Askofu Willybard Lagho wa Kanisa katoliki jimbo la Malindi, Kenya ametoa waraka kwa makasisi wote wanaosimamia parokia za dayosisi hiyo, akiwaagiza wasiwape nafasi za pekee wanasiasa wakati wa misa takatifu.
Kulingana na waraka huo, uliopatikana na BRK, wanasiasa wamekatazwa kuhutubia wafuasi wakati wa misa na pia hawapaswi kupewa viti vya pekee au vilivyohifadhiwa.
"Waumini wote, wakiwemo wanasiasa, wanapaswa kutendewa kwa usawa, na hakuna anayestahili kupata viti vya pekee au mipango ya kuketi tofauti. Mtu anayearifu uongozi wa kanisa kuhusu mpango wake wa kuhudhuria misa siku na nyakati maalum bila shaka ni mtu anayetafuta nafasi ya pekee," waraka huo wenye maneno makali unasema.
Aidha, askofu anawaonya makasisi wowote wa majimbo hayo ambao watashindwa kufuata agizo hili kwamba watawajibishwa