PreGE2025 Askofu wa Anglikana aomba viongozi wa dini kuwa na mwakilishi bungeni

PreGE2025 Askofu wa Anglikana aomba viongozi wa dini kuwa na mwakilishi bungeni

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mambo ya Kaisari mpeni Kaisari, na mambo ya Mungu mpeni Mungu

Kwa hiyo huyu Askofu anapingana na Kristo?

Siasa si ya Mungu na Mungu si mwanasiasa
 
Hilo bunge litakuwa lina udini wa kufa mtu. Kila dini na dhehebu litakuwa na muwakilishi wao, ongeza waganga wa kienyeji na wapagani jumlisha na waabudu shetani itakuwa ni vurugu tupu bungeni. Kama vipi viongozi wa dini wasimame wenyewe au kwa vyama vyao wagombee sambamba na wengine kama wanaona inapendeza. Au wajiunge na vyama vya siasa kama kina gwajima, msigwa, mwanjala, nantse wagombee ubunge kupitia ccm, chadema, act, cuf, chauma, nccra, tlp, tadea nk.
Kwa hoja hii nimekuelewa, bado machief wa kila mkoa nao watataka wawakilishi
 
Wakuu,

Askofu wa Pili wa Kanisa la Anglikana, Jimbo la Tarime mkoani Mara, John Nyaitara, ameiomba serikali kuwapa viongozi wa dini nafasi ya uwakilishi bungeni ili waweze kushughulikia changamoto zinazozikumba taasisi za dini.

Askofu Nyaitara alitoa ombi hilo juzi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, wakati wa ibada ya kusimikwa kwake, akibainisha kuwa taasisi za dini zinakabiliwa na changamoto zinazohitaji utatuzi kupitia uwakilishi rasmi bungeni.

Soma pia: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Tunaomba viongozi wa dini wawe na uwakilishi bungeni ili baadhi ya mambo yanayozitatiza taasisi za dini yashughulikiwe kabla ya kufanyika kwa maamuzi na kutungwa kwa sheria mbalimbali," alisema Askofu Nyaitara.

Mbali na ombi hilo, aliiomba serikali kupunguza kodi katika shule, hospitali na taasisi nyingine za dini kwa kuwa zinatoa huduma kwa gharama nafuu kwa wananchi.


"Kodi inavyoongezeka, wananchi wengi wanashindwa kumudu gharama za huduma. Tunaomba serikali ifikirie kutoa ruzuku kwa taasisi hizi ili ziendelee kutoa huduma bora kwa jamii," aliongeza.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, aliwataka viongozi wa dini, wazazi na walezi kushirikiana katika kupambana na mmomonyoko wa maadili unaoikumba jamii kutokana na athari za utandawazi.

"Jamii yetu inakabiliwa na changamoto za mmomonyoko wa maadili. Ni jukumu la viongozi wa dini, wazazi na walezi kuhakikisha tunakemea hali hii ili tuandae taifa bora la baadaye," alisema Kanali Mtambi.

Soma, Pia: Viongozi wa Dini waomba kwa Rais Samia kuwa na uwakilishi Bungeni kulingana na Madhehebu Yao. Mimi napinga Wazo hilo

Source: Nipashe
Huyu Akofu wa Anglikana ana tatizo la msingi.
Wito wake si katika utunzi wa sheria bali ushawishi kwa waumini ambao wanaingia bengeni ama wabunge.
Akishindwa kuwashawishi wananchi wake waumini, hata akienda Bungeni ni kazi bure, huko atakuwa anaenda kutafuta posho tu.
 
Back
Top Bottom