Askofu wa Kanisa Angliakana Dayosisi ya Mpwapwa afariki siku 6 baada ya kuwekwa wakfu

Msitari wa pambizo

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2014
Posts
3,098
Reaction score
5,451
Katika hali ya majonzi na maskitiko askofu mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania Mahimbo Mndolwa ametangaza kifo cha Askofu mpya wa kanisa Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa George Chiteto leo tarehe 3.9.2022 ikiwani nitakribani siku sita tangu askofu huyo alipowekwa wakfu wa kuwa askofu mkuu wa dayosisi hiyo.

Mauti yamemkuta akiwa mkoani Tanga ambapo alikwenda kwa ajili ya maziko ya mke wa Askofu Lugendo wa dayosisi ya Southern Highlands (mama Hilda Lugendo)

Bishop Chiteto ndio aliyehubiri ktk ibada hiyo ya maziko na dakika chache baadaye alizidiwa na kupoteza fahamu na baada ya kumpeleka hospitali alifariki dunia
 
Ndumba
 
What a beautiful ending? MUNGU nipe mwisho mwema! Pumzika kwa Amani Mama Lugendo
 
Ukijua wamebaki watu wangapi kufikia zamu yk ufe.
Nafkiri muda huu ungekuwa unasifu na kuabudu
 
Kuna mawili. Presha ya furaha ya ushindi ilimzidi ama kapigwa kipapai na aliowashinda kwenye uchaguzi.
 
Bwana Ametoa
Bwana Ametwaa
Jina Lake Lihimidiwe

Apumzike Kwa Amani, Amen
 
Yule waziri aliyeshindwa kusoma tu kiapo katunzwa wapi jamani. Binadamu hatari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…