.
Ulimbo, tuweke na mipaka basi ili isije onekana ni chuki binafsi dhidi ya watoto wa viongozi. Uongozi haurithishwi, ni ama kipaji mtu anazaliwa nacho (born leader) kama kina Nyerere au na maandalizi, groomed leaders (man made) kama kina JK .
Hao vijana wanauwezo wao binafsi waliozaliwa nao, ndio maana wanafuata nyayo za wazazi wao. Issue iwe ni uwezo wa uongozi ndio uwe msingi wa mjadala na sio ni mtoto wa nani. Mimi binafsi nawakubali baadhi ya vijana wote wenye uwezo na kuamua kutangaza nia, hata kama majina yao ya ubini ni mtaji.
Kwa mfano, binafsi namkubali sana huyu kijana Nape, amesimama independently kuhesabiwa na sio kwa mgongo wa baba, japo katika harakati za Ubungo, nina side na JJ.Myika.
Kuna issue ya kuwa na kipaji cha uongozi, kijana Riz alikuwa kiongozi pale UDSM, wakati huo baba hajaingia Magogoni, kama ana interest, na ana uwezo, kwanini asigombee?!. Yaani apoteze haki yake ya kuchagua ama kuchaguliwa eti kwa sababu tuu baba ni fulani?. No way!,
Mbona Vita yuko mjengoni?, nenda Riz nenda Janu pia nenda, Nape nae aende, kama Fred ana interest pia aingie, William pia aingie, Kina Steve na Niko pia kama wana interest nao waacheni waingie. Tuwahukumu hawa vijana with their own merits na sio kutokana na majina yao ya ubini.