Assembly & Manufacturing Business

Chu China

Member
Joined
Mar 9, 2023
Posts
9
Reaction score
8
Nawa salimu kwa jina la M/Mungu.

Niko na wazo la muda mrefu, nataka nianze Biashara ya uunganishaji (Assembly Business) kwa Bidhaa mbalimbali.

Changamoto yangu Ni:

1. Nitumie njia gani ili niweze kuagiza parts (vipuli) za Bidhaa hizo ninazo taka kuanza kuzifanyia assembly.. Sababu parts zote hazipatikani nchini Kwetu Ila nitatakiwa kuagiza kwenye nchi kama China & India.

2. Sijawahi fanya Biashara ya Bidhaa hizo kabla, hivo Sina uzoefu zaidi ya utafiti nilio na ninao Endelea kuufanya. Sasa je ni bora niende moja kwa moja kwende assembly au nianze kwanza kuuza finished goods zilizopo ili nipate uzoefu wa mauzo kivitendo?

3. Nianze kutafuta order (wanunuzi) kwanza.. nimelenga wale wauzaji wa Maduka ya Jumla, Maduka ya Reja reja, makampuni husika na taasisi au niingize Machine na Vipuli kwanza then nitapokuwa nmeanza uzalishaji ndio nitafute soko? (Japo kwa ujumla naona Bidhaa ninazo taka kuanza kuzizalisha mwenyewe hapa nchini Kupitia kuagiza vipuli vyake nje.. Naona fursa ya soko ipo).

NB: Future yangu nataka sana nije nimiliki factory ya Kufanya Manufacturing & Assembly ya products mbalimbali.

Karibu kwa mawazo.
 
Ulicho nacho hadi sasa ni idea tena ni kama hujafanyia ufuatiliaji kidogo. Unahitaji muda kufanya utafiti kuweka sawa wazo lako, usome na ujue kuhusu manufacturing. Hapo ndio utaanza kulipanga upya wazo lako na kuondoa makosa. Sanasana huwa ni vigumu kuomba ushauri wa kitu usichojua, kila unaloambiwa unabeba labda utake kuiga kila kitu.

Uanze na segment moja kama zana za kilimo, vifaa vya ofisini, bidhaa za ngozi au kingine ila kimoja kwanza. Huwezi anza mara hiyohiyo ukawa na vitu vingi. Kwanza inabidi uwe na ardhi hekali ngapi za kuweka factory ama assembly plant.

Wateja si lazima uwe nao sasa utawapataje na hizo bidhaa huna, unless uanze ukiwa agent wa manufacturer uwe unachukua bidhaa kiwandani kwa MOQ kubwa upate wateja mbalimbali kisha ushawishi kiwanda muingie ubia kufungua factory au utafute wawekezaji muanze maana wateja wapo. Otherwise kuna bidhaa hazina ulazima uwe na wateja kabla kama kuna demand kubwa na una marketing strategies nzuri kama price, quality, etc.

Swali la kwanza linajibika ila sina jibu.

Swali la pili wengine huenda kuishi China akikaa miaka minne hivi akiwa wakala anakuwa trusted na manufacturers mpaka anakopeshwa mzigo arudishe hela baadae. Experience ni muhimu kuliko maelezo, vigumu sana kushawishi mtu katafuta hela yake kwa jasho eti awekeze kwenye kitu hujui ukajifunzie mtaji wake.

Swali la tatu naona unataja vipuri, vya nini magari au? Manufacturing rahisi kibongobongo ni food production. Au agiza bidhaa zikiwa na label yako kisha baadae ukishapata wateja anza production. Kwani Mo Electro zinatengenezwa wapi, so usishangae Mo akaanza kuzitengeneza nchini miaka ijayo. Au fatilia kuhusu HC sanitary pads
 
Mkuu biashara yoyote ili uweze kuimudu na kuiendesha vizuri lazima uanzie chini kulisoma soko na wateja wako kisha inakuwa polepole hadi kuwa kubwa.

Sasa wewe unasema hujawahi kabisa kufanya biashara halafu unaongelea biashara ya mabilioni ya pesa.
Unapoongelea assembly plant unaongelea mabilioni ya pesa japokuwa hujaweka wazi ni assembly plant ya vitu gani,kama ni assembly plant ya magari sio jambo dogo ni kitu ambacho hata serikali yetu inachemka kuwekeza kwenye hizo projects.

Fikiria hata assembly ya bodaboda tu ni Mo dewji peke yake ndio anafanya assembly na kusambaza nchi nzima sina hakika kama kuna mwingine.

Kwa hiyo unapohitaji kuwa mfanyabiashara serious kuwa makini sana kwenye kuchagua wazo la biashara.
 
Ahsnte sana Mkuu. Umenifungua vya kutosha.

Bado Naendelea kujifunza na kukamilisha uchunguzi katika hili.

NB:- Hizi product ninazo zifanyia uchunguzi ili kuanza kuzifanyia assembly.. kwa mujibu ya utafiti wangu, nilichogundua na kuona baadhi ya wanaofanya huko nje ( China & India ) sio lazima nipate ekali or jumba kuuubwa hapana.. Hata nikiwa ndani ya chumba Chenye 100 m² au Chini ya hapo bado assembly itafanyika Vizuri tu. PIA by Training na uendeshaji Wala haihitaji skilled workers kwa sana.

Cha Msingi ni Mimi Nipate hivo vitendea Kazi vikiwemo:

1. Assembly Machine ya Bidhaa husika
- hii Mashine Inapatikana India.. na Zina Kuwa Set Tano, na Tayari nimeshawasiliana na Manufacturers wa hizo mashine zaidi ya wawili.. CHANGAMOTO hapa Ni NAMNA GANI ITANIFIKIA hapa Tz. (that's y pale juu niliuliza Kuwa nawezaje Kusafirisha Mashine Kutoka INDIA TO TZ) sababu Kampuni Nyingi hapa D'salaam za Usafirishaji Ni China, Turkish, UK.. India Sijabahatika kuipata.


2. Raw materials (parts for assembly) - Kuhusu Raw materials za Kuanzia Tayari nimejihakiki wapi pa kuzipata ( Kupitia hao hao manufacturer wa machine.. Nitapokuwa nimefanikiwa kupata namna ya kuifikisha Mashine tz Basi Raw materials nazo zitakuja pamoja na mashine hiyo. (They will supply me.)

NB:- Hapa kwenye Raw materials lengo ni kuanza kwanza kwa kuagiza parts zote Kutoka nje.. then later niangalie katika hizo parts zipi nazimudu kuziunda mwenyewe hapa hapa nchini.
 
Ahsnte Mkuu, mawazo yako nayazingatia vya kutosha..

NB:- Assembly hii ninayotaka chunguza kuianza sio ya kuzalisha big machine Kama Magari n. k, Hapana.. Ila Nataka Kufanya assembly ya bidhaa ambayo karibia kila mtu nchi hii na dunia at alarge wanaitumia.. hasa hasa taasisi za serikali na binafsi pia.. mlengo wangu ni walau kujihakikia soko kwa 60%+.
Ambapo kwa hapa Kwetu Bidhaa hii at large Kama sio at all zinaingizwa kutoka India kwa sana.

"Kuna njia mbili.. moja inapita kushoto, Nyingine inapita kulia.. hii inayopita kulia imejaa watu wengi saaana ( sababu ya comfort , u short cutt n.k).. wakati hii inayopita kushoto inawatu wachache ( No comfort, it's too long, changamoto Nyingi.. Ila Ushindani kidogo)).. hivo nikipita njia hii afu nikafanya kwa ku-make different natumai nitapata Faraja huko mbeleni..

#M/mungu anifanyie wepesi kuyatekeleza haya. AMEENA.
 
Kumbe wewe changamoto yako ni kusafirisha tu hizo mashine?hiyo ishu ndogo sana.
Nakupa akili moja,mimi niko Dubai nitakusimamia kuipokea hapa dubai kutokea India maana Dubai na India ni kama pua na mdomo,kisha ikishafika hapa Dubai tunaipandisha meli hadi Tanzania.
 
Una material sanaa 😀
 
Labda unataka manufacturing ya vifaa vya stationary. Na uzingatie tofauti ya assembly na manufacturing. Assembly unaunganisha vifaa na manufacturing unazalisha, it's easier to start assembly line then baadae uifanye iwe manufacturing plant.

Na kwa comment yako nyingine umesema unataka ufanye local. Viwanda vidogo vya China vingi viko hivyo na viko characterized na mazingira magumu, malipo kidogo, usafi na safety ndogo na efficiency ya kawaida. Tunaviita "sweatshops" mtu anaweza geuza nyumba iwe kiwanda. Probably utaanza hivi wala haishangazi
 
Ahsnte.. nadhani umenielewa sasa. [emoji1666]
 
"..it's easier to start assembly line then baadae uifanye iwe manufacturing plant."

YES hichi ndio kitu ambacho nataka nikifanye. [emoji1666]
 
Wazo zuri sana..Huu mpango kazi umepanga kuanzisha mkoa gani Mkuu vijana bado ajira ni changamoto...Tupatie lacation mapema tujipange kuomba ujira as volunteers hadi hapo mipango inapokua imekaa sawa sawa...
 
Nenda kwa shipping agent kama MSC Maersky watakupa utaratibu wa namna ya kuagiza machine zako na gharama yake.

Or

Ingia kwa website zao hao shoppers unaweza kupata mwanga. Na kama ni full container unaweza kufanya booking mwenyewe

Or

Huko india unapoagiza machine zako waambie wakupakilie kwenye meli kabisa,wakupe price ya FOB au CIF dar es salaam.
 

Unataka kufanya assembly ya kitu gani ili usaidiwe mawazo
Kwanza eneo ukubwa waeneo utakusaidia
Suppliers inabd uwe na supplier ambao wanakuingizia vifaa
Vibali vya kuingiza na kusajili pia eneo kma manufacture hyo ni baadhi
 
Anza kuingiza ma pikipiki ya kichina then uje uanze agiza vifaa vyake utanishukuru baadae WACHINA NA WA INDI wamepigia sana hela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…