Askofu Niwemugizi: Rais Magufuli aliagiza nirejeshewe Passport yangu na alisema 'Wewe ni Askofu wangu utanizika'

Askofu Niwemugizi: Rais Magufuli aliagiza nirejeshewe Passport yangu na alisema 'Wewe ni Askofu wangu utanizika'

Askofu nae aache unafiki siku zote kwa nini hakutangaza ?ina mana hata Magufuli asingekufa ni lini tungejua kuwa alirejeshewa.hu msiba tutaona na kusikia mengi.

Kuna tetesi tena kilya kwa hery.

Naomba niishie hapo tafadhali.
Naona unachangia mada ambayo huijui vizuri. Ishu ya huyu Askofu ni ya muda mrefu. Aliingia kwenye ligi na Magu baada ya
Yule aliyesaidiwa kwenye matibabu yake ni yupi?
Askofu Mkuu wa DSM, Yuda Thadei Ruwa'ichi alipewa ndege ya Magu. Ili kumuwahisha kutoka KCMC kuja MOI kufanyiwa operesheni ya kichwa.

Mwingine aliyesaidiwaga ni Askofu Msaidizi Methodius Kilaini, enzi za Kikwete. Alipelekwa India kwa msaada wa JK
 
Upepo umevuma kwenda upande mwingine..."Askofu wa Makamanda" leo wamemgeuka!
Wasiojua ndio wanafikiri hivyo, soma maelezo ya Askofu katikati ya mistari kuna message kali.

Hakuunga mkono juhudi kama kina Kakobe, alibaki na msimamo thabiti ila karejeshewa paspoti yake baada ya Magu kuzidiwa
 
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi amesema aliyekuwa Rais wa Tanzania marehemu, John Magufuli aliagiza arejeshewe hati yake ya kusafiria na alimtamkia mara mbili kuwa kiongozi huyo wa kiroho ndiye atakayemzika.

Akizungumza leo Alhamisi Machi 25, 2021 katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato, Askofu Niwemugizi ambaye hakutaja muda maalum wa agizo la kurejeshewa hati hiyo, amesema Magufuli aliagiza idara ya uhamiaji kumrejeshea.

"Kwa kweli niwaambie mara mbili, Magufuli aliniambia, ‘wewe ni Askofu wangu utanizika. Mwaka ule 2015 akaniambia hivyo, mara ya pili akamwagiza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anirudishie passport akaniambia wewe ni Askofu wangu utanizika.”

Wasalaamaidi, soma: Askofu Niwemugizi wa Kanisa Katoliki aitwa Uhamiaji kuhojiwa juu ya uraia wake
Msituletee porojo,
Cha msingi hapa kwanini passport yake ilichukuliwa?
Sababu ni moja tu,Jiwe hakupenda kuambiwa ukweli.haiwezeksni mtu akupige ngumi ya jicho harafu akupereke hospitari,harafu umwambie asante.
 
..lakini swali dume hapa ni: Je, ni nani aliyeagiza watu wa immigration wampore askofu hiyo passport? Au ni kwamba watu wa uhamiaji waliamua tu kumnyanganya askofu hiyo passport kwa kujikomba tu na kumfurahisha meko??!!
 
Hapa kuna chai kidogo kwa hiyo alijuaje kwamba yeye atatangulia kufa amuache Askofu kiasi kwamba amwambie yeye ndo atamzika?
Kama kuku alikula mahindi kadhaa utajua. Achana na mambo ya kusaka utajiri na madaraka.
 
Hivi uhamiaji wangethubutu kumgusa askofu tena wa katoliki jimbo analotoka Rais bila baraka ya Rais?

Huyu Niwemugizi alichukiwa sana na Magu na uzuri huyu Askofu hakuwahi kunyamazia upuuzi.

Askofu Niwemugizi

Askofu Bagonza

Askofu Shoo ingawa kuna muda alinywea

Askofu Mwanakula

Historia itawakumbuka hamkuwahi kutukuza au kushabikia upuuzi.

Askofu Bagonza na fayaaaaa...
 
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi amesema aliyekuwa Rais wa Tanzania marehemu, John Magufuli aliagiza arejeshewe hati yake ya kusafiria na alimtamkia mara mbili kuwa kiongozi huyo wa kiroho ndiye atakayemzika.

Akizungumza leo Alhamisi Machi 25, 2021 katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato, Askofu Niwemugizi ambaye hakutaja muda maalum wa agizo la kurejeshewa hati hiyo, amesema Magufuli aliagiza idara ya uhamiaji kumrejeshea.

"Kwa kweli niwaambie mara mbili, Magufuli aliniambia, ‘wewe ni Askofu wangu utanizika. Mwaka ule 2015 akaniambia hivyo, mara ya pili akamwagiza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anirudishie passport akaniambia wewe ni Askofu wangu utanizika.”

Wasalaamaidi, soma: Askofu Niwemugizi wa Kanisa Katoliki aitwa Uhamiaji kuhojiwa juu ya uraia wake
Meko alipenda sana maigizo.
Kujitekenya na kucheka
 
Back
Top Bottom