Askofu Wolfgang Pisa: Padri Charles Kitima atarejea katika majukumu yake hivi karibuni

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Wolfgang Pisa amesema hali ya kiafya Padri Charles Kitima, katibu mkuu wa Baraza hilo, inaendelea vyema na atarejea katika majukumu yake hivi karibuni.

Padri Kitima alishambuliwa Aprili 30, 2025 na kitu butu kichwani alipokuwa kwenye ofisi za TEC Kurasini Temeke jijini Dar es Salaam na kulazwa katika Hospitali ya Aga Khan.

Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ilieleza kuwashikilia watu wawili wakishukiwa kuhusika na tukio hilo na kuwa watafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.

Soma Pia: Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Mwananchi limemtafuta leo Jumapili Mei 25, 2025, Kamanda wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro kujua upelelezi wa tukio hilo ulipofikia, lakini hakupatikana kwani simu yake ilikuwa ikiita bila kupokea na hata ujumbe mfupi aliotumiwa haukupata majibu.

Akizungumza leo kwenye misa ya kuwekwa wakfu kwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, Josephat Jackson Bududu, Rais huyo wa TEC amezungumzia afya ya Padri Kitima na matumaini yaliyopo.
Muliro kaingiziwa Mil ngapi masna IGP amekula 1Bil anyamaze na njaa zake....kanunua hisa damu za watanganyika zimwagike....kusa Mama Abdul afanye atakavyooo
 
Nasikia huko, jitu limepotoko huko nje, mijitu imejikulia yenyewe yenyewe tuu, yaan ni tafrani tupu
 
Wasishiriki vipi wakati mgombea Mwenza ni Mkatoliki kindakindaki. Au atajiuzulu?
mgombea mweza aje kwanza na majibu ya kitu butu alichopigiwa kichwani katibu wa maaskofu dr kitima padri
 
Kamanda wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro kujua upelelezi wa tukio hilo ulipofikia, lakini hakupatikana kwani simu yake ilikuwa ikiita bila kupokea na hata ujumbe mfupi aliotumiwa haukupata majibu.
Hawezi kujibu kitu
 
Mungu ni Mwema! Shetani alitaka kuizima sauti ya mtetezi wa Wanyonge lakini ameshindwa.
 
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Wolfgang Pisa amesema hali ya kiafya Padri Charles Kitima, katibu mkuu wa Baraza hilo, inaendelea vyema na atarejea katika majukumu yake hivi karibuni.

Padri Kitima alishambuliwa Aprili 30, 2025 na kitu butu kichwani alipokuwa kwenye ofisi za TEC Kurasini Temeke jijini Dar es Salaam na kulazwa katika Hospitali ya Aga Khan.

Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ilieleza kuwashikilia watu wawili wakishukiwa kuhusika na tukio hilo na kuwa watafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.

Soma Pia: Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Mwananchi limemtafuta leo Jumapili Mei 25, 2025, Kamanda wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro kujua upelelezi wa tukio hilo ulipofikia, lakini hakupatikana kwani simu yake ilikuwa ikiita bila kupokea na hata ujumbe mfupi aliotumiwa haukupata majibu.

Akizungumza leo kwenye misa ya kuwekwa wakfu kwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, Josephat Jackson Bududu, Rais huyo wa TEC amezungumzia afya ya Padri Kitima na matumaini yaliyopo.
Hawezi kujipeleleza milo muhuni
 
Back
Top Bottom