Pre GE2025 Atakayeshidwa CHADEMA avunje makundi

Pre GE2025 Atakayeshidwa CHADEMA avunje makundi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
MIJADALA inayotawala sasa hivi kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusu uchaguzi wa Chadema ngazi ya taifa, huku mchuano ukiwa kati ya mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na makamu wake, Tundu Lissu kutangaza nia ya kuwania uongozi wa juu.

Tunashuhudia minyukano ya makada na hoja zenye mitazamo tofauti za wadau wa siasa, wanaharakati na wananchi wa kawaida.

Makada wa chama hicho wameonekana kugawanyika katika makundi mawili yanayoshutumiana, huku yale ya Lissu yakitaka Mbowe apumzike kwa kuwa ameongoza chama hicho kwa zaidi ya miaka 20.

Soma Pia: Wanachama, Viongozi CHADEMA wagawanyika kambi tofauti, hofu ya mpasuko yaongezeka

Kundi la Mbowe linamshutumu Lissu kuwa ni msaliti kwa kujenga hoja kuwa anaweza kukipasua chama, hivyo wanaona nafasi hiyo iendelee kushikiliwa na Mbowe.

Kwa maoni yangu, kinachoonekana ni kukomaa kwa demokrasia ndani ya chama hicho, lakini sasa tungetamani kuona baada ya kumalizika uchaguzi, atakayeshinda arudishe makundi yote pamoja na kusonga mbele.

Tanzania inahitaji sana uwepo wa vyama vya siasa vyenye nguvu ili kuwa na ustawi.
 
Kwa akili ya Lissu hana akili wala busara ya kuvunja makundi. Busara hiyo na akili hiyo angelikuwa nayo, asingelipingwa vikali na viongozi wenzake wanaomfahamu nje ndani!
 
Back
Top Bottom