Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Tumaini Mabula miaka 9 iliyopita alifika rafiki yake Justine Peter nyumbani kwake akiwa na mpenzi, rafiki yake alimuomba chumba chake alichopanga Mwananyamala akiwa na rafiki yake wa kike kwasababu yeye alikuwa anakaa kwa shemeji anayeishi na dada yake.
Tumaini alimpa maelekezo wakimaliza aache funguo kwa Mangi dukani lakini aliporudi mangi alikana kupewa funguo. Alipofika chumbani alikuta mwanamke(shemeji yake kwa Justine) akiwa amelala na macho yasiyofumba. Mwanzo alidhani ameamua 'kujirudisha' lakini alipofikika mwenyekiti wa mtaa akamwambia mwanamke husika amefariki.
Walipofika Polisi walimbeba Tumaini na safari yake ya kusota ikaanza rasmi, polisi walichukua alama za vidole zilizokuwa kwenye mwili wa marehemu zikiwemo za Justine na Tumaini alizoacha wakati anamuamsha. Justine alikimbia na walipofika kwa shemeji alipokuwa anaishi wakakuta nyumba nzima wameshahama na kuhamisha vitu usiku mmoja kabla yake.
Justine aliamua kwenda kuishi mpakani akiukimbia mji na kuogopa kukamatwa akiuza samaki wa Tanzania nchini Burundi. Siku moja alikumbana na askari wa uhamiaji na alipoulizwa ni raia wa nchi gani alisema Burundi lakini lafudhi nzuri ya Kiswahili chake iliwapa hofu maafisa uhamiaji wakaamua kuscan vidole vyake.
Alama zake za vidole zilijitokeza kuwa alikuwa anatafutwa kwa kesi ya mauaji, alama zilizochukuliwa wakati wa uchunguzi wa mwili wa marehemu.
Mwanzo Justine alijitetea kwamba hakujua marehemu alifariki na alimpiga bahati mbaya kisogoni baada ya mchumba wake kupigiwa simu mfululizo bila kupokea na baadae kutumiwa SMS mhusika akimlalamikia kutofika kwake wakati ameegesha mlango wazi akimsubiri yeye.
Changamoto aliyoipata Justine ni kukimbilia mpakani pamoja dada na shemeji yake kuhama usiku wa manane kama alijua hakufanya kitu.
Kwa hisani ya Millard