Aslay na Nandy wapigwa faini ya TZS 5M kwa wizi wa wimbo 'Subalkheri Mpenzi'

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Wasanii Aslay na Nandy wamepigwa faini ya milioni 5 kwa pamoja kutokana na kukiri, kukubali kosa kuimba wimbo wa 'Subalkheri Mpenzi' bila kufanya mawasiliano na wamiliki wa wimbo huo ambao ni kikundi cha Utamaduni cha taarab asilia visiwani Zanzibar.

Kikundi hicho kilikusudia kuwafikisha mahakamani wasanii hao lakini kabla ya kuchukua hatu hiyo Aslay na Nandy wakiwakilishwa na kiongozi wao walifika visiwani humo na kufanya mazungumzo na kikundi hicho ambapo wamehitaji kulipwa milioni tano.

Katibu Mkuu wa kikundi cha utamaduni cha tarabu asilia, Taimur Rukuni Twaha, amesema kikundi hicho cha tarab kimewataka wasanii hao kulipa faini kutokana na kuimba wimbo huo bila ya ridhaa yao, pia amedai kuwa wamekubaliana leo Alhamisi na kufikia muafaka huo baada ya wasanii hao kupitia kwa kiongozi wao kukiri kufanya kosa hilo.

Twaha amesema licha ya kukiri makosa hayo pia meneja huyo wa Aslay ameomba kuingia mkataba na kikundi hicho cha tarab kufanya biashara ya kuziimba tena nyimbo zao zengine za zamani.

Katibu huyo amesema kuhusu nyimbo zao kuimbwa tena hilo bado hawajaafikiana kwa sababu walishapewa agizo na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Dk Salmin Amour Juma wakati akiwa rais, kuwa wasikubali nyimbo zao za tarabu asilia kuzibadili na kuzifanya katika mfumo wa muziki wa kisasa.
----
Mapema mwezi Februari zilikuja taarifa kwamba wasanii hao watashtakiwa kwa kosa la kuiba wimbo. Zaidi soma => Aslay na Nandy kupelekwa Mahakamani

Kusikiliza nyimbo hizo fuata hizi links...


 
Wimbo huo ulimgusa sana Hallat Samia Suluhu mpaka akawaalika Chai Nyumbani kwake kumbe umekwapuliwa sehemu, Kweli Bongo ni Juma Nyoso
 
Alie weka nyimbo zote hapa pamoja kafanya jambo bora sana. Ukiisikiliza unasikia hao wahenga sauti zinatoka uzuri tu na hawa damu changa sauti kama wanalazimishwa achilia mbali mikwaruzo kwa vijana. Pia uzingatiaji wa kutamka maneno katika lafudhi yake bado ni changamoto kwa vijana wetu.
 
Waliyourudia wameuharibu sana... Manjonjo yamezidi mpaka nyimbo imekua mbaya...


Original yake ni mzuri zaidi...


Cc: mahondaw
 
aslay kaishiwa tayari akachunge mbuzi tu mziki wake unaishia hivyo...keep this post
 
Bado hiyo million 5 ni kama punje ya mchicha kwenye embe dodo.Kupitia huu wimbo Aslay na Nandy wamepiga hela ndefu sana.Binafsi ningekua nawawakilisha hao wazee ningewaambia wawape bure tu wao wapate royalties hata asilimia hamsini tu.Walichokifanya ni kama wameshapewa chao na huo wimbo sasa ni mali ya Aslay na Nandy malipo yoyote kupitia wimbo huo hayatawahusu otherwise kuwe na terms na conditions ambazo hatuzijui
 
Wasanii wa Tanzania wanashangaza sana...wakiibiwa kazi zao wanalalamika kweli ila wanaibiana wao kwa wao
 
fundisho ilikua wimbo usipigwe popote pale. Watu waliumiza vichwa kipindi hiko leo vijana wanaleta mambo ya kitonga.
 
Niliandika huu uzi ukafutwa hapa, nilisema kwamba wajiandae kushtakiwa.. [emoji111]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…