Wakuu,
Wananchi tunaangusha hii nchi, kubaki kulalamika vitendo 0, ikifika muda wa kupiga haoooo tunaenda kupigia mifuko ya sukari na vitenge🤦♂️🤦♂️
====
Ni kweli kama maaskofu wa tanzania tumetoa matamko mengi, na hilo siyo jambo ambalo tunalifanya kwa kukurupuka, ni jambo ambalo tunalitambua kama jukumu la kinabii la baraza letu.
Endapo baraza letu litakaa kimya wakati tunapitia vipindi vigumu nchi yetu itaenda pabaya. Tunashukuru kwamba tunapotoa tamko, raia wa nchi hii hata ambao siyo wakatoliki wanashukuru na kuthamini.
Sasa kama yanafanyiwa kazi au lah ni shauri ya wale wanaohusika, ni jukumu lao kuwa wasikivu, kujipanga na kufanya mambo inavyopasa, wasipofanya hivyo raia wanayo haki na fursa ya kuwawajibisha
Askofu Rwaichi akijibu swali la mwandishi alilouliza juu ya matamko mengi wanayotoa na kama yanafanyiwa kazi na kuwa na faida yoyote