Masanja Maguzu
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 547
- 396
Kwanza naanza kutoa pongezi kwa ATCL kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuliweka hai shirika letu la ndege. Natoa pongezi pia kwa kuanza safari za nje ya nchi katika kupanua wigo wa huduma za ATCL. Kwa sasa ipo njia mpya ya Dar KIA Entebbe nawapongeza kwa hilo.
Napendekeza iwepo safari ya Dar Mwanza Entebbe Dar na abiria waruhusiwe kubeba mizigo isiyozidi 50kg na kilo zitakazozidi basi walipie kidogo, safari hii ikiwezekana basi iwe mara moja kwa wiki. Kwa sasa kuna Bus nne kila siku zinatoka Mwanza hadi Kampala na abiria walio wengi ni wafanyabiashara na watumishi wa mashirika ya dini na mashirikia ya umoja wa mataifa. Hivyo kuna abiria wasiopungua 1000 kwa wiki wanaosafiri kati ya Mwanza na Kampala lakini sidhani kama kuna abiria wanaofika mia wanaosafiri kutoka Moshi au Arusha kwenda Kampala.