ATCL bado hawajajipanga vizuri

Airline nyingine huwezi kuona captain anaweka kijiwe na cabin crews! Sana sana ndege ikiwa angani utamuona anaenda maliwatoni na kurudi kwao.

Hujajibu captain haruhusiwi kuzungumza na cabin Crew? Madhara yake ni nini? Ni kinyume cha policy?
 
Shirika la makada na machawa wao kupiga hela za bure, ndege zikifa wanasubiri JPM mwingine aje azinunue huku wenyewe hawana ujanja.
 
sasa mkuu mbona pointi mosi haina maana ...kwani wahudumu we wanakukwaza nini wakati ulichofata ni usafiri tu. anyway vp na ndege wangekua wanaangalia sura kama unavyowatazama wahudumu ..na sura lako bovu ungepanda ndege kweli
 
kwa mana kiswahili wamekikwepa? dah halafu unaweza kutu mtu analalmika kubauguliwa wakati tulishaanza kujibagua sisi wenyewe
 
Atcl gharama zao ziko juu mno juzi nimekata tiketi ya kwenda mwanza na kurudi dar 437x2
 
sasa mkuu mbona pointi mosi haina maana ...kwani wahudumu we wanakukwaza nini wakati ulichofata ni usafiri tu. anyway vp na ndege wangekua wanaangalia sura kama unavyowatazama wahudumu ..na sura lako bovu ungepanda ndege kweli
Bus la Kimbinyiko wameweza kuajiri wahudumu wazuri.Ajira za ATCL vimemo vimetawala ndio maana tuna wahudumu wana matumbo makubwa kama wanywa togwa.
 
Tumeshindwa kuendesha BRT tu, unafikiri tutaweza kuendesha Shirika la ndege la Kimataifa, bora apewe Bakhresa aliendeshe hilo shirika, litanfa kazi vyema kabisa.
 
Subiria ripoti ya CAG itakuwa yenye maumivu makali kuliko kudondokewa kufuli mguuni. Wanayafanya ayo yote Kwa sababu zikipungua wanachota kwenye kapu na kujazia mkuu
 
Kati ya ndege 14 zilizonunuliwa ni kumi tu zinazoweza kuwa angani kama hazina hitilafu za dharula. Uhalisia ni ndege 6 au 7 zinatumika sasa. Inashangaza jinsi kampuni yetu ya ndege inavyokimbilia safari za nje wakati hizi za ndani hawajazimudu.
Kwa nini hakuna ndege inayoruka kati ya Dodoma-Mwanza? Kigoma? Mbeya?
Kwa nini hakuna ndege inayoruka kati ya Kigoma-Mbeya? Mwanza? 😳 😳
 
Shukrani kwa bandiko lako kwenye mashiko ndugu, ubarikiwe. Kwa uzoefu wako, ni ndege gani Ina gharama stahimili; kutoka Dar to Dubai?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…