#COVID19 Askofu Niwemugizi, asitisha Misa na Ibada zote Jimbo la Rulenge, awataka waumini Wasali Majumbani pia Wajikinge na Corona

#COVID19 Askofu Niwemugizi, asitisha Misa na Ibada zote Jimbo la Rulenge, awataka waumini Wasali Majumbani pia Wajikinge na Corona

Mungu kaagiza kuwa msiache kukusanyika huyo Askofu Nani amuige yeye anasema marufuku kukusanyika kwenye ibada!!! Mungu ni mkubwa kuliko huyo Askofu mpiga marufuku watu kukusanyika Ibadan. hakuna cha kuiga kwa huyo askofu mpagani
Mjinga wewe hospital huwa unafata nini?
 
Walipokusanyika kumuombea Tundu Lissu mliwapiga mabomu, wakati huo Biblia haikuwepo?
Hapa ndipo tatizo kubwa lililopo kanisa katoliki.Sheria za Kanisa hazotakiei kuwa juu ya sheria ya Mungu ambayo in Biblia.Biblia imeagiza watu wasiache kukusanyika kuabudu.Papa na Hugo askofu wanaagiza waumini wasikusanyike kuabudu Vatican na Jimbo la Rulenge Wapagani hao
Wamevunja sheria ya Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ndipo tatizo kubwa lililopo kanisa katoliki.Sheria za Kanisa hazotakiei kuwa juu ya sheria ya Mungu ambayo in Biblia.Biblia imeagiza watu wasiache kukusanyika kuabudu.Papa na Hugo askofu wanaagiza waumini wasikusanyike kuabudu Vatican na Jimbo la Rulenge Wapagani hao
Wamevunja sheria ya Mungu

Ni nani alikwambia ili sala yako ikubaliwe ni lazima ukusanyike na wenzio

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ni nani alikwambia ili sala yako ikubaliwe ni lazima ukusanyike na wenzio

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kusali na kuabudu Ni vitu viwili tofauti Sala waweza sali popote kuabudu lazima altare au madhabahu iwepo na inapatikana kanisani sio popote
 
Nawashauri Katoliki waliofungiwa wasiabudu makabisani huko Rulenge waende kusali makanisa yeyote watakayopenda ambayo hayajafungwa na wasirudi Tena Katoliki
 
Hapa ndipo tofauti ya 'baba askofu' na 'askofu' inaonekana.Ila labda amefikia malengo ya mapato, na wengine labda wanasubiri kutimiza malengo yao ya mapato. Ila wajue uchumi unashuka na mapato yao yatakuwa yanashuka.
 
Kanisa Katoliki Jimboni Rulenge-Ngara, wamesitisha kabisa Ibada/misa. Watu wasali nyumbani! Pia amewataka waumini wajikinge na COVID-19 na kuchukua tahadhari

Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge-Ngara limesema limesitisha Ibada za Misa, maadhimisho mengine yanayokusanya Waumini wengi Kanisani na sala za Jumuiya kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia Aprili 19, 2020

Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo hilo amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kutafakari alama za nyakati na kujifunza kutoka kwa watu wa Ulaya, Marekani na nchi za jirani na hatua ambazo Baba Mtakatifu alizichukua kwa kutoa maelekezo kwa Maaskofu Wakatoliki Duniani na namna ya kuadhimisha Ibada

Amesema pamoja na kumshukuru Rais Magufuli kutotoa amri ya kufunga Makanisa na Misikiti, akihimiza kufanya ibada kumuomba Mungu atunusuru na janga hili, kama Mchungaji wa Jimbo la Rulenge-Ngara ameamua kuchukua uamuzi huo

Aidha, Askofu Niwemugizi amesema pale itakapowezekana wataomba redio Kwizera irushe adhimisho la Misa fupi na Waamini wafuatilie redioni. Baada ya mwezi kuisha Kanisa litaangalia hali ilivyo ili kama iliongeze muda

Pia, amewataka mapadre kuadhimisha misa peke yao kwa niaba ya waumini kuwaombea na kuiombea dunia ili Mungu atunusuru na #COVID19 hili na kuagiza sala za Jumuiya kufanyika ndani ya familia kwa familia moja moja
View attachment 1422602

Askofu pekee. Kweli maisha yanaenda sababu ya maamuzi yetu. Naamu tunawajibika sababu ya kila tunaloamua

Nawashauri Katoliki waliofungiwa wasiabudu makabisani huko Rulenge waende kusali makanisa yeyote watakayopenda ambayo hayajafungwa na wasirudi Tena Katoliki
Wapumbavu ndo watafanya hayo, wakatoliki si mabwege ki hivyo
 
Back
Top Bottom