Aston Villa yarejea ligi kuu ya England

Hivi bingwa wa championship na bingwa wa playoff final nani anapata mkwanja mrefu zaidi,
Nauliza kwa kupata elimu mkuu sio naku challenge [emoji120]

Ok, bingwa wa play-off anapata zaidi kutokana na fedha nyingi inayokusanywa kutokana na mapato ya televisheni na matangazo ya ndani na nje ya Uingereza.

Kisha kuna fedha inayoitwa Merit payments ambayo timu hulipwa kuwa ubora wa uchezaji wake hadi kushinda mechi ya play-off.

Halafu kuna kitu chaitwa equal share payments kwa kila timu itakayocheza hiyo play-off hivyo pia kuweka umuhimu kwa kila timu angalau kufikia hiyo stage.

Kwahio zikikusanywa zote hizi fedha zinafikia kiasi kama hicho cha pauni milioni170 na bingwa anapata kitita chote hicho.

Kiasi hicho huweza kupungua au kuongezeka kulingana na mchanganuo nilioulezea.

Bingwa wa Championship yeye anapata mgao wake wa kawaida wa ligi ambayo hugawanya kwa timu zote kuanzia yule bingwa hadi timu ya chini kabisa, ila bingwa anapata zaidi.

Hivyo basi, bingwa wa play-off anapata zaidi ya bingwa wa championship.

Lakini macho na masikio mara nyingi huelekezwa kwenye mechi ya Play-off.
 
Hao wamiliki ni wawili ila ni watatu!
 
Shukrani mkuu kwa maelezo yanayojitosheleza.
Be blessed [emoji120]
 
Huyo mchina amewaita hao wawili na ana shea ndogo sana.

Hao wawili ndo majority shareholders.

🙂🙂
Extra Question mkuu.
What if,an England team from League one side wins Europa cup,
Will it play the Next season's Uefa?
 
Extra Question mkuu.
What if,an England team from League one side wins Europa cup,
Will it play the Next season's Uefa?

League One ni ya pili katika ligi ndogo za chini lakini ni ligi ya tatu kwa mfumo wa ligi za Uingereza.

Yaani kuna Premier League, Championship na League One.

Bingwa wa League One hupanda kucheza Championship na hawezi kuruka kwenda Europa mpaka awe amecheza Championship hadi Premier league.

Timu zinazocheza Europa ni za kutoka kwenye Premier league ambazo kwa msimu ujao zitakuwa ni Arsenal, Manchester United na Wolverhampton.
 
Akikata ticket via F.A cup mkuu
 
Akikata ticket via F.A cup mkuu

Kwa kuwa Manchester City alishinda FA Cup na tayari anafuzu kucheza champions league, basi Wolverhampton ndie aliepewa nafasi ya kucheza Europa league.
 
Kwa kuwa Manchester City alishinda FA Cup na tayari anafuzu kucheza champions league, basi Wolverhampton ndie aliepewa nafasi ya kucheza Europa league.
Sijakupata mkuu..
Nliongelea team ya league one kuingia Europa kwa ticket ya F.a cup'
 
Sijakupata mkuu..
Nliongelea team ya league one kuingia Europa kwa ticket ya F.a cup'

Ni vigumu sana kwa sasa kwa timu ya League One kushinda FA Cup.

Mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 1980 West Ham United ilipofanya hivyo.

FA Cup ni njia mojawapo ya kuzisaida timu ndogo kuongeza fedha za mapato kwa kucheza na timu kubwa, lakini si kujitutumua kutaka kutwaa kombe la FA.
 
kwenye mpira yote yanawezekana mkuu, sikuu man city inacheza fa na kale ka team(nimesahau jina). kakampiga city mbili za harakaharaka bahati nzuri city akazisawazisia dk za mwishoni akafunga la ushindi. hapo city chupu atupwe nje za mashindano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…