Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Akituelekeza namna ya kufika nyumbani kwake Kigamboni leo asubuhi Bi. Mwajame bint Dossa Aziz akamaliza kwa kusema, "Ukifika hapo utaona kibao kimeandikwa "Mwajame Street."
Mpwa wangu Yusuf aliyekuwa ananiendesha akashtuka na kuzungumza na Bi. Mwajame akasema "Mjomba Mtaa una jina lake!"
Hakika hata mimi nilishtuka.
Bi. Mwajame ni mtoto wa Dossa Aziz.
Dossa Aziz ni katika wazalendo 17 waliounda TANU mwaka wa 1954 na kati ya wafadhili wakubwa wanne wa chama hicho: John Rupia, Dossa Aziz na ndugu wawili Abdul na Ally Sykes.
Nimeshtuka kwa sababu juu ya makubwa ambayo baba yake kafanya katika kupigania uhuru wa Tanganyika hajatunukiwa mtaa si nyumbani kwao Gerezani wala popote pale.
Iweje mwanae apewe mtaa?
Yusuf Makamba kapewa mtaa jirani na alipozaliwa Dossa Mtaa wa Mbaruku na Congo na waliotoa mtaa huo kumpa Makamba ni kama vile hawamjui Dossa Aziz wala hawajapata kumsikia.
Wewe nani umtangulie Dossa kupata mtaa?
Dossa Aziz katika siku za mwanzo kabisa za kupigania uhuru alitoa gari yake kumpa Mwalimu Nyerere imsaidie katika kufanikisha majukumu yake kama President wa TANU.
Kasahaulika!
Hana mtaa wala chochote cha kuonyesha kutoka nchini kwake na kutoka chama alichokiunda na kukifadhili. Dossa hakupewa hata mtaa. Mwanae Mwajame kapewa mtaa Kigamboni.
Hakika nilistaajabu sana. Haya mambo yakoje?
Wakati wake Dossa walimpa lakabu wakimwita "The Bank."
Huendi benki ukaambiwa fedha zimekwisha njoo kesho.
Hana mtaa kwao Gerezani.
Nimeshuka kwenye gari na Shariff Yusuf mpwa wangu akanipiga picha kwenye kibao hicho chenye jina la dada yangu Mwajame.
Mwajame bint Dossa ana mtaa Kigamboni. Da Mwajame anasema mtaa ule hakuupata kwa kutumia mgongo wa baba yake.
"Mimi nilipigiwa simu na Mwenyekiti wa Mtaa kuelezwa kuwa jina langu limepewa mtaa ninaokaa kwa kuwa mimi ni mkazi wa zamani kupita wote.
Baada ya kupewa mtaa ndipo niliposikia wakimtaja baba yangu kuwa alikuwa mfadhili wa TANU na rafiki wa Nyerere."
Bi. Mwajame anakumbuka maasi ya Tanganyika Rifles mwaka 1964 na simanzi iliyomfika baba yake wakati huo Dossa akiishi shambani kwake Ruvu.
"Baba kaja nyumbani Mtoni kwa Aziz Ali na mkewe Bi. Nagla anaendesha Land-rover akamweleza bibi kuwa kumetokea maasi ya wanajeshi na Nyerere kapotea hajulikani alipo.
Baba akasema kuwa anamwacha mkewe hapo yeye anakwenda kumtafuta Nyerere.
Kwanza Bi. Nagla akasema yeye hakubali Dossa aende peke yake lazima awe na yeye. Bibi akamuuliza baba, "Dossa utampata wapi Nyerere na vurugu hili?"
Baba akawa anabishana na mama anamwambia, "Nagla utaniponza tukamatwe sote, wanajeshi wanakamata Wahindi na Waarabu." Bi. Nagla alikuwa kachanganya damu.
"Mwishowe baba na mama wote wakaondoka. Siku nzima nyumba nzima ilikuwa na simanzi wakihofia maisha ya Nyerere na ya baba aliyekwenda kumtafuta rafiki yake.
"Usiku baba alirudi nyumbani peke yake hoi kachoka, akamweleza bibi kuwa Nyerere yuko salama."
"Yuko salama wapi?" Bibi anataka kujua.
"Baba hakumwambia yeye kashikilia tu kuwa Nyerere mzima yuko salama.
"Baba alisimamishwa mara mbili na wanajeshi wakati anatoka Mtoni.
"Alisimamishwa makutano ya Pugu Road na Msimbazi karibu na ofisi za mabasi ya DMT yaani Dar-es-Salaam Motor Transport na makutano ya Msimbazi na Kitchwele.
"Kote aliachiwa kupita bila matatizo wale wanajeshi wakisema, Dossa huyo mwacheni apite."
Hakuna ambae hakuwa anajua uhusiano na Dossa Aziz na Nyerere.
Lakini baba anasema aliona magari mengi pembeni ya barabara yametobolewa matairi.
Ilikuwa wazi wanajeshi hawakutaka kuona magari barabarani.
Nyerere wakati wa kupigania uhuru hata kazi ya ualimu hajaacha alikuwa akija nyumbani Mtaa wa Mbaruku na Congo na Abdul na Ally Sykes wakati mwingine akilala pale.
Kama atalala nyumbani chumba chake.kilikuwa cha kaka yangu Ali Aziz na Ali atakwenda kulala kwengine kwani alikuwa mtoto bado yuko shule.
Nilikuja kujua baadae kuwa baba katika fikra zake alikuwa anadhani Nyerere kwa kuwa hayuko Government House atakuwa kenda kujificha Ruvu shambani kwake ambako wakati wa kupigania uhuru walijenga handaki endapo itabidi kujificha.
Nimemuuliza baba mara nyingi wapi Nyerere alijificha wakati wa maasi lakini baba alikataa kuniambia.
Nikimghasi kutaka aniambie akisema, "Mwajame una maswali kama askari."
Mwajame baada ya kumaliza masomo alijiunga na jeshi la polisi.
Muhimu wanahistoria wafanye utafiti kujua hili handaki shambani kwa Dossa liko wapi kwani ni sehemu muhimu ya historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Bi. Mwajame anasema baba yake alipata kumweleza kuwa ile nyumba ya baba yake Ruvu walikuwa wakiitumia wakati mwingine kama sehemu yao moja ya kutafuta faragha TANU inapokuwa na jambo lake lililohitaji kujadiliwa kwa utulivu.
Lakini anasema lile handaki ilikuwa siri kubwa.
Yeye alikuja kulisikia kwa mfanyakazi wao mmoja wa shamba.
Huyu ndiye aliyemfahamisha miaka mingi baadae kuwa katika moja ya mashamba ya Dossa Aziz palijengwa handaki.
Historia ya Nyerere alitoka vipi Government House wakati wa maasi niliyosikia kutoka kwa Kitwana Kondo inatofautiana kidogo na historia aliyoandika Peter Mbwimbo katika kitabu chake, ''Mlinzi Mkuu wa Mwalimu Nyerere,'' (2015).
Bi. Mwajame ana mengi katika udugu na urafiki baina ya baba yake na Nyerere ambae anasema baba yake akipenda kumwita, "Kambarage."
"Nilikwenda kwa baba kumuomba mtaji nifuge kuku."
Baba akaniambia, "Nenda kwa Kambarage." Nilikuwa naogopa lakini yeye akanishikilia niende.
Nilikwenda Msasani.
Foleni ya kuonana na Mwalimu ndefu mpaka naingia kumuona jua limekuchwa. Mwalimu alikuwa kanisahau. Nikamweleza shida yangu.
Mwalimu akataka kujua mahitaji yangu. "Mwalimu nitapokea chochote utakachonipa."
Mwalimu akaweka oda nipewe vifaranga 500 pamoja na chakula na madawa.
Mwalimu alipojua kuwa naendesha scooter akaagiza nipelekwe na "escort" hadi nyumbani.
Baada ya siku mbili vifaranga na kila kitu changu vikaletwa nyumbani Mtoni.
Kuku wangu walipokua nikachukua kuku 20 nikawachinja nikampelekea Mwalimu.
Wasaidizi wa Mwalimu waliponiona walikuwa sasa wananifahamu wananiita Mtoto wa Dossa.
Wakanipeleka kwa Mama Maria. Mama Maria alinishangaa, "Mwajame umekuwa mkubwa kiasi hiki!"
Mwanahistoria mkubwa wa historia ya Tanganyika John Iliffe alipata kusema kuwa historia nyingi ya TANU ipo mikononi mwa watu binafsi.
Mimi nakubaliana na yeye kwani mimi kila ninapopata nafasi ya kuzungumza na wale waliokuwapo nyakati zile za kupigania uhuru hukutana na historia ambayo kamwe sijapata kuisikia popote.
Hasa ninapokutana na watoto wa wapigania uhuru hawa huwa na historia za kusisimua.
Mimi sikujua kuwa ile nyumba aliyotafutiwa Nyerere na TANU Maduka Sita Magomeni, mdogo wake Dossa Ramadhani Aziz yeye alikuwa pale kabla akiendesha duka lake.
Kiasi mtu unapata picha kama vile marafiki wa Nyerere hawakutaka Mwalimu awe popote pale peke yake bila ya wao kuwa na mtu wao jirani yake.
Dossa Aziz