Kuna msomali flani, aliniambia kuna kijiji flani mpakani mwa Somalia na Ethiopia, alshabaab walipitia hicho kijiji wakiingia Ethiopia, hicho kijiji kilikosa ku repot kwa serekali ya Ethiopia, baada ya siku kadhaa,Jeshi la Ethiopia lilifika hapo na kijiji chote kiliuliwa na nyumba na ngome,mbuzi kuchomwa, sababu eti "wasaliti", Akasema hii ndo maana wanavijiji walio mpakani mwa Ethiopia wako raadhi wapigane na Alshabaab wenyewe kuliko kuwaacha wapite manake wanaogopa Serekali ya Ethiopia kuliko Alshabaab...
Huyo msomali alipo nipigia hio story nilimuangalia tu, sikumuamini , nikamwambia kama jeshi la Ethiopia lingekua linafanya hivyo kwa wananchi wake hapo mpakani ingekua tuliskia kwa vyombo vya habari... Lakini kwa upande mwengine, hua hausikii habari zozote za Alshabaab huko Ethiopia... Kuna kauwezekano sababu ni hio ya hakuna uhuru wa vyombo vya wanahabari.