Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 46,405
- 138,158
Hii kesi Mbowe amefutiwa kwa huruma ya viongozi wa dini baada ya kumlilia na kumwangukia Rais Samia aingilie uhuru wa mahakama.
Siyakuzi na wala sina hayo mamlaka. Sina hata ndugu uvccm.
Hoja ni kwamba mfumo wetu wa utendaji haki kwenye jinai upo vizuri?
DPP angeamua kuifuta hii kesi kabla mahakama haijasema wana kesi ya kujibu, ilikuwa logical kwamba upelelezi na ushahidi aliopelekewa na polisi ameona haujitoshelezi. Sasa mahakama ilishathibitisha kwamba ushahidi dhidi ya mashitaka unajitosheleza ndiyo maana ikawataka walete utetezi wao kuiconvice kinyume chake. Sasa hoja ya DPP Kusema hana nia ya kuendelea na kesi ni ipi?
Siku moja tutajua tu kwamba hii katiba tuliyonayo ni famba.
Hii kesi angekuwa ameshatakiwa Neema kandambili kwa mchongo huuhuu angefungwa vizurii kabisa.
Ni jambo la kushukuru Mbowe kajitoa muhanga kwa ajili ya wengi. Naamini baada ya hii kesi ya mchongo,baadhi ya sheria mbovu mbovu kama hizi za kuwakata watu na kuwabambikizia kesi, zitafumuliwa kwa manufaa ya umma.