Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
PICHA: Askofu Severine Niwemugizi
Toka mezani kwa Askofu Severine Niwemugizi
Tumesikia pendekezo la kikao cha ushauri cha mkoa wa Geita kuhusu uundwaji wa mkoa mpya wa Chato. Lakini ushauri wa mkoa wa Geita tu hautoshi kufanya uamuzi. Kagera zaidi inahusika katika hili kama wilaya zake mbili zitamegwa.
Ingetazamwa historia mkoa usingeitwa Chato. Mtawala wa kijerumani aliweka ngome ya utawala wake Biharamulo, akiheshimu kuwa hapo palikuwa makao ya Chifu wa Rusubi ambayo Chato ilikuwa sehemu yake. Na hata hayati JPM alianza harakati za kisiasa ikiwa Chato ni sehemu ya wilaya ya Biharamulo na jimbo la uchaguzi la Biharamulo.
Kwa haki nionavyo mimi kugawa Kagera na Kigoma ili kuunda mkoa ingekuwa ni kutazama mahitaji ya raia zaidi. Ukweli wazo la awali katika awamu ya nne ilikuwa kuunda mkoa kwa kutenga Kigoma na Kagera. Ukizingatia kuwa kanda ya magharibi ya Ukaguzi wa elimu ina mikoa hii miwili. Fikiria makao ya kanda ni Kigoma. Mtu anapaswa kusafiri zaidi ya km 700 toka Bk hadi Kigoma!
Najua mazungumzo yalishaanza. Halmashauri za kakonko, Biharamulo na Kibondo zilishapiga hatua za kuafikiana kuunda mkoa. Ngara ingepanda basi hilo. Nilisikia makao huenda yangekuwa Nyakanazi.
Awamu ya tano ikaupiga mkasi mpango wa mkoa ule na kuanza wa Rubondo. Huu ulikuwa na msukumo unaoakisi ubinafsi tu. Yaani toka Geita hadi Chato km zisizofika 100 uwe mkoa, wakati mtu anapiga km 700 toka Bk hadi Kg!! Inashangaza tunavyowaza na kupanga, si kwa maslahi ya raia kweli bali ya watawala.
Mama Samia Suluhu hassan asishinikizwe na kauli za kumpima kwa kutekeleza mipango iliyokuwepo ya JPM. Ashauriwe vizuri kwa kutazama uhalisia wa mahitaji ya kiutawala na maendeleo ya watu. Kutangaza mkoa kwa kuenzi watawala tu si kigezo kizuri, vinginevyo aanze na mkoa wa Butiama kwa Baba wa Taifa!