Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 25,968
- 36,044
Miongoni mwa maamuzi ya hovyo zaidi kuwahi kuyaona basi hili la Assemahle Wellem kutoka South Africa kutoka huko kwao kuja Tanzania kupigana kwa bendera ya Tanzania chini ya Mafia boxing.
Jamaa kabla hajaja Mafia boxing alikuwa Predator kweli kweli , anatembeza kichapo balaa mpaka almanusura amstaafishe ngumi Selemani Kidunda maana alimtandika kisawa sawa mpaka jeshi likaona Kidunda akae pembeni kidogo apumzike asije akdharirisha jeshi bure.
Mbali na Kidunda , alimchakaza vilivyo pia Twaha Kiduku.
Aina yake ya upiganaji na ring IQ aliyokuwa nayo ilikuwa ngumu sana kwa mabondia wa TZ kutaka kupigana naye maana alikuwa moto wa kuotea mbali.
Ila sasa baada ya kuja Tanzania na kujiunga na Mafia boxing jamaa kawa bondia wa hovyo sana.
Ngumi zake hazivutii, mapambano mengi hata kama anashinda , kiwango anachokionesha huwa hakiridhishi kabisa.
Na idadi ya losses imeongeza sana kiasi kwamba hata ikitangazwa jamaa anapigana ule mvuto aliokuwa nao mwanzoni wa kumtazama haupo kabisa.
Mliokaribu naye mkateni sikio azinduke na aondoke hapo Mafia haraka iwezekanavyo kabla mambo hayajawa mabaya zaidi kwake.