Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Kumekucha tena.
Hili siala limeshajadiliwa sana sehemu mbalimbali. Hivi kwa taifa hili changa tunajivunia nini kuanza kujadili michezo redioni na kwenye televisheni saa 2 asubuhi? Kweli?
Najua wapo watawala wana hofu kuhusu wenye nchi kuwa na uelewa wa mambo yanayowahusu na hatimaye kuchukua hatua stahiki. Najua pia vipo vyombo vya habari vyenye hofu hiyo ya kuonekana kinzani. Najua pia vipo vyombo vya habari vyenye hofu ya kupoteza wateja na matangazo kwa sababu hizo.
Watanzania wanapaswa kujengwa katika namna ambayo itawainua kifikra. Media leo inataka kuheshimiwa wakati 24/7 ni mpira na matangazo ya kamari tu? Leo ukiuliza nusu ya watanzania bajeti iliyopitishwa juzi ni ya thamani gani hawajui.
Ifike pahala media zione tija katika kuwapa maarifa wananchi kuhusu hatima zao kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiteknolojia, na kiburudani pia.