BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
WAKATI WA KIKWETE TULIACHA KIPOLO, TUTAKIMALIZIA WAKATI WA MAGUFULI!
Mwishoni mwa mwaka jana tulipotangaza adhma ya kuandaa "Matembezi ya Hiyari" kuanzia Januari 2021 kwa lengo la kuuhamisha umma ili kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na kuandika Katiba Mpya, wapo watu waliokuwa na wasiwasi kama tutafanikiwa! Andiko hili limelenga kuwaelewesha watu kuhusu sababu zitakazopelekea kampeni hii kufanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu!
Rais Magufuli yupo katika kipindi chake cha mwisho cha kikatiba, hivyo Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya haviwezi kumuathiri yeye binafsi. Kwa sababu hiyo, hawezi kukubali kuchafua jina lake kwa kutumia nguvu dhidi ya wananchi kwa lengo la kutaka kuvuruga mchakato ambao hauwezi kumuathiri yeye binafsi.
Kwa kuwa tunauanza mchakato mapema, tofauti na wakati wa Kikwete ulipoanza mwishoni mwa kipindi chake cha mwisho, safari hii tuna muda wa kutosha kukamilisha mchakato huu kabla Rais Magufuli hajamaliza kipindi chake.
Watakaotaka kukwamisha kampeni yetu ni kundi dogo lenye nguvu ndani ya CCM ambalo linakusudia kumrithi Rais Magufuli na hivyo kutaka kutumia udhaifu wa Katiba ya sasa katika kuingia Ikulu. Lakini kwa kuwa tunao muda wa kutosha kuanzia sasa, kwa neema ya Mungu tutaweza kulidhibiti kundi hili kabla hata halijaanza kuvuruga! Pia, ndani ya CCM kuna nguvu kubwa inayoshinikiza Katiba Mpya. Mfano mzuri ni sauti ya Mzee Warioba na kitabu cha Mkapa. Sambamba na hayo, kundi 'lililodhibitiwa' ndani ya CCM ambalo ndilo kubwa, halitakubali kundi 'lile dogo' liendelee na udhibiti wake, hivyo kutakuwa na uungwaji mkono mkubwa kutoka ndani ya CCM!
Tayari ndani ya CCM kumeanza kumeanza kusikika manung'uniko yanayoonyesha wazi kuhusu udhaifu wa Katiba iliyopo unayowafanya wateule wa Rais kuwa wababe zaidi.
Matokeo ya Uchaguzi uliopita yameacha maumivu yasiyoelezeka kwa vyama upinzani. Hii itasaidia kuvifanya vyama vya upinzani kuunganisha nguvu zaidi katika kudai Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya kuliko kipindi kingine chochote kile katika historia ya nchi.
Jumuiya ya Kimataifa ambayo imeionyeshea kidole Tanzania kwa kuminya demokrasia, haki na kukiuka utu wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita inafuatilia kwa makini sana yanayoendelea nchini. Serikali ya Magufuli haiwezi kuendelea kujichafua mbele ya Jumuiya ya Kimataifa kwa kuvuruga "Matembezi ya Hiyari" wakati jambo lenyewe linalotafutwa haliwezi kumuathiri Rais aliyeko madarakani.
Kitendo cha Askofu kujitolea kuongoza "Matembezi ya Hiyari" kinatoa msisimko na nguvu ya ziada. Askofu huyo anao uzoefu wa kutosha kwa kuwa wakati wa Kampeni za Uchaguzi alizunguka nchi nzima akitoa kauli nzito kwa ujasiri mkubwa na katika mazingira ya hatari. Hivyo, hakuna wasiwasi kuwa Askofu huyo ataweza kukimbia au kuogopa na kutelekeza mapambano!
Uwepo wa Askofu na kuwa mstari wa mbele kutasaidia kuyaunganisha makundi mbalimbali ya kisiasa na kijamii nchini hasa ikizingatiwa kuwa Askofu siyo mwanachama na hana uongozi wowote wa chama cha siasa nchini.
Wafanyakazi wa Serikali na wafanyabiashara ni makundi yaliyoumizwa sana kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi. Makundi haya yanatarajia kutoa msaada mkubwa usio wa moja kwa moja katika kampeni hizi. Tukifanikiwa kujenga nguvu na matumaini kwa makundi haya pamoja na la wasiokuwa na ajira tutanikiwa kwa kiwango kikubwa!
Acha woga! Sambaza elimu hii na jiandae kuingia barabarani pamoja na Askofu! Imeandikwa: "kwa jasho lako ndipo utakula"! Pasipo kupambania haki haiwezi kudondoka yenyewe?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula.