Asubuhi ni muda wa kujadili masuala ya kitaifa/kimataifa kwenye vyombo vya habari (media), sio burudani

Kumekucha tena.

Hili siala limeshajadiliwa sana sehemu mbalimbali. Hivi kwa taifa hili changa tunajivunia nini kuanza kujadili michezo redioni na kwenye televisheni saa 2 asubuhi? Kweli?

Najua wapo watawala wana hofu kuhusu wenye nchi kuwa na uelewa wa mambo yanayowahusu na hatimaye kuchukua hatua stahiki. Najua pia vipo vyombo vya habari vyenye hofu hiyo ya kuonekana kinzani. Najua pia vipo vyombo vya habari vyenye hofu ya kupoteza wateja na matangazo kwa sababu hizo.

Watanzania wanapaswa kujengwa katika namna ambayo itawainua kifikra. Media leo inataka kuheshimiwa wakati 24/7 ni mpira na matangazo ya kamari tu? Leo ukiuliza nusu ya watanzania bajeti iliyopitishwa juzi ni ya thamani gani hawajui.

Ifike pahala media zione tija katika kuwapa maarifa wananchi kuhusu hatima zao kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiteknolojia, na kiburudani pia.
Unawapangia watu walioweka mitaji yao
 
Ni kweli kabisa. Lakini kwa hali ya sasa inahitaji juhudi za ziada kuhakikisha kwanza huu mtazamo wa sasa unaondoka. Kwamba hata wanaoanzisha media wanaona soko lipo katika burudani. regulations ziwepo kwanza. Muda wa burudani unaweza kuwa kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 1 usiku. Muda mwingne ni wa kuwajenga wananchi kifikra.
Pengine pia sina uwezo wa kuanzisha media. natoa mawazo yangu kama hivi ili wenye nguvu wakiona fursa waitumie.
Nimewahi kusikikia kuna muda maalumu kisheria wa kunywa pombe Bar, kwamba siku za kazi ni kinyume cha sheria kunywa pombe asubuhi au mchana, sina uhakika kama ni kweli.
 
Kwa habari ya maslahi ya kitaifa, hakuna namna. Taarifa za kimaendeleo ziwe kama dozi. Utake usitake. Yani kijana anasikioiza michezo redioni akiwa anachokonoa meno na stiki toka china, mtumba toka Taiwan, sandals toka china, saa na simu imported. Redio yenyewe toka Malaysia, Mafuta ya kujipaka toka Kenya. Pakistani hapo watu wako na viwanda barabarani kama wamachinga wanazalisha vitu hatari. Tumebakia kusema wacha tusikilize tunachopenda
Kweli mkuu ila hiyo kazi wanaiweza TBC tu
 
Kila mtu ana uhuru wa kuchagua anachopenda.

Kuna watu wengine hawajali tu mambo mnayojali nyie, na hilo sio lazima limaanishe wamedumaa akili.
Kutokujali mambo muhimu yanayogusa ubora wa maisha yako directly na kujali(kuwa obsessed na)mambo yasiyogusa ustawi wa maisha yako ni udumavu wa akili.
 
Hapana.

Kumuamulia mtu mwingine jambo gani ni muhimu kwake ni arrogance ya hali ya juu. Muache aamue mwenyewe. Wewe sema jambo gani ni muhimu kwako.

Kuna watu wamekimbia hizo mbio zenu wamewapita mpaka wakawazunguka mara mbili.

Kuna watu wamesoma siasa, wamesoma falsafa, wamesoma sayansi, na wamegundua kuwa dunia hii ina matatizo ya kimsingi kabisa ambayo hizi kelele zenu za kubadili mifumo hazitasaidia kitu kubadilika, na hata mkibadili kitu, mtazalisha matatizo mapya muendelee kulalamika vilevile.

Kwa hivyo, kitu muhimu ni kufanya unayopenda. Kama unapenda michezo, fuatilia michezo.

Na kuna mtu michezo ndiyo jambo litakalomtoa kwenye maisha haya, sasa huyo unamlazimishaje afuatilie siasa sana?
 
Kumekucha tena.

Hili siala limeshajadiliwa sana sehemu mbalimbali. Hivi kwa taifa hili changa tunajivunia nini kuanza kujadili michezo redioni na kwenye televisheni saa 2 asubuhi? Kweli?

Najua wapo watawala wana hofu kuhusu wenye nchi kuwa na uelewa wa mambo yanayowahusu na hatimaye kuchukua hatua stahiki. Najua pia vipo vyombo vya habari vyenye hofu hiyo ya kuonekana kinzani. Najua pia vipo vyombo vya habari vyenye hofu ya kupoteza wateja na matangazo kwa sababu hizo.

Watanzania wanapaswa kujengwa katika namna ambayo itawainua kifikra. Media leo inataka kuheshimiwa wakati 24/7 ni mpira na matangazo ya kamari tu? Leo ukiuliza nusu ya watanzania bajeti iliyopitishwa juzi ni ya thamani gani hawajui.

Ifike pahala media zione tija katika kuwapa maarifa wananchi kuhusu hatima zao kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiteknolojia, na kiburudani pia.
Mpira siyo asubuhi tu yaani masaa yote ni habari za.michezo asubuhi yombo vyetu vya habari havipo huru mchana .jioni na usiku. Tunapumbazwa sana bonbo ili tusahau mambo ya msingi
 
Hapana.

Kuna watu wamekimbia hizo mbio zenu wamewapita mpaka wakawazunguka mara mbili.

Kuna watu wamesoma siasa, wamesoma falsafa, wamesoma sayansi, na wamegundua kuwa dunia hii ina matatizo ya kimsingi kabisa ambayo hizi kelele zenu za kubadili mifumo hazitasaidia kitu kubadilika, na hata mkibadili kitu, mtazalisha matatizo mapya muendelee kulalamika vilevile.

Kwa hivyo, kitu muhimu ni kufanya unayopenda. Kama unaoenda michezo, fuatilia michezo.

Na kuna mtu michezo ndiyo jambo litakalomtoa kwenye maisha haya, sasa hiyo unamlazimishaje afuatilie siasa sana?
Nakuhakishia wengi wao hawajagundua hata hayo unayosema wamegundua wala hawajafanikiwa kupata ellimu ya maana, pia kimsingi sio kwamba washaangaji wanawataka wafuatilie siasa zao bali wafuatilie masuala yanayogusa maisha yao kama barabara, maji, hospitali na umeme.
Kutaka barabara ya lami sio siasa,
Kutaka umeme usikatike sio siasa,
Kutaka hospitali bora sio siasa.
 
Unataka kufanya social engineering jamii iwe unavyotaka wewe, wakati jamii yenyewe kwa kiasi kikubwa haitaki kuwa hivyo.

Unaliangalia tatizo kutoka upande mbaya, unaanzia juu kuja chini badala ya kuanzia chini kwenda juu.

Watu wengi wakipata elimu na kuelewa vipaumbele ni vipi, wafanyabiashara wenyewe watabadili priority kwenda na market demand.

Sasa hivi market inataka kusikiliza habari za Diamond na mpira, kwa sababu hapo ndipo utashi wa watu ulipo.

Ukiwalaumu wafanyabiashara kwa kuwapa watu wanachotaka unakuwa hujawatendea haki hao wafanyabiashara wala hao watu.
Nikikazia kwenye aya ya tatu, watu wengi wakipata elimu. Sasa elimu inatoka kwenye hizo hizo media, na media zinaendeshwa na wafanyabiashara. Ukiacha elimu ya msingi (formal), hii nyingine itapatikana kwa ushawishi pia.
Serikali inapotaka jambo lake litekelezwe huwa haiangalii utashi wa watu, bali utekelezaji wa kilichopangwa. Wakati mwingine sio kwa lazima, bali kwa ushawishi na takrima
 
1. Unaweza kufikiri utawaelimisha watu, halafu watu wakakuelimisha wewe zaidi. Angalia post inayofuata hapo chini #32 .

2. Wafanyabiashara wana haki ya kupanga vipindi wanavyotaka wao kwa kuangalia hadhira yao inataka nini na faida itapatikanaje.

3. Wewe pia una haki ya kuanzisha media yako na kutangaza unachotaka.

4. Serikali isiyoangalia utashi wa watu ni serikali ya kidikteta ambayo inaweza kutumia pesa nyingi kuleta maendeleo ambayo watu hawayataki.

5. Acha watu wawe na uhuru wa kusikiliza na kupanga wanacjotaka kisikilizwe. Kama hukiowndi, na wewe una haki ya kusikiliza unachotaka au kupanga unachotaka kisikilizwe. Tafuta hela uanzishe media yako upange cha kusikikizwa, usipangie watu baki waliowekeza hela zao nini cha kutangaza.
 
Nakuhakishia wengi wao hawajagundua hata hayo unayosema wamegundua wala hawajafanikiwa kupata ellimu ya maana, pia kimsingi sio kwamba washaangaji wanawataka wafuatilie siasa zao bali wafuatilie masuala yanayogusa maisha yao kama barabara, maji, hospitali na umeme.
Kutaka barabara ya lami sio siasa,
Kutaka umeme usikatike sio siasa,
Kutaka hospitali bora sio siasa.
Niende kujieleza kwa mfano mmoja.

Balozi wa Marekani alienda Kojani, Kojani huko Zanzibar, Pemba visiwa vidogo vya karibu na Pemba huko.

Alipofika huko, akavutiwa sana na mandhari ya kisiwa cha Kojani.

Lakini akaona kile kisiwa hakina daraja la kukiunganisha na kisiwa cha Pemba.

Kwa akili zake yule balozi, akaona hapa ni muhimu sana kuwe na daraja.

Akawauliza wale Wakojani, hapa vipi, je, mnataka kuwe na daraja?

Wale Wakojani wakakataa, wakasema hatutaki daraja hapa asilani.

Yule balozi akashangaa sana. Akaona hawa Wakojani vipi? Akawa anawaelewesha hapa mkipata daraja mtapata maendeleo, kwa nini hamtaki daraja? Akaanza kuona wale Wakojani kama wajinga hivi kwa kukataa daraja.

Wale Wakojani wakamuambia balozi, ujue kwa mtazamo wako, daraja litaleta maendeleo hapa, lakini, unafikiri hivyo kwa sababu hupaelewi hapa tu. Kwetu sisi tunaopaelewa hapa, tuna migogoro mingi na serikali ya CCM. Kila kwenye uchaguzi kuna mauaji, polisi wananyanyasa raia. Sisi hapa Kojani tunapata afadhali kwa sababu hakuna daraja. Mkiweka daraja hapa, mtawarahisishia sana polisi kuja kutuua huku.

Yule balozi akawa kawaelewa.

Habari hii inatufundisha nini?

Usimuone mtu mjinga kwa sababu hajachagua kitu ulichochagua wewe, wakati hujui sababu zake za kuchagua alichochagua hivyo ni zipi.

Nyie mpaka sasa mnachofanya ni kumlazimisha Mkojani apende daraja kama yule balozi wa Marekani.

Mnamhukumu Mkojani kwamba ni mjinga kwa kutotaka daraja, wakati hata hamjui sababu zake za kukataa daraja.
 
Kumekucha tena.

Hili siala limeshajadiliwa sana sehemu mbalimbali. Hivi kwa taifa hili changa tunajivunia nini kuanza kujadili michezo redioni na kwenye televisheni saa 2 asubuhi? Kweli?

Najua wapo watawala wana hofu kuhusu wenye nchi kuwa na uelewa wa mambo yanayowahusu na hatimaye kuchukua hatua stahiki. Najua pia vipo vyombo vya habari vyenye hofu hiyo ya kuonekana kinzani. Najua pia vipo vyombo vya habari vyenye hofu ya kupoteza wateja na matangazo kwa sababu hizo.

Watanzania wanapaswa kujengwa katika namna ambayo itawainua kifikra. Media leo inataka kuheshimiwa wakati 24/7 ni mpira na matangazo ya kamari tu? Leo ukiuliza nusu ya watanzania bajeti iliyopitishwa juzi ni ya thamani gani hawajui.

Ifike pahala media zione tija katika kuwapa maarifa wananchi kuhusu hatima zao kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiteknolojia, na kiburudani pia.
Simba na Yanga ni project za CCM za kuwapumbaza Watanganyika.
 
Huwa nikiona mzee wa azam kakusanya watu huko mtaan na anawafanya watu wabishane kwa mambo ya mpira,huwa nasikitika sana yaan watu wanavyoshupaza shingo kubishana
 
Niende kujieleza kwa mfano mmoja.

Balozi wa Marekani alienda Kojani, Kojani huko Zanzibar, Pemba visiwa vidogo vya karibu na Pemba huko.

Alipofika huko, akavutiwa sana na mandhari ya kisiwa cha Kojani.

Lakini akaona kile kisiwa hakina daraja la kukiunganisha na kisiwa cha Pemba.

Kwa akili zake yule balozi, akaona hapa ni muhimu sana kuwe na daraja.

Akawauliza wale Wakojani, hapa vipi, je, mnataka kuwe na daraja?

Wale Wakojani wakakataa, wakasema hatutaki daraja hapa asilani.

Yule balozi akashangaa sana. Akaona hawa Wakojani vipi? Akawa anawaelewesha hapa mkipata daraja mtapata maendeleo, kwa nini hamtaki daraja? Akaanza kuona wale Wakojani kama wajinga hivi kwa kukataa daraja.

Wale Wakojani wakamuambia balozi, ujue kwa mtazamo wako, daraja litaleta maendeleo hapa, lakini, unafikiri hivyo kwa sababu hupaelewi hapa tu. Kwetu sisi tunaopaelewa hapa, tuna migogoro mingi na serikali ya CCM. Kila kwenye uchaguzi kuna mauaji, polisi wananyanyasa raia. Sisi hapa Kojani tunapata afadhali kwa sababu hakuna daraja. Mkiweka daraja hapa, mtawarahisishia sana polisi kuja kutuua huku.

Yule balozi akawa kawaelewa.

Habari hii inatufundisha nini?

Usimuone mtu mjinga kwa sababu hajachagua kitu ulichochagua wewe, wakati hujui sababu zake za kuchagua alichochagua hivyo ni zipi.

Nyie mpaka sasa mnachofanya ni kumlazimisha Mkojani apende daraja kama yule balozi wa Marekani.

Mnamhukumu Mkojani kwamba ni mjinga kwa kutotaka daraja, wakati hata hamjui sababu zake za kukataa daraja.
Mkuu, huu mfano japo balozi aliwaelewa, alichagua tu kuwaelewa bali aliwaacha na fikra zao. Kama Kojani ni sehemu ya Tanzania, unadhani serikali itaenda kutaka ridhaa ya wakojani kuweka miundombinu? Siku wakitaka maji ya kinywa na serikali ikasema msiipangie watasemaje? Wakati ukifika serikali aidha kwa hela za ndani au za huyo balozi, daraja litajengwa. Hivyo serikali au taasisi zikiamua, upepo wa kifikra utabadilika.

Hivi unadhani leo hii ikatokea serikali iwe ya upinzani na ccm wakawa wapinzani ila bado wakabaki na ushawishi fulani huoni wanaweza kushawishi media kuwa na vipindi vya kiharakati kuwafumbua wananchi macho kuhusiana na watawala?
 
1. Unaweza kufikiri utawaelimisha watu, halafu watu wakakuelimisha wewe zaidi. Angalia post inayofuata hapo chini #32 .

2. Wafanyabiashara wana haki ya kupanga vipindi wanavyotaka wao kwa kuangalia hadhira yao inataka nini na faida itapatikanaje.

3. Wewe pia una haki ya kuanzisha media yako na kutangaza unachotaka.

4. Serikali isiyoangalia utashi wa watu ni serikali ya kidikteta ambayo inaweza kutumia pesa nyingi kuleta maendeleo ambayo watu hawayataki.

5. Acha watu wawe na uhuru wa kusikiliza na kupanga wanacjotaka kisikilizwe. Kama hukiowndi, na wewe una haki ya kusikiliza unachotaka au kupanga unachotaka kisikilizwe. Tafuta hela uanzishe media yako upange cha kusikikizwa, usipangie watu baki waliowekeza hela zao nini cha kutangaza.
Utashi ni pamoja na mambo yenu huko Ulaya na Marekani ya WOKE. sasa ikifika hatua wananchi/kikundi fulani wakaanza kutaka mambo ya my body my choice, serikali itaridhia tu? Na ni maendeleo gani ambayo watu hawatayakata? Sijawahi kuona. Ukishasema maendeleo tayari ni hali chanya. Hao wakoani si ndio wale wakienda kuuza nazi na mteja akija kununua zote hawataki kuuza? Eti ukinunua zote n'tauza nini miye 😀
 
Kitu cha msingi ni kwamba kila mtu ana haki ya kujiamulia maisha yake mwenyewe yaendeje, hii ni haki ya kikatiba na kibinadamu, ipo katika Universal Declaration of Human Rights tangu December 10 1948.

Wewe kumuamulia mtu anayetaka kusikiliza mpira kwamba mpira si muhimu, asikilize unachotaka wewe, ni arrogance, hata kama unachosema ni kweli.

Chukua muda wako umuelimishe vizuri.

Pia, mfanyabiashara akitumia hela yake kuanzisha media yake, huna haki ya kumpangia atangaze nini.

Fungua yako na wewe upange unachotaka kutangaza.
 
Well said. Ndio maana sehemu fulani nilizungumzia ushawishi na tskrima. Uzuri mambo kama haya huanza kama vuguvugu/trend kisha hushika hatamu. Wakati utafika watu (hasa wazima miaka 35+) wataona kusikiliza burudani mfululizo ni utoto.

Kama ambavyo imetokea wakongwe wa bongo fleva wamechoka kusikiliza hawa Gez Z na sasa wanarudi kwa millennial na Gen X. Hivyo hivyo itatokea kwa upande huu tunaoujadili
 
Back
Top Bottom