PreGE2025 Askofu Shoo: Maslahi binafsi yasitupofushe dhidi ya mazuri ya Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
"Sisi Viongozi wa dini, Viongozi wa kiroho tunahitaji kuhimiza pamoja na haya mambo haya ya kisiasa au mambo yanayohusu uchaguzi Mkuu, Kuhimiza maboresho katika utoaji wa huduma muhimu kwa jamii. Ustawi wa watu unategemea upatikanaji bora wa huduma za afya, elimu, maji safi na huduma nyingine za kijamii.

Tangu mwanzo taasisi za dini zimetunza sana huduma hizi, ni haki ya kila mtu kupata elimu iliyo bora, kupata tiba iliyo bora, kupata maji safi na kadhalika. Tunashukuru sana juhudi kubwa za serikali yetu chini ya Uongozi wa Rais wetu,kweli mama Samia Suluhu Hassan katika uboreshaji wa huduma hizi za kijamii na maendeleo ya Taifa.

Moja ya matatizo tuliyonayo watanzania ndiyo hiyo ya watu wenye maslahi binafsi kutaka kutushawishi tusione yale yaliyo mema, tena yaliyo mengi tu yaliyokwisha kufanywa na serikali hii ya awamu hii ya sita.

Ni wajibu Viongozi wa dini kuwaambia aaha fungueni macho tazameni yale ambayo yamefanyika, pongezeni hayo, muappreciate hayo, sio kuishi katika kulalamika wakati wote. Haina maana kupuuzia yale ambayo hayajafanyika vizuri ambayo tunahitaji yafanyike lakini lazima tuone pale pa kupongeza tupongeze, pakushauri tushauri, pa kukemea tukemee.

Kwaajli hiyo kwa pamoja na kwa umoja wetu na hapa tumefanya vilevile, tunamuombea Rais wetu Mungu azidi kumpa nguvu, ampe ujasiri wa kufanya maamuzi, ampe afya njema na aweke kando wale wote ambao kwa hila wanataka kuonesha kwamba uongozi huu haujafanya kitu. Ni wajibu wetu kama Viongozi wa dini tumtie moyo.

Tunapenda kutoa wito pia kwa Vyombo vya dola vilivyopo chini ya mamlaka yake kuwa na weledi na uadilifu mkubwa katika kutimiza majukumu yao mahali pengine tumeona pametumika nguvu ya ziada na hata watu wasio na hatia wakati mwingine kujeruhiwa, kupigwa na kadhalika, haya tunapenda kusema hatupendi kuyaona."- Askofu Fredrick Shoo kwenye Mkutano wa Viongozi wa dini Mkoani Singida.
 
Hakuna aliyesema Raisi Samia hafai kwa kila kitu. Hata Magufuli hakuwa mbaya kwa kila kitu. Ila sasa, pale wanapokuwa wabaya, wanakuwa wabaya kwelikweli kiasi cha kukosa sifa za kuwa kiongozi. Hata muuaji Hitler alikuwa na uzuri wake.
 
Alipotufikisha panstosha kabisa..Atuache tuendelee na wengine.Kiongozi yy tu. Wapo wengi wenye uwezo mkubwa wa kututoa kwenye hili tope zito
 
"Sisi Viongozi wa dini, Viongozi wa kiroho tunahitaji kuhimiza pamoja na haya mambo haya ya kisiasa au mambo yanayohusu uchaguzi Mkuu, Kuhimiza maboresho katika utoaji wa huduma muhimu kwa jamii. Ustawi wa watu unategemea upatikanaji bora wa huduma za afya, elimu, maji safi na huduma nyingine za kijamii.

Tangu mwanzo taasisi za dini zimetunza sana huduma hizi, ni haki ya kila mtu kupata elimu iliyo bora, kupata tiba iliyo bora, kupata maji safi na kadhalika. Tunashukuru sana juhudi kubwa za serikali yetu chini ya Uongozi wa Rais wetu,kweli mama Samia Suluhu Hassan katika uboreshaji wa huduma hizi za kijamii na maendeleo ya Taifa.

Moja ya matatizo tuliyonayo watanzania ndiyo hiyo ya watu wenye maslahi binafsi kutaka kutushawishi tusione yale yaliyo mema, tena yaliyo mengi tu yaliyokwisha kufanywa na serikali hii ya awamu hii ya sita.

Ni wajibu Viongozi wa dini kuwaambia aaha fungueni macho tazameni yale ambayo yamefanyika, pongezeni hayo, muappreciate hayo, sio kuishi katika kulalamika wakati wote. Haina maana kupuuzia yale ambayo hayajafanyika vizuri ambayo tunahitaji yafanyike lakini lazima tuone pale pa kupongeza tupongeze, pakushauri tushauri, pa kukemea tukemee.

Kwaajli hiyo kwa pamoja na kwa umoja wetu na hapa tumefanya vilevile, tunamuombea Rais wetu Mungu azidi kumpa nguvu, ampe ujasiri wa kufanya maamuzi, ampe afya njema na aweke kando wale wote ambao kwa hila wanataka kuonesha kwamba uongozi huu haujafanya kitu. Ni wajibu wetu kama Viongozi wa dini tumtie moyo.

Tunapenda kutoa wito pia kwa Vyombo vya dola vilivyopo chini ya mamlaka yake kuwa na weledi na uadilifu mkubwa katika kutimiza majukumu yao mahali pengine tumeona pametumika nguvu ya ziada na hata watu wasio na hatia wakati mwingine kujeruhiwa, kupigwa na kadhalika, haya tunapenda kusema hatupendi kuyaona."- Askofu Fredrick Shoo kwenye Mkutano wa Viongozi wa dini Mkoani Singida.
View attachment 3327018
Bishop your age is done , you have nothing to loose! My kids are still young I am fighting for the better Tanzania for them.
Please Bishop go and rest in peace with your heart!
 
Back
Top Bottom