Asubuhi Moja Kigamboni na Bi. Mwajame bint Dossa Aziz

Asubuhi Moja Kigamboni na Bi. Mwajame bint Dossa Aziz

Hasha wa kala "kijiko kiitwe kijiko"
Plato...
Ahsante sana.
Umeeleza vizuri. Mwajame kaeleza vizuri. Inaonyesha Wazee wetu walifanyiana hisani nyingi ila kwa sababu ya adabu zao wakawa hawatangazi.

Ashakum si matusi ila Mzee MS Inaonyesha ni Mtu ambaye akikusaidia atakusimanga mpaka kaburini. Na kuna wakati unaweza kuona anaeleza habari zako kumbe 'simango'. Tuliozaliwa Pwani tunajua hayo.

Atakwambia mpaka alichokuwa Mwalimu anakula kwa Sykes.
Shukuru...
Haikuwa kazi nyepesi kuandika kitabu cha Abdul Sykes.

Mimi nimejitahidi sana kuandika maisha ya Mwalimu kwa tahadhari kubwa.

Sijamtusi wala sijamsimanga Mwalimu la kama una ushahidi kuwa nimefanya hivyo lete hapa ushahidi wako wote wauone.

Nina makala iliyoandikwa na Daisy Sykes mwaka wa 2018 katika kumbukumbu ya miaka 50 ya kifo cha baba yake.

Makala hii iliandikwa kwa Kiingereza nami nikaitafsiri kwa kuchapwa na Raia Mwema.

Ilichapwa matoleo matatu.

Daisy kaeleza udugu wa ndani uliokuwa baina ya baba yake na Nyerere.

Hapa Daisy alikuwa hajafikisha hata umri wa miaka 10.

Kama kueleza habari ya chakula Daisy ndiye kaeleza kama kumbukumbu yake jinsi alivyokuwa akimpikia Mwalimu chai kila alipokuja kwao akitokea Pugu.

Daisy ndiye aliyeeleza urafiki uliokuwapo baina ya mama yake Bi. Mwamvua na Mama Maria yeye Daisy akitumwa na mama yake kumpelekea chakula Mama Maria kwenye duka lake la mafuta ya taa Mtaa wa Mchikichi na Livingstone.

Kwangu mimi na kwa wasomaji wengi hii ilikuwa historia ya kujitolea kwa wazalendo kukabiliana na maisha magumu wakati Mwalimu kaacha kazi kuitumikia TANU na sasa anaishi nyumbani kwa Abdul Sykes.

Haya si masimango.

Daisy hakuwa anaandika bali alikuwa analia na kumuomboleza baba yake dunia imjue alikuwa nani na aliifanyia nini Tanganyika.

Daisy anaeleza kejeli zilivyoanza dhidi ya baba yake pale ilipokuwa dhahiri kuwa uhuru wa Tanganyika uko mlangoni unabisha hodi.

Wanasema viongozi wapya katika TANU New Street kuwa Abdul hakuongoza chama chochote cha siasa.

Wanasema Abdul Sykes aliongoza TAA chama cha starehe.

Makala hii ya Daisy ilinipa changamoto kubwa kuitafsiri kwa Kiswahili na kuiweka katika hali ambayo haitatuumiza sote.

Inataka moyo mkubwa kustahamili haya yote na nakueleza kuwa kuna mengi hayajasemwa.

Yawezekana wewe unaona masimango kwa kuwa Abdul Sykes alifutwa katika historia na nilipoandika historia yake wewe kwa kuwa hukuwa unaijua umepigwa na dhoruba kali.

Wengi hili limewapata lakini hakutokea hata mmoja kuniambia nasimanga.

Yako mengi ningeweza kukueleza tena kutoka kinywa cha baba yangu kwani alikutana na Abdul Sykes Matasalamat Building Independence Avenue siku chache kabla ya kifo chake.

Dar es Salaam ilikuwa inawaka moto kwa mgogoro wa EAMWS na masheikh kukamatwa usiku wa manane.

Baba yangu alikuwa sehemu ya historia ya Abdul Sykes na Mwalimu kwani alimuona Nyerere kwa mara ya kwanza nyumbani kwa Abdul Mtaa wa Aggrey na Sikukuu.

Historia hii si nyepesi.
 
Back
Top Bottom