Mkuu
brazaj, naomba kuanza na a point of correction, mimi sio mwanasheria nguli, ni mwanahabari nguli.
Issue ya IGA ya DPW na Bandari zetu ina pande 4,
1. Kiuhalisia
2. Kisheria
3. Kisiasa
4. Kiuchumi,
hivyo mtu yoyote yuko huru kutoa maoni yake yoyote kuhusu jambo lolote hata kama sio mtu wa fani husika, ndio maana tumeshuhudia, Prof. Shivji akitoa maoni yake ya kisheria, yakabezwa na shehe ubwabwa!.
Alichokisema Prof Assad ni ukweli, tuna tatizo kubwa la uelewa toka kule juu mpaka chini. Tuna wanasheria na viongozi wazuri toka juu mpaka chini, ila pia na wanasheria na viongozi vilaza wa ajabu toka juu mpaka chini!, vilaza hawa wametamalaki ndani ya serikali yetu, Bunge letu, hadi kwenye Mahakama zetu!.
Issue ya IGA ilihitaji tuu elimu kwa umma, wananchi kuelimishwa IGA ni nini na HGA ni nini, ila pia
Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
P.