Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Hivi bingwa wa championship na bingwa wa playoff final nani anapata mkwanja mrefu zaidi,
Nauliza kwa kupata elimu mkuu sio naku challenge [emoji120]
Ok, bingwa wa play-off anapata zaidi kutokana na fedha nyingi inayokusanywa kutokana na mapato ya televisheni na matangazo ya ndani na nje ya Uingereza.
Kisha kuna fedha inayoitwa Merit payments ambayo timu hulipwa kuwa ubora wa uchezaji wake hadi kushinda mechi ya play-off.
Halafu kuna kitu chaitwa equal share payments kwa kila timu itakayocheza hiyo play-off hivyo pia kuweka umuhimu kwa kila timu angalau kufikia hiyo stage.
Kwahio zikikusanywa zote hizi fedha zinafikia kiasi kama hicho cha pauni milioni170 na bingwa anapata kitita chote hicho.
Kiasi hicho huweza kupungua au kuongezeka kulingana na mchanganuo nilioulezea.
Bingwa wa Championship yeye anapata mgao wake wa kawaida wa ligi ambayo hugawanya kwa timu zote kuanzia yule bingwa hadi timu ya chini kabisa, ila bingwa anapata zaidi.
Hivyo basi, bingwa wa play-off anapata zaidi ya bingwa wa championship.
Lakini macho na masikio mara nyingi huelekezwa kwenye mechi ya Play-off.