Deadbody
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 4,274
- 6,595
Ni hoja nyepesi sana kuijibia kwanini ulikohoa ulipopishana na mwanamke.
Wala haihitaji uwepo wa Peter Kibatala au Tundu Lissu(Kaka wa taifa) wala Fatuma Karume kuijibia kesi hiyo.
Hii ni kesi ambayo hata mtoto mdogo anayesoma shule ya msingi minazi mirefu anaweza simama akashinda mahakamani dhidi ya "porise" mwenye manyota ambayo hayahesabiki begani kwake.
Ni kesi ambayo hata wale wenye broken za ajabu au vituko vilivyoteka JF kutokea kule Facebook wanaweza shinda .
Ni rahisi sana kujibu kesi hiyo kuliko kuelezea kwanini 10 gawanya kwa 5 ni 2.
Ni kesi ambayo hakuna mwanaJF anayeweza shindwa kujibu.
Kama sheria zinazokuja zitakuwa kama hii basi hakuna haja ya kwenda kusoma sheria maana ni kupoteza muda tu.Ukishindwa kujibu kwanini ulikohoa utakuwa sio mtanzania halisi wala mzao wa Adam.
Ni majibu marahisi kabisa yatakayomfanya jaji akupe ushindi.
Ukishindwa kuyasema utakuwa ni "raia wa ajabu kuwahi kutokea"
Upande wa mshtaki :Kwanini ulikohoa ulipopita mbele ya mwanamke?
Deadbody: Nilipaliwa na mate
Hayo ni moja ya majibu ambayo mshtaki hana ushahidi wa kuweka mahakamani.
Majibu yapo mengi ila nasisitiza kuwa ukitiwa hatiani jua wewe ndio KILAZA namba moja East Africa.
Deadbody.