Askofu Ruwa`ichi: Nyie mapadre nani aliwakataza msioe?

Askofu Ruwa`ichi: Nyie mapadre nani aliwakataza msioe?

Akioa anakuwa na wazazi wanne wanamtegemea tofauti asipooa anakuwa na wazazi wawili tu. Halafu wazazi wake waliomzaa wanaweza kutibiwa na Kanisa maana wamemtoa sadaka mtoto wao kwa ajili ya Kanisa. Ila akishaoa mambo yanakuwa mengi, ndio maana makanisa ambayo wachungaji wanaoa hawana taasisi nyingi eg shule ,vyuo, hospital na zinazoendeshwa kwa weledi kama Katoliki. Mfano mzuri shule za masista zinafanya vizuri kwa sababu masista hawana familia wanaziangalia hizo shule 24/7.
Ujinga mtupu, kwahyo hapa ndo umeongea point mwenyw?
 
Sio kwa ubaya,
Mtu unakataa kuoa kisa kumtumikia Mungu kweli?Hatya vipi nyie ambao hamjaoana.Je,wazazi wenu wasingeoana mgekuja kumtumikia huyo Mungu asiyetaka muoe.

Haya na wale masister mnazijua behind on the scene’s zao?

Je,Mungu yupo teyari kudanganywa kama ninyi navyofanya(kuzini)?
Kwa sababu binafsi hakuna mwanamume anayeweza kuishi siku 365 bila kulomba,uongo.
Tatizo ni Wito.
 
Sio kwa ubaya,
Mtu unakataa kuoa kisa kumtumikia Mungu kweli?Hatya vipi nyie ambao hamjaoana.Je,wazazi wenu wasingeoana mgekuja kumtumikia huyo Mungu asiyetaka muoe.

Haya na wale masister mnazijua behind on the scene’s zao?

Je,Mungu yupo teyari kudanganywa kama ninyi navyofanya(kuzini)?
Kwa sababu binafsi hakuna mwanamume anayeartweza kuishi siku 365 bila kulomba,uongo.
Mbona kama huelewi ? Kuna masharti yamewekwa sio lazima kama hauwezi basi , kama hao wamejitoa basi ni maamuzi yao .

Kuhusu watu kuoana mpaka kupata watoto , kuna watu hawana watoto ..Dunia unavyoina ndivyo ilivyo , maisha yapo duniani kama utazaa basi utakuwa uleta maisha ya kiumbe mwingine ambapo kuna majukumu ya kumlea , kama haujazaa wala haikuhusu ..Hivyo , kila mtu anaishi vile anavyotaka , hautodaiwa ada ya mtoto hamtomzaa ila ukimzaa kumlipia ada ni lazima.
 
Askofu yuko sahihi hakuna Mtu anayelazimishwa kuwa Padre, Upadre ni Wito kabla ya kuamua kuwa Padre inabidi kujitafakari kwa kina.
 
Ukimtumikia Mungu ndiyo imekatazwa usioe?, unaweza weka andiko la hilo katazo mkuu?, mwili ulio timamu lazima uwe na matamanio, Shahawa zinazalishwa kila leo zinatumika wapi?, au masista wapo kwa kazi hiyo? ndiyo maana wanapata maskandali kuwala vijana wanaofanya kazi huko Makanisani aisee.

Naona helewi kwa kina mambo haya!
Yesu alisema kuwa huwezi kutumikia mabawana wawili, mali na Mungu. Hiyo akionesha kuwa ukitaka kumtumia Mungu, ujitoe kwaajili ya Mungu, achana na mengine.

Kanisa Katoliki ndiyo kanisa pekee ambalo ni the most conservative institution, yaani ambalo halibadiliki, ndiyo maana msingi wake mkuu ni Mapokeo na Biblia.

MAPOKEO:
Mitume wa Yesu, mara baada ya kuchaguliwa kuwa mitume, waliokuwa wameoa, waliwaacha wake na familia zao moja kwa moja, wakabakia na kazi moja tu ya kumtumikia Mungu. Mitume ambao wakati wanachaguliwa kuwa mitume walikuwa hawajaoa, hawakuoa kabisa, walibakia hivyo. Katika kusisitiza hilo Mtume Paulo ameweka wazi kuwa kila mwanadamu ana karama yake, na akasema wenye karama ya kumtumikia Mungu wabakie kama yeye, yaani wasioe, lakini kama huwezi, nenda kaoe kuliko kuwaka tamaa.
 
Ukifuatilia historia ya dini ya katoliki ni kweli mapadri hawatakiwi kuwa na familia
na masista hivo hivo ni suala la historia sio dini dini ya katoliki na mapadri wanajua hilo!
 
Askofu yuko sahihi, nadhiri walioweka mapdre kulitumikis Kanisa Katoliki ndio inawazuia kuoa hawajuzuiliwa na askofu wala Papa.
 
Kwahiyo asipooa hata kaka na dada zake wa tumbo undugu unakatika?
Anakuwa ana ndugu wachache wa kuwahudumia ambao kwa connection ambazo mapadri wanazo anaweza kuwasaidia wakapata kazi sehemu nzuri za kuwaingizia kipato wakaacha kumtegemea.
 
Kweli kabisa mkuu,padre anaruhusiwa pia kuacha upadre aende kuoa tena ndoa ya kanisani Wala Haina shida kabisa,iwapo atashindwa kutunza nadhiri alizoweka,na hii habar ya kuchit watu wanachit tu hata waliokwenye ndoa
Walio kwenye ndoa wanachit sana hilo mbona linajulikana.
 
Hujamwelew askofu, aliposema upadri ni wito anamaanisha kabla ya mtu kuweka nadhiri ya upadri alijua kabisa akiwa padri hataruhusiwa kuoa.
Iweje wakishapata daraja la upadri ndio waone umuhimu wa kuoa wakati hakuna mtu aliyewashikia fimbo kuwa mapadri.
Hapo wanaonyesha walitafuta ajira badala ya kumtumikia Mungu.
Mtu aliyeingia upadre halafu baadaye aanze kusumbua na kutaka kuoa huyo hakuwa nae wito Aliingia huko ili afanye escapism tu.Aliyatoroka maisha ambayo yamemtangiza kwa mbele na tumejua uhalisia wake.Upadre siyo escapism ya maisha ya mtaani.
 
Hujamwelew askofu, aliposema upadri ni wito anamaanisha kabla ya mtu kuweka nadhiri ya upadri alijua kabisa akiwa padri hataruhusiwa kuoa.
Iweje wakishapata daraja la upadri ndio waone umuhimu wa kuoa wakati hakuna mtu aliyewashikia fimbo kuwa mapadri.
Hapo wanaonyesha walitafuta ajira badala ya kumtumikia Mungu.
Isitoshe Kanisa bado limetoa uhuru hata ikitokea Padre anataka kuoa, anaruhusiwa kuachana na Upadre, na kuingia maisha ya ndoa.

Sema tu kwa upande wangu pia nina mashaka na Watawa, na Mapadre walio wengi kusaliti viapo vyao vya kuishi maisha ya useja na kujitoa. Hivyo Kanisa linatakiwa kufanya tathmini ya kina ili kuomdokana na huu unafiki kwa baadhi ya watumishi wake.
 
Wakuu nyie mnaionaje hii?

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus Ruwa`ichi amesema upadre ni wito, akieleza kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakimuuliza kwa nini mapadre wa Kanisa Katoliki hawaruhusiwi kuoa. ‎

Akizungumzia suala hilo, amesema mara kwa mara amekuwa akipokea watu ofisini kwake wanaotaka kujua sababu za mapadre kutooa, huku akiwataka kutafakari maana ya wito wa upadre. ‎ ‎“Mara chache wanakuja watu ofisini kwangu wananiuliza kwa nini unawakataza mapadre wasioe. Nyie mapadre mpo hapa, nani aliyewakataza msioe? Kuwa padre siyo balaa au nongwa, upadre ni wito,” amesema. ‎ ‎

Kauli hiyo imeibua mjadala kuhusu wito wa upadre na utaratibu wa Kanisa Katoliki kuhusu useja wa mapadre. ‎

Lakini ukiifikiria hii kauli haimaanishi kuwa mapadre wanatakiwa kuoa, kwasababu upadre ni wito basi sadaka yao ni kuji commit wasioe. Maana askofu amesisitiza kuwa kila wito una sadaka yake, kwahivyo pengine wao kutooa ndio sadaka ya wito wao. Au nyie mnasemaje wenzangu?

Hebu wenye ujuzi kuhusu hili mtueleweshe hapa aisee.
View attachment 3696701
Askofu yuko sahihi,
hakuna padre aliekatazwa kuoa, mapadre walikua na fursa ya kuoa kabla ya kujitoa sadaka ya kumtumikia Mungu pekee🐒
 
Wakuu nyie mnaionaje hii?

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus Ruwa`ichi amesema upadre ni wito, akieleza kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakimuuliza kwa nini mapadre wa Kanisa Katoliki hawaruhusiwi kuoa. ‎

Akizungumzia suala hilo, amesema mara kwa mara amekuwa akipokea watu ofisini kwake wanaotaka kujua sababu za mapadre kutooa, huku akiwataka kutafakari maana ya wito wa upadre. ‎ ‎“Mara chache wanakuja watu ofisini kwangu wananiuliza kwa nini unawakataza mapadre wasioe. Nyie mapadre mpo hapa, nani aliyewakataza msioe? Kuwa padre siyo balaa au nongwa, upadre ni wito,” amesema. ‎ ‎

Kauli hiyo imeibua mjadala kuhusu wito wa upadre na utaratibu wa Kanisa Katoliki kuhusu useja wa mapadre. ‎

Lakini ukiifikiria hii kauli haimaanishi kuwa mapadre wanatakiwa kuoa, kwasababu upadre ni wito basi sadaka yao ni kuji commit wasioe. Maana askofu amesisitiza kuwa kila wito una sadaka yake, kwahivyo pengine wao kutooa ndio sadaka ya wito wao. Au nyie mnasemaje wenzangu?

Hebu wenye ujuzi kuhusu hili mtueleweshe hapa aisee.
View attachment 3696701
Tuseme wana nyumba ndogo mtaani!
 
🤣🤣🤣 statement yake ipo very trick, kiufupi hawalazimishwi kuwa mapadre
 
Back
Top Bottom