ASLAY awe makini na hii COMBINATION kati yake na NANDY

srinavas

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2011
Posts
4,195
Reaction score
4,013
Habari za ijumaa wakuu

Moja kwa moja niende kwenye mada kama kichwa kinavyojieleza hapo juu

Kumekuwa na promo nyingi sana kumhusu aslay na nandy , kutoa nyimbo mbalimbali pamoja, kufanya shoo pamoja, kuingia mikataba mbalimbali pamoja ikiwemo mikataba ya kuitangaza tatu mzuka. Lakini pia kurudia baadhi ya nyimbo za askay pamoja.

Sasa jamani mimi naona hiki kitu ni kizuri ila hakitafika mbali na kitamuacha aslay pabaya. Watu wengi wanaompenda aslay na kumsapoti kwenye ngoma zake alizokuwa anazifululiza mwanzo nadhani kwa sasa wanasita kumsapoti kwa hii kiki mpya anayopewa na hawa CLOUDS ambao wote mnawatambua vizuri sina haja ya kuelezea hapa.

Jamani mimi nachoona ni kwamba siku si nyingi aslay atafyonzwa kama mua na hatakuwa na utamu tena na watantupilia mbali.

Ushauri wangu kwa kijana aslay ni aendelee na ule utaratibu wake wa mwanzo na aachane kabisa na hawa watu wa sasa

Ni hayo tu nawasilisha
 
Lengo lao wanasema wanataka awe wa Kimataifa haliyakuwa Wasanii wao wa THT pamoja na kuwa na Vipaji wamewatumia kwa Manufaa yao na bila aibu wamewatelekeza!!!
Kweli kabisa. Mimi ningekuwa nna mawasiliano ya dogo ningempigia kwa kweli
 
Hivi Ali Kiba yuko wapi siku hizi?
 
si rahisi kumuacha ruge
ngoja kwanza wa m rugelize
 
Okey ni kweli ila muhimu kujiandaa
Clouds hawajawahi kumuacha aslay
Kweli kabisa. Mimi ningekuwa nna mawasiliano ya dogo ningempigia kwa kweli
clouds haw ajawahi kumuacha aslay, hata ya moto ilipovunjika aslay ameendelea kupewa promo na clouds kuliko wenzake kuanzia interviews kwenye leo tena mpaka xxl.
Bado wampeleka kwenye jiwe la mwezi mara mbili.
Ni maneno ya watu tu kudai promo kaanza pewa sasa.
Si waona collabo yake na nandy imempa mkataba mnene au hayo siyo mafanikio?
 
Unachosema si kweli, Aslay baada ya kutoka Yamoto na kuanza kutoa ngoma zake karibu nyimbo zake nyingi amezindulia mtandaoni UTube/Insta, na ngoma zake hazikuwa zinapata airtime kivile si Clouds tu bali hata Redio/TV nyingine, sema kwakuwa alikuwa na ngoma kali na mitaani watu wanazielewa zinapigwa kila mahali na U-Tube zinagonga views za kutosha Clouds wakaona Impact ya dogo ndio na wenyewe wakamdaka na kumfanya 'wao', yaani tena baada ya Fiesta naona ndio wakaamua wamuweke karibu zaidi na msanii wao wa THT Nandy ili watengeneze combination ili wampige vizuri. Sema hakuna namna ya kumkwepa Ruge kwa msanii mchanga wa bongo kama Aslay, ni kufanya naye tu kazi walau uvidake hivyo vilaki 5 kuliko kukosa kabisa, awe na akili tu hizo hela kidogo anazopata a invest maana ya baada ya miaka miwili Ruge hatakuwa na time naye tena atamtafuta 'Aslay' mpya, na Nandy naye awe makini asije kuishia kuwa kama kina Recho na Rubby
 
Wamezunguka naye kwenye jiwe la mwezi mara mbili kabla hata ya fiesta... alifanyiwa interview kwenye kipindi cha leo tena alipotoa ngoma angekuona...
Kati ya wote aslay ndiye anapewa support zaidi hata beka flavour hajapata support kama ya aslay
 
Kweli kabisa mkuu. Hivi vipi saida karoli nae siku hizi?
 
Naunga mkono hoja yako umewaza mbali sana ...aslay kipaji chake kinatosha kabisa kujitangaza na hasa kujiwekes msingi mzuri nyumbani (hapa tz) mengine ni suala la mda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…