Habari za mchana wana Jf , mm binafsi ni shabiki mkubwa wa nyimbo za dogo aslay ukweli ni kwamba dogo anajitahidi . Ila kilonifanya niandike hii thread kuna wimbo wa aslay umetoka sijui kautoa mwenyewe au umevuja au VP maana wimbo wenyewe una verse moja tu lkn mashairi ya wimbo huo hayajawafurahisha wanawake wengi ikiwemo Mimi .
Ni wimbo ambao unamdhalilisha mwanamke huyu do go anapaswa atambue kwamba mashabiki wa mziki wake wengi ni wanawake .hata kama umeachana na mwanamke huwez kumtolea matusi kama ya kwenye wimbo wa aslay . so aslay kama umo humu Jf acha kudhalilisha wanawake ambao ndo mashabiki zako wakubwa including Ray 4 real.
Baadhi ya mashairi katika huo wimbo;[emoji116]
Kiuno kizito kama engine ya fuso ,
Hauna lolote kitandani yaani upopo,
Unashindwa hata kufua vichupi vyako,
Unanuka jasho makwapani kama choo cha soko..
Hayo ni baadhi ya mashairi kwa kweli hayajatufurahisha wanawake na ni udhalilishaji
So aslay if u are also in Jf na ukasoma hii thread ujue umetudsappoint 90% ya wanawake Tz. Yangu ni hayo sema nimeshindwa kuapload hiyo audio.