DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Askofu wa Jimbo Katoliki la Mahenge, Mhashamu Agapiti Ndorobo amesema kuwa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ni vyema kuchagua Kiongozi anayefaa, na anayejali kila mmoja bila kuangalia Dini, rangi, kabila, wala utaifa.
Askofu Ndorobo ameyasema hayo leo Oktoba 3, 2025 wakati akitoa Homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 75 ya Seminari ya Mtakatifu Francis – Kasita, jimboni humo.
Aidha, Askofu huyo amewataka Waamini kujitafakari na kuona kwamba wamekuwa wajumbe wa Kristo kwa kiasi gani, hasa katika haki, kuleta amani, pamoja na kutenda mema.
“Na ndiyo maana ndugu zangu, ni lazima tufahamiane, Uchaguzi unakuja, ni lazima tuchague mtu anayefaa, kwa sababu anatuona, anatujali kila mmoja wetu, bila kujali Dini, rangi, kabila, na utaifa. Na hicho ndicho kinachotakiwa,” amesema Askofu Ndorobo.