Assad alipolikoroga tuyakumbuke ya Lwaitama

Kumbe huyo mzee alishawahi kutumika kwenye hiyo mihadhara ya kidini? basi wanaohusisha imani kujibu kile alichozungumza wako sahihi.
 
ndio alimpinga kwasababu ni mkristo hakuna jingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama iliyotoa hukumu huko Mbeya ipo Tanganyika huku huku tulipo. Hizo haki za Tanganyika ni zipi?.

Na naiona hoja ya utanganyika ikienda kupotea kwa miaka mingi mpaka atakapokuja rais mwingine kutoka Unguja au Pemba.
 
ndio alimpinga kwasababu ni mkristo hakuna jingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunasahau kuwa Prof Assad aliondolewa na JPM kutoka katika cheo chake cha CAG na watu wakapiga kelele wakisema katiba imekiukwa, kwa sababu aliamua kuutetea weledi kazini.

Namuona Profesa akiwa anasimamia elimu na maarifa kwenye utendaji kuliko kuwa sehemu ya magenge ya wanaopenda kujikomba kwa wenye vyeo.
 

Mkataba na DP world ni hoja ya kisheria. Prof Assad awe na nini cha kisheria zaidi ya akina Shivji, Nshala, Slaa, LIssu na wa namna hiyo?

Zingatia wengine hapo ni Havard Laureates.

Labda tumwombe ndugu Paskali mwanasheria nguli atupe mwongozo.

Paskali Kwa heshima na taadhima tafadhali.
 
Kumbuka kuwa CAG ana uelewa mpana sana wa uchumi haswa uwekezaji ambao unafanyika pale TPA.

Kapiga ikulu ndio sababu ya chuki yote anayokutana nayo mitandaoni.
 
Kumbuka kuwa CAG ana uelewa mpana sana wa uchumi haswa uwekezaji ambao unafanyika pale TPA.

Kapiga ikulu ndio sababu ya chuki yote anayokutana nayo mitandaoni.

Suala la DP world ni suala la kisheria. Kulikoni kutowatambua Havard Laureates kwenye maeneo yao ya kujidai?

Hujiulizi huyu mwamba kutokomea kusikojulikana?



Kwamba Lipumba, Ndakichako, Mkenda, Janabi au wa aina ya Maji Marefu (rip) kujitosa kwenye ya taaluma za wengine si ni kutaka kutuchosha bure tu?

Ya uchumi Assad tutamsikiliza, siyo ya afya ya moyo.

U professor siyo wa kila kitu mjomba.
 
Mkuu brazaj, naomba kuanza na a point of correction, mimi sio mwanasheria nguli, ni mwanahabari nguli.

Issue ya IGA ya DPW na Bandari zetu ina pande 4,
1. Kiuhalisia
2. Kisheria
3. Kisiasa
4. Kiuchumi,
hivyo mtu yoyote yuko huru kutoa maoni yake yoyote kuhusu jambo lolote hata kama sio mtu wa fani husika, ndio maana tumeshuhudia, Prof. Shivji akitoa maoni yake ya kisheria, yakabezwa na shehe ubwabwa!.

Alichokisema Prof Assad ni ukweli, tuna tatizo kubwa la uelewa toka kule juu mpaka chini. Tuna wanasheria na viongozi wazuri toka juu mpaka chini, ila pia na wanasheria na viongozi vilaza wa ajabu toka juu mpaka chini!, vilaza hawa wametamalaki ndani ya serikali yetu, Bunge letu, hadi kwenye Mahakama zetu!.

Issue ya IGA ilihitaji tuu elimu kwa umma, wananchi kuelimishwa IGA ni nini na HGA ni nini, ila pia Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
P.
 
Hii mada yako hii inatatiza sana.
Uozo mwingi ndani ya siasa unaoonekana sasa hivi kote nchini unasimamia kwenye dhana hii potofu kabisa.

Hata hivyo, kuna ninachokubaliana nacho kwenye mada yako. Laiti kama ungejikita huku kwenye "Kukubaliana kwenye agenda za kudumu", mada yako ingeeleweka vizuri sana.
 

Kwamba ni kwa maneno yako kuwa wewe si nguli wa sheria bali habari? Huo ni uthubitisho kuwa tujikite kuhabarishana ya kina Mayele Mayele kwenye ngao za hisani uwanjani mkwakwani huko.

Ya magonjwa ya moyo tuwaachie kina Janabi. Sheria kina Shivji, Assad uchumi, Ndalichako Elimu, Maji marefu miti shamba, Mwandosya Umeme, Mruma Madini, Einstein nuclear, Dr. Msukuma matango pori:



Tuheshimu taaluma za watu.

Nakazia suala la DP World kinachogomba ni mambo ya kisheria. Kama huko hatuna weledi - tuufyate zaidi sana ni kujiroga kwa mayala ya matumbo yetu tu!
 

Kutatizika na mada ya mtu ni jambo la kawaida wala hakuna geni hapo. Kimsingi ieleweke niliandika kuwatatiza wasio mwelewa Prof. Lwaitama.

Usitatizike vipi ndugu kama humwelewi Prof. Nguli huyu wa mambo ya siasa?

Zingitia mada nzima Ina sentensi 9. Kila moja ikiwa imekamilika kwa maana yake kamili.

Wasikwazike vipi mamburula wenye kutaka tuandike wanayotaka wao kuyasikia?

Ukitaka kusikia ya kupendeza masikioni mwako si uambatane na kina Simba huko?

"Ama kwa hakika 'Iyena Iyena' ikakutatize vipi?"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…