Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Baba Askofu Severin Niwemugize
Mawazo ya waliomo humu Ndani ya Precision air kabla ya uokozi ni mawazo ya kipekee.
Hawawazi benki wana shilingi ngapi, hawawazi Simu ya macho 3/iphone 14 pro max, hawawazi majumba ya kifahari na magari aina ya Lexus v8.
Hawawazi kula bata George and Dragon, hapo walipo wanawaza "Yesu na sala zao za Mwisho"
Hawawazi kwamba Nina PHD[Oxford or Havard], Nina Masters[SAUT au Makumira], huko nje Kuna wavuvi wameishia darasa la 7, hawajui hata kiingereza Cha kusema Yes,
Walioko ndani maji yanazidi kuingia wanatamani maisha ya wavuvi wasio na uwezo wa kupanda ndege yawe yao, mkojo unawatoka na haja kubwa inawatoka.
Wangeambiwa "toeni milioni 10 Ili tuwatoe" wangetoa, wangeambiwa "jivueni Vyeti vya elimu yenu mseme nyie ni darasa la 7 Ili muokoke" wangekubali.
Ni wema wa Mungu hawa watu wameokoka.
Haya maisha tuishi kama tupo ndani ya hii ndege huku hatujui tutaokolewa/opolewa saa ngapi.
Ukiishi kama hawa watu hautatupa chakula, hautadharau yoyote hata kama hajasoma, hautaringia pesa zao, wala hautaringia baba Yako eti ni waziri ndio maana Unaweza kutukana yoyote.
HAUTAONEA MTU