Aston Villa special thread (Blue army)

Wakifungwa sana hata umuhumu wa Samatta utashuka.

Mpira tambo lake ni ushindi.

Timu unayofungwa 10-1 haiwezi kutamba kwamba imefungwa magoli 10 lakini ina goli moja ka Samatta.

Be sensibke please.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nakubaliana na wewe!

Ila mkuu kufungwa 10 haifanyi mchango wako usionekane, utaonekana tu. Sasa kama mtu unafunga upande wa ulinzi unafanya vituko kwanini usionekane mchango wako!

Kifupi samata afunge awezavyo, aoneshe kiwango kizuri hata villa ikishuka daraja iwe rahisi kupata timu!
 
Hii ni defeatist attitude.

Kama kuna uwezekano wowote wa kutoshuka daraja, hiyo ndiyo iwe focus. Si "hata Villa ikishuka daraja...".

Villa ikishuka daraja, rekodi hiyo itakaa na Samatta daima. Kwamba alishindwa kuinusuru Villa kushuka daraja. Hiyo si rekodi nzuri.

Samatta kaletwa Villa kwa malengo.

Moja ya malengo haya ni kuinusuru Villa isishuke daraja.

Prince William ni mshabiki wa Villa, kawaambia msiniangushe. Msishuke daraja. Sitaki timu yangu ishuke daraja.

Washqbiki kibao wa Villa hawataki ishuke daraja.

Sasa hapo Samatta kazi yake kuhakikisha wanashinda na Villa haishuki daraja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Watashinda kwa samata kufunga tu vipi kuzuia! Haya samata ndio ameshafunga, villa wana matatizo kocha anashindwa kubadilika yule grealish si mzuri akitokea pembeni, ingependeza kama angempa jukumu la free role acheze chini ya mshambuliaji ama washambuliaji!

Hata villa ikishuka! Maana yake hilo ndio chaguo la mwisho kabisa! Hamna hamna! Nakubali villa wana malengo yao ila haimaanishi lazima wafikie! Wamemchukua samatta aongeze idadi ya magoli na kafanya hivyo!

Samata kufunga anatimiza wajibu wake ndani ya villa lakini pia anajitengenezea mazingira mazuri binafsi yake.
 
Samatta anaweza kuinusuru Villa isishuke daraja au hawezi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Villa ni timu natumai unaelewa maana ya timu, kushuka ni kutegemea na jitihada za kuanzia kwa kipa mpaka 11, na mipango kabambe ya benchi la ufundi huko, kwa mchezo ule anaweza asiwanusuru.
Hujajibu swali nililouliza, na ulilojibu sijauliza.

Timu inajengwa na watu, haijengwi na matofali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuliwaonya humu acheni kupeleka siasa za Simba na Yanga kwenye ligi ngumu ya EPL mkatuona sisi ni mabeberu weusi ...


Naona mmeanza kuisoma namba. Aston Villa ni team ya hovyo saaaaaaana , Haina kiwango hata Cha kuifikia Genk. Na Kwasisi wapenzi wa EPL tulionya kuwa samata atapata wakati mgumu kwenye Hilo litimu maana tunalijua Linavyohangaika kiuchezaji...


Ni Mara 100 Popa angeenda zake Sheffield United, AFC Bournemouth hata Newcastle. Hizi ni team zenye Temple ya Kumshambulia haswa. Na strikers wao wanatengenezewa nafasi za kumwaga.


Hata Jana ukiwaangalia Bournemouth striker wao WILSON hakuwa tu makini ila aliwekewa mapande ya maana kuanzia Cross za maana na penetration zilizokwenda shule ...

AstonVila iko disorganized sana. Top scorer wao ni Grealish ambae ana magoli 6. Kila anapopata mpira anataka kutunga yeye na ukiangalia team ni Kama imejengwa kumtuata yeye.


Namuombea sana samata afanye vyema yeye binafsi ila sioni team Yake ikifanya vizuri


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujajibu swali nililouliza, na ulilojibu sijauliza.

Timu inajengwa na watu, haijengwi na matofali.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nimekujib vizuri swali lako, ila jibu hulioni sababu sijajibu jibu ulilotaka wewe.

Kwani mie nimesema timu inajengwa na nani!![emoji13][emoji13]🤣🤣[emoji23][emoji23]
 
Nimekujib vizuri swali lako, ila jibu hulioni sababu sijajibu jibu ulilotaka wewe.

Kwani mie nimesema timu inajengwa na nani!![emoji13][emoji13][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23]
Umeongelea timu kama dubwana moja hivi kubwa halivunjiki into individual players.

Umekataa kujibu swali langu la kumhusu Samatta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongelea timu kama dubwana moja hivi kubwa halivunjiki into individual players.

Umekataa kujibu swali langu la kumhusu Samatta.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nimekujibu, tatizo wewe ukiwa unasoma ukifika kwenye jibu langu unafunba macho mzee.

Yawezekana tunaongelea kitu kimoja, ila tuna hamu tu ya kubofya bofya vibofyeo vyetu! Nimekwambia timu inaundwa na wachezaji kumi na moja wa uwanjani na benchi la ufundi! Wale wa uwanjani kila mmoja ana nafasi yake samatta atafunga, vipi kama huku ukuta unavuja thamani ya goli la samatta litapotea katika kupata point kwa timu. Kama jana wasingeruhusu goli basi goli la samatta lingekuwa na thamani kwa timu nzima! Lingewapa pointi 3 kama wangeruhusu moja basi lingekuwa na thamani ya pointi moja kwa timu lakini kwa kuwa wamefungwa wao, goli la samatta linakuwa muhimu kwake, kwenye takwimu zake.
 
Naomba serikali ya awamu ya tano iingilie hili swala la Jack Glealish kuwa mchoyo Sana wa pasi hivyo kumnyima nafasi champion boy Mbwana Samatta kupachika magoli.

Ni wazo tu😎
 
Hiki ni kikundi cha wahuni na wavuta bangi kilichoamua kucheza mpira.
 
Kama kawaida ......

Tupo pamoja na Samatta kupeana Updates zote hapa .

Mechi ya kwanza ya Samatta Leo 28-01-2021
Aston Villa Vs Leicester City

Sent from my SM-J700H using Tapatalk

Modereta; tafadhali pin uzi huu pale mbele uwe sticky kusudi na sisi wafuasi wa Samatta tuwe tunaangushia kidogo kidogo kwa urahisi. Wale wachawi wa Samatta, waache walie tu. Pamoja na kuwa hakufunga bao, lakini alikuwa wa kuogopwa. hata lile bao la kwanza walilojifunga, lilikuwa tayari ni lake.

 
Hawa Aston villa ni kama vile wamedhamilia kushuka daraja....mpaka Dk 55 hawana shot on target dhidi ya southampton
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…