[emoji23] nimesoma huu uzi nikacheka kweli.
1. Kwani ni lini ndege haikua salama? Kipindi chote tangia izuiwe na mahakama imelindwa na serikali ya SA hadi ilipoachiwa na imerudi salama.
2. Hao "abiria wetu" sio kwamba wameacha kwenda SA...ni kwamba hela yao badala ya kuingia ATCL imeenda SAA, KQ, Rwandair, Ethiopian, malawai airlines na wengine ambao bado wanaruka kwenda huko.
3. Kama mnasubiri "maandishi" ya serikali ya SA mnaweza mkasubiri sana...maana ATCL inavyozidi kutoruka kwenda SA basi shirika lao linaneemeka zaidi.
Mimi nadhani huu uamuzi ulifanywa kwa kukurupuka na kwa hasira na sio kwa kuzingatia principle za biashara. Actually ATCL walikua wameshadhamiria kuendelea na safari za SA baada ya ndege kuachiwa na walikua wameshatangaza hivyo kwenye insta...lakini simu ikatoka "juu" ya kutengua huo uamuzi. Kusema kweli kama shirila letu litaendeshwa kwa namna hii halitafanikiwa...menejmenti ingeachiwa ifanye haya maamuzi na serikali isiingilie. Waangalia namna ambavyo serikali ya Ethiopia inavyoendesha shirika lao la ndege..hutasikia hata siku moja eti waziri anaamua kusitisha route.