Askofu Niwemugizi apinga hoja ya Chato kuwa mkoa. Ataka Rais Samia asishinikizwe bali ashauriwe vizuri

Askofu Niwemugizi apinga hoja ya Chato kuwa mkoa. Ataka Rais Samia asishinikizwe bali ashauriwe vizuri

Yule Nduli na fashisti aliwakanyaga sana maaskofu waliokua na mawazo tofauti nayeye. Acha watu wateme nyongo zao.
Sawa ni maoni yake.

Hata hivyo Nduli ni kwa mtazamo wako
 
Mara niwemugizi mara mwamakula..mara katoliki mara morovian...

Mbona mnataka husisha kanisa na mambo ya ajabu ajabu
 
hii story inakuwa sawa na yule jamaa anayemchukia mfanyakazi mwenzake ambaye anamshahara mzuri kuliko yeye ingawaje wote wanafanya kazi moja. TZ hatuwezi endelea na unafiki wa kiwango hiki cha lami.
 
Hebu heshimuni maamuzi ya marehemu Jiwe , si alizuia kuongeza mikoa na wilaya mpya lini alitengua ?
Lakini chini ya kapeti akiongea na wazee wa chato akawaahidi kuifanya chato kuwa mkoa.
Rejea yule mzee mwakilishi siku ya mazishi pale chato.
 
unaongea kama nani Nchi hii wewe ?

imeshapita hio wewe wacha ngonjela …
 
Hivi tunaelekea wapi jamani? Mimi ni Mkatoliki japo siko Rulenge-Ngara. Leo ni siku ya Utatu Mtakatifu. Jee, ni sahihi mahubiri yajikite kwenye kutoa hoja za kwa nini mkoa uwe mahali fulani na siyo mahali fulani?

Tunaelekea wapi? Kama ni kumshauri Rais Samia, ingefaa kupitia kwenye vyombo husika kuhakikisha habari zinamfikia mlengwa. Hayo mahubiri, kama atayapata, yatakuwa kama tetesi tu. Askofu ana njia nyingi tu za kuweza kufikisha habari kwa mlengwa.
View attachment 1802465
PICHA: Askofu Severine Niwemugizi

Toka mezani kwa Askofu Severine Niwemugizi

Tumesikia pendekezo la kikao cha ushauri cha mkoa wa Geita kuhusu uundwaji wa mkoa mpya wa Chato. Lakini ushauri wa mkoa wa Geita tu hautoshi kufanya uamuzi. Kagera zaidi inahusika katika hili kama wilaya zake mbili zitamegwa...
Hivi tunaelekea wapi jamani? Mimi ni Mkatoliki japo siko Rulenge-Ngara. Leo ni siku ya Utatu Mtakatifu. Jee, ni sahihi mahubiri yajikite kwenye kutoa hoja za kwa nini mkoa uwe mahali fulani na siyo mahali fulani, badala ya mafundisho kuwa juu ya Utatu Mtakatifu? Kama ni kumshauri Rais Samia, ingefaa kupitia kwenye vyombo husika kuhakikisha habari zinamfikia mlengwa.

Hayo mahubiri, kama atayapata, yatakuwa kama tetesi tu 'anazosikiasikia'. Askofu ana njia mbadala za kuweza kufikisha habari kwa mlengwa. Asipoteze muda kuleta mambo yasiyohusika na dini. Muumini hahitaji kwenda kanisani kusikia mawazo ya Askofu kuhusu mkoa uwe wapi.
 
hii story inakuwa sawa na yule jamaa anayemchukia mfanyakazi mwenzake ambaye anamshahara mzuri kuliko yeye ingawaje wote wanafanya kazi moja. TZ hatuwezi endelea na unafiki wa kiwango hiki cha lami.
Unaelewa maana ya Unafiki kweli wewe??.Hivi mtu km ameeleza maoni yake kwa kadamnasi bila kuficha kitu anakuwaje mnafiki??
 
View attachment 1802465
PICHA: Askofu Severine Niwemugizi

Toka mezani kwa Askofu Severine Niwemugizi

Tumesikia pendekezo la kikao cha ushauri cha mkoa wa Geita kuhusu uundwaji wa mkoa mpya wa Chato. Lakini ushauri wa mkoa wa Geita tu hautoshi kufanya uamuzi. Kagera zaidi inahusika katika hili kama wilaya zake mbili zitamegwa...
Safi sana Baba Askofu, haujawahi kutuangusha tangu enzi za Mwendazake, hadi Misa ya mwisho ya Mwendazake. Ila angalia wasiojulikana bado wapo ila mtoa amri ya kuteka hayupo.
 
Back
Top Bottom