Nukuu ya mazungumzo ya kwenye video
"Wapinzani wanailaumu Serikali, wanalaumu mifumo, wanalaumu mahakama, wanalaumu Jeshi la Polisi, na kadhalika.
Lakini wanasimama viongozi wa Serikali, wanawalaumu wapinzani, wanalaumu Diaspora, wanalaumu watu walioko nje.
Hakuna anayekaa mahali pa kuleta suluhisho. Sasa sio kwamba naionea Serikali. Serikali ndio inatakiwa kuwajibika kwetu na sio wapinzani. Na inawajibikaje kwetu? Kwa kutupa matumaini, ituambie wana suluhisho gani juu ya hilo tatizo, sio na wao wanawalaumu tena wengine. Watuambie wametengeza mfumo gani wa hayo yanayolalakiwa, sio na wao walalamike.
Sasa Serikali ikiwa ya walalamikaji, wanaondoa matumaini. Unasikiliza hotuba za watu, unasikiliza maneno ya watu, unasema sasa kwa hiyo tunafanyaje? Bwana eh, mimi nimekuwepo tangu wakati wa Nyerere. Wakati wa Nyerere kulikuwepo na matishio ya kweli. Nyerere aliwahi kujaribiwa kupinduliwa, hatukusikia kwenye vyombo vya habari, hakuna mtu aliyesema. Walipokamatwa ndio taarifa zote zikaanza kutolewa kuwa huyu alikuwa anafanya moja, mbili, tatu. Sijui kama unanielewa.
Idi Amin wakati wa Nyerere, tishio kubwa aliingia kabisa Tanzania, akavamia Tanzania. Hatukusikia, wakakaa, ikao vyao, wakatengeneza mambo yao, wakachuja, paap, Nyerere akatoa hotuba. Hotuba aliyoitoa ilikuwa ya hiki ninachokisema ya matumaini. Alisema, uwezo wa kumpiga tunao, sababu za kumpiga tunazo, nia ya kumpiga tunayo. Tunataka dunia ituelewe hivyo. Kila mtu aliinuka kusema hii vita tunashinda. Wakajiunga watu, tukashinda ile vita.
I am kindly encouraging, urging, viongozi wa Serikali wa ngazi zote wajifunze na waanze kutoa matumaini. Tusiwaone wakilalamika. Na tukisema hivyo hatutumii mamlaka, tunawaomba wasiendelee kulalamika."