ATCL anzisheni safari ya Dar Mwanza Entebbe

Masanja Maguzu

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
547
Reaction score
396
Kwanza naanza kutoa pongezi kwa ATCL kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuliweka hai shirika letu la ndege. Natoa pongezi pia kwa kuanza safari za nje ya nchi katika kupanua wigo wa huduma za ATCL. Kwa sasa ipo njia mpya ya Dar KIA Entebbe nawapongeza kwa hilo.

Napendekeza iwepo safari ya Dar Mwanza Entebbe Dar na abiria waruhusiwe kubeba mizigo isiyozidi 50kg na kilo zitakazozidi basi walipie kidogo, safari hii ikiwezekana basi iwe mara moja kwa wiki. Kwa sasa kuna Bus nne kila siku zinatoka Mwanza hadi Kampala na abiria walio wengi ni wafanyabiashara na watumishi wa mashirika ya dini na mashirikia ya umoja wa mataifa. Hivyo kuna abiria wasiopungua 1000 kwa wiki wanaosafiri kati ya Mwanza na Kampala lakini sidhani kama kuna abiria wanaofika mia wanaosafiri kutoka Moshi au Arusha kwenda Kampala.
 
Inapendeza Dar-Mwz-Ebb via Bkb kuna abiria wengi wanao connect kampala kwa kutokea Bkb tena hiyo safari sio zaidi ya masaa ma wili paka EBB.
 
Inapendeza Dar-Mwz-Ebb via Bkb kuna abiria wengi wanao connect kampala kwa kutokea Bkb tena hiyo safari sio zaidi ya masaa ma wili paka EBB.
Nikweli tuweke pia Bombardier moja iwe inatoka Mwanza Bukoba Entebbe, inasubiria abiria wanaoshuka na Dreamliner wanaunganisha kwenda Bukoba au Entebbe. Wakati wakurudi inawahi ili abiria wa Entebbe wanaokwenda Dar wanaunganisha usafiri Mwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…