Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Akizungumza kwenye Ibada ya mazishi ya marehemu Johara Mtei , ambaye ni Mama Mkwe wa Freeman Mbowe , Aliyeko gerezani kutokana na kesi ya uzushi ya Ugaidi , amesema hata kama siasa ni mchezo mchafu lakini walio kwenye madaraka wajaribu kutenda haki badala ya kutenda mambo yanayovuka mipaka ya utu maana hayana mwisho mwema .
DR Shoo ametoboa siri kwamba yeye na maaskofu wenzake ndio waliomuita na ndio waliomshauri Mbowe kusitisha operesheni UKUTA ili kuepusha mauaji ya Raia wasio na hatia na akatii na kusitisha maandamano yale , Bila kumung'unya maneno Askofu Shoo amesikitishwa sana na kitendo cha Mbowe kusingiziwa Ugaidi , na Amemuomba Dr Lilian ambaye ni Mke wa Mbowe kuwa na uvumilivu