kuu ili yasiyoke.

Kitabu cha Kabendera kitasaidia katika mambo muhimu. Kwamba tukisome na kumjua Rais Magufuli nje ya uelewa uliojulikana. Baada ya hapo, tuone kuwa alikuwa binadamu kama sisi na mwenye mapungufu na kisha tumsamehe. Kikubwa, kama jamii tutafute njia ya kuponya ikiwemo kuondoa vimelea au masalia ya yale aliyoayaasisi ambayo hayakuwa mazuri na hili itawezekana kama tutasoma na kuielewa sura ya mwisho ya Kitabu cha Kabendera.

Kitabu hiki kinaposambazwa na kusomwa ni vizuri tujue kuwa kinayahusu maisha fichika ya Rais Magufuli na sio maisha ya familia na ukoo wake. Hatuhitaji kwa namna yeyote kuwaona ndugu hata familia kama sehemu ya mambo aliyoyafanya kama Rais kwani nao walikuwa ni washangaaji kama sisi.

Mwisho, natoa wito kwa viongozi wa dini walio karibu na familia ya Ben Sanane na familia ya Azorly Gwanda kuzifikia kwa ajili ya huduma ya kiroho. Kupitia kitabu cha Erick Kabendera na mahojiano yake ni rasmi sasa ya kuwa umma umejulishwa kuwa watu hao hawapo pamoja nasi katika maisha haya.

Hekima iliyo ndani ya kilindi cha moyo wa Rais Samia inaweza kumsaidia afanye nini kwa ajili ya familia hizo. Bila shaka, CHADEMA itatafuta namna njema ya kuhitimisha kwa heshima kwa kumkumbuka Ben, mwanachama na Msaidizi maalum wa Mhe. Mbowe. Kadhalika, Gazeti la Mwananchi litaona pia namna ya kulihitimisha l kwa heshima ya Azorly, aliyekuwa mtumishi.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 3 Januari 2025; saa 2:00 usiku
Pascal Mayalla naomba ulete ule Uzi wako, wajue wasiojulikana watakaojulikana! Kumradhi kama nimekosea title! Ingawa wanasema wewe Ndio ulimchoma Kabendera kwenye Mamlaka za Jiwe!
 
Pascal Mayalla naomba ulete ule Uzi wako, wajue wasiojulikana watakaojulikana! Kumradhi kama nimekosea title!
karibu Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana
Ingawa wanasema wewe Ndio ulimchoma Kabendera kwenye Mamlaka za Jiwe!
hili la mimi kumchomea EK ni kweli nilihisiwa,alipofiwa na mama, kwanza nilimuombea kwa JPM Personal Plea Kwa Rais Magufuli: Kama ameweza kuwasamehe wabakaji, wauaji, mafisadi, wahujumu, anaweza pia kumsamehe Eric Kabendera, amzike mama yake
Mimi ni miongoni mwa waandishi tuliomzika mama yake EK, kisha nikajibu tuhuma Pascal Mayalla ndiye aliyemchongea Erick Kabendera kwa dola
Nikiwa UK, nikamtafuta,akanijulisha jinsi alivyokuwa akipelekewa print out za jf jinsi ninavyomchomea!。 Thanks God he is an intelligent man,angekuwa mjinga mjinga angeamini huo ujinga!
P
 
Kwa tafisiri hiyo ni Kuwa Askofu anatuambia Kuwa Erick kabendera ndio Amekuja Kuverify Kuwa Azory Gwanda na Ben Saanane wamefariki? Duh
 
Anataka kubariki drama za kitabu n ngumu sana kusahau mazur ya magufuli marais wote wana mazur na mabaya yao kwa nn wamekomalia kwa magu tu
Mkuu, hilo swali, 'kwa nini wamekolia kwa Magu" jiuluze wewe, tafakari kwa upana na undani wake, ukiwa neutral, bila upande.
 
Haisaidii, sasa kama Magu alikuwa muuaji kina ben watafufuka? Hakuna cha maana zaidi ya kupandikiza chuki kwenye hilo likitabu lenu la uongo na kutunga.
Inasaidia Sana kuweka kumbukumbu ili Kama taifa
Kwa maneno mengine, Askofu anatuthibitishia kwamba yaliyoandikwa katika kitabu cha Kabendera ni kweli kwani naye alipewa taarifa hizohizo ila hakuwahi kuzisema kokote.

Ndio maana yake.

Askofu ni Shahid muhim ikiwa Kabendera atahojiwa.

Kabendera hajakurupuka ,, aliyoyasema yapo vifuani mwa wengi.
 
Ukitaka kujua mtu muongo aliyekubuhu wana sifa moja za kufanana wawe maaskofu au yeyote utasikia marehemu aliniambia wakijua marehemu hawezi fufuka kujitetea au kusema muongo huyu Askofu

Askofu Mwamakula anaangukia kwenye hilo kundi la waongo wabobezi kwa nini hakusema hayo Magufuli akiwa hai?
Nilitegemea aina hii ya coments
 
Back
Top Bottom